Kesi ya Karamagi yafutwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Karamagi yafutwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Aug 3, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,375
  Likes Received: 5,660
  Trophy Points: 280
  Kesi ya Karamagi yafutwa


  Na Rabia Bakari

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imefuta kesi ya wizi iliyokuwa ikimkabili Bi. Nadya Karamagi, baada mlalamikaji katika kesi hiyo Bi. Maselina Rweyemamu, kuwasilisha barua ya maombi ya kufuta kesi.

  Akitoa uamuzi wa kufuta kesi hiyo, Hakimu Mkuu Mkazi, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Bw. John Msafiri, alisema kuwa kesi hiyo imefutwa chini ya kifungu cha sheria namba 224 cha mwenendo wa makosa ya jinai (CPA).

  Katika kesi ya msingi iliyokuwa ikikambili Bi. Karamagi ambaye ni raia wa Urusi, ilidaiwa kuwa Juni 17 mwaka huu katika maeneo ya Osterbay Kinondoni, aliiba simu na cheni ya dhahabu vyote vikiwa na thamani ya sh. 245,000 mali ya mlalamikaji.

  Awali, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama aliiomba mahakama kumnyima dhamana mtuhumiwa kwa kuwa si raia wa Tanzania au awasilishe hati ya kusafiria mahakamani hapo, masharti ambayo mtuhumiwa aliyakamilisha na hatimaye kupewa dhamana.

  Wakati wa kufuta kesi hiyo, Bw. Sisiwaya alisema kuwa upande wa mashtaka hauna pingamizi na ombi la mlalamikaji kwani amekubali kuyamalizia nyumbani.
   
Loading...