Kesi ya IGP Mahita na tuhuma za kuzaa na mtumishi wake wa ndani

Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,657
3,035
I was thinking people like IGPs should be different, at least ... repect!

-------------------------

House girl sues Mahita over child upkeep

FAUSTINE KAPAMA

Daily News; Wednesday,September 27, 2006 @00:07


A house girl, Ms Rehema Shaban, has filed a suit in which she wants to collect maintenance allowances from the former Inspector General of Police (IGP), Mr Omar Mahita, whom she claims is the father of her eight-year-old child.

In the civil case, which comes up for mention before Principal Resident Magistrate Pellagia Khaday at the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam this morning, Rehema would ask the court to declare the then IGP the putative father of the boy (name withheld).

She further wants the court to order Mr Mahita to provide 100,000/- monthly as maintenance allowances until the boy attains adult age and completes his studies.

According to the house girl, Mr Mahita (respondent) should also be ordered to pay maintenance fees that the former IGP had allegedly not paid to the former at the rate of the said 100,000/- since 1997 up to the day of determination of the case.

In her affidavit to support the application, Rehema has alleged that she had extra marital affairs with the respondent from May 1996 up to October the same year, when she was working with him as a house girl in Moshi, Kilimanjaro Region, when the respondent was the regional police commander (RPC).

In the course of their relationship, she claims, she conceived in 1996 and duly informed her employer about it. However, according to her, the latter advised her to go back home at Kondoa for fear of his wife knowing. She says that on that day, Mahita gave her 40,000/-, promising that he would be providing the required allowance every month.

Rehema claims that at no material time had Mr Mahita denied being responsible for putting her in the family way. The house girl claims in her affidavit that she gave birth in 1997, adding that he had accepted the child and promised that he would continue providing the allowances.

However, the house girl claims, the respondent prohibited her from going to either his office or home to collect the allowances. She alleges that at first it was plain sailing as she did not get any problems in taking care of the child before 2003 as Mr Mahita had been giving her some money whenever she visited him.

She further claims that the situation turned sour at the end of 2003 when she went to visit the house of the respondent at Ukonga in Dar es Salaam. According to her, members of the Field Force Unit (FFU) of the police force, who were guarding the house, denied her access ''probably on instructions from their boss''.


The house girl charges that she tried to talk to the respondent on the matter several times to no avail. She alledges that within the same year, the latter decided to send an FFU member, Peter, and a house boy, Hussein, who took the baby boy to an undisclosed place without her consent.


After deciding to make follow up on the whereabouts of his son, she claimed, she ended up at the Central Police Station in the city after being accused of committing a crime. She further alleges that she was later taken to the house of Sheikh Yahya who was taking care of the baby.

''Since then, I never got access to the child until April this year when Sheikh Yahya brought the baby to me,'' she claims in the affidavit.

Rehema concludes that she decided to go to court after all efforts to reach a solution, including seeking the help of the social welfare department failed her.
 
Last edited by a moderator:
Mahita adaiwa kumtia mimba hausigeli wake

  • Tayari mtoto keshazaliwa
  • Adaiwa kukwepa kumtunza
  • Anasimama leo kizimbani Kisutu

na Irene Mark

MKUU wa Jeshi la Polisi mstaafu, Inspekta Jenerali Omari Mahita (Ngunguri), leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akituhumiwa kumtia mimba yaya wake, kuzaa naye na kisha kukataa kutoa fedha za matunzo.

Mahita anadaiwa kuzaa na binti huyo miaka minane iliyopita.

Kesi hiyo ya madai namba 2/2006 ilifunguliwa Agosti 10, mwaka huu mahakamani hapo na Rehema Shaabani, kwa msaada wa Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu.

Uamuzi huo ulitokana na IGP huyo mstaafu kushindwa kumhudumia mtoto huyo kwa miaka yote, na juhudi za usuluhishi kushindikana.

Mahita katika kesi hiyo anatetewa na wakili wa kujitegemea aliyejulikana kwa jina moja la Semigalawa.

Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Pellagia Khaday.

Kwa mujibu wa hati ya madai, mlalamikaji, anaiomba Mahakama imtambue Mahita kama baba halisi wa mtoto wake, na imwamuru kulipa matunzo ya sh 100,000 kila mwezi kuanzia mwaka 1997, mwaka ambao mlalamikaji alijifungua.

Hati hiyo ya kiapo inaeleza kwamba uhusiano wa kimapenzi kati ya Mahita na yaya wake ulianza Mei 1996 hadi Oktoba 1996, wakati huo Mahita akiwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Kilimanjaro.

Mlalamikaji anadai kuwa, wakiwa katika uhusiano huo wa kimapenzi, alipata ujauzito. Mdaiwa alimpa sh 40,000 na kumshauri arudi kwao Kondoa, ili mke wa ndoa wa Mahita (ambaye sasa ni marehemu), asifahamu kilichokuwa kikiendelea.

Mlalamikaji anasema kuwa makubaliano hayo yalifikiwa kwa masharti ya kumtaka Mahita amhuhudumie mtoto atakayezaliwa.

Mtoto alizaliwa mwaka 1997 na kupewa jina la Juma, baba wa mtoto (Mahita), na aliahidi kutoa matunzo.

Inadaiwa kwamba hakuna siku ambayo Mahita aliwahi kumkana mtoto huyo.

“Alinikataza kumfuata ofisini na nyumbani kumdai matunzo ya mtoto,” inaeleza sehemu ya hati ya kiapo cha yaya huyo.

Anadai kuwa juhudi za mdai huyo za kutaka usuluhishi wa suala hilo ziligonga mwamba baada ya Mahita, kukaidi amri za kuitwa kwenye ofisi za ustawi wa jamii na mabaraza mbalimbali tangu mwaka 2003.

Hali hiyo ilisababisha mlalamikaji kufikia uamuzi wa kutafuta msaada wa kisheria na kufungua kesi.

Hati hiyo ya kiapo ilieleza kwamba, Mahita, alimtuma askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, aliyejulikana kwa jina la Peter, na mfanyakazi wake mvulana aliyetajwa kwa jina la Hussein, ambao walimchukua mtoto na kumpeleka kusikojulikana.

Mdai aliamua kufuatilia aliko mtoto huyo, na alikamatwa na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, na kubambikiwa makosa asiyoyafahamu.

Baada ya kukaa rumande kwa siku kadhaa, watu anaoamini kuwa walitumwa na Mahita, walimchukua na kumpeleka katika nyumba iliyopo Mkwajuni kwa Sheikh Yahaya, na kufanikiwa kumwona mtoto wake.

Mdai anasema tangu wakati huo, hajamwona tena mtoto huyo, na kwa sababu hiyo, anataka arudishiwe mwanawe, na alipwe kiasi cha fedha alichokitumia kwa matunzo kwa muda wote aliokuwa naye.

Kesi hiyo inatarajiwa kuvuta hisia za wengi, hasa wanaharakati wa haki za wanawake na watoto.
 
mbona hilo siyo geni! RPC mmoja hivi aliwahi kuwa Arusha baadaye Kigoma... alizaa na Secretary wake... huku akiwa ana mke na watoto... waangalie wasije kuwa wanafungua kisanduku cha pandora! Asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe!!
 
<< Nimeondoa link ya picha ya huyu mtoto .. ikiwa ni kuunga mkono maoni ya wanabodi hapo chini >>

An eight-year-old boy, Juma (left), claimed to be son of former Inspector General of Police Omari Mahita sits besides his mother, Rehema Shaaban, at the Kisutu resident Magistrate's court in Dar es Salaam yesterday. (Photo by Faraja Jube)

Source: Daily news
 
thats when ma paternity test comes to play. Chukua DNA ya Mahita ya mama, na mtoto. Run PCR hapo mzee tuone vitu. The kid looks Mahita's to me.

resize_imagefront.php
 
Wanabodi,

Nimesikitishwa sana na kitendo cha waandishi wa habari wetu uchwara wa hapo bongo kwa kubandika picha za huyu mtoto kwenye kila gazeti . Jamani huyu mtoto ni " Innocent " kwa nini tumuingize kwenye haya matatizo ? Jee wameangalia ni matatizo gani yatamkuta kwenye siku za usoni especially kutaniwa na wenzake akiwa . Kusema ukweli kitendo hiki kitamuathiri huyu mtoto kimaomo na kisaikolojia .
 
Hayo ya viongozi kutokuwa waaminifu ktk ndoa zao mbona mambo ya kawaida kuyasikia jamani! Mmesahau ya Makamu wa Rais-Zuma SA! Ila inasikitisha wasivyojipenda, wanafanya mapenzi nje ya ndoa bila kinga "kondomu" hilo la secretary sio noma saaana kama hili la housegirl, na yaonesha alimlanghai kuwa atamfukuza kazi kama hatampa tunda, wakati huo rehema bado kabinti kadogo maskini!

By the way, kwanini hili swala liibuke sasa? hapa pana support toka pahala fulani, na huyo mama nahakika amesha wini hii kesi, kwani hata shekhe Yahya amekiri kuwa alikabidhiwa mtoto na Mahita ati amfundishe Quruani (Je Kwa YAHYA kuna boarding School???) Kaaaziii kweeeeli kweeeli!

........................
:U Can't Change The Nature:
 
Rufiji,

Nakubaliana nawe kabisa kuwa ilikuwa sio sahihi kuweka picha ya huyo mtoto kwenye gazeti.Vyombo vyetu vya habari vimekuwa vikipuuza sana haki za watoto (na hata akinamama) hususan panapokuwa na matukio kama ya ubakaji,unyanyaswaji kijinsia na kutelekezwa.Pengine nia yao ilikuwa nzuri (hata mtaalamu wa DNA anaweza kudhani wanataka kumpotezea muda kwa jinsi mtoto alivyo kopiraiti na ngunguri) lakini walipaswa kujua kuwa wanaweza kumsababishia usumbufu mkubwa mtoto huyo katika siku za mbeleni.

Mr Clean,kwa mawazo yangu,nadhani suala hilo limeibuka sasa kwa vile Mahita hayuko madarakani.Ukiwa IGP ni kama Mungu-mtu kwa Bongo na si rahisi kesi dhidi yake ingeweza kutia mguu kwenye vyombo vya sheria.On the other hand,yayumkinika kusema kwamba Mahita alijitengenezea maadui wengi tu wakati akiwa IGP:maadui ambao pengine waliona amewaonea (ilhali yeye alikuwa anatekeleza tu majukumu yake) au wale ambao pengine kweli walionewa.Kwa sasa Mahita ni kama anaishi kwenye nyumba ya vioo huku amezungukwa na vichaa walioshika mawe (symbolically).

Inanikumbusha yalomkuta Lt Gen Imrani Kombe...
 
Naungana na Mlalahoi hapo juuu...
Binafsi naamini kuwa kuna watu nyuma ya mlalamikaji na hilo limesababisha ushabiki kiasi kwamba kanuni na maadili (kumwonyesha mtoto kwenye vyombo vya habari). Sidhani kama angekuwa Bw X au Y kesi ingekuwa na mvuto kiasi hicho na mpaka kutoa picha magazetini. Mbona kesi za namna hiyo ziko nyingi tu!?

Yote kwa yote, huenda kuanzia sasa kukawa na wimbi la kesi za namna hiyo dhidi ya waliokuwa vibosile kwenye awamu iliyopita, kama vile mawaziri, wabunge au ma-RPc waliotemwa!

Yangu masikio.
 
Na Ester Bulaya

MKUU wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali mstaafu Omar Mahita amemkana mtoto anayedaiwa kuzaa na aliyekuwa mtumishi wake wa ndani, Rehema Shaaban (36).

Kwa mujibu wa hati ya utetezi, aliyowasilisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kupitia wakili wake Charles Semgalawe, Mahita alimkana mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka minane (jina limehifadhiwa).

Mahita katika utetezi wake alidai kuwa mwaka 1996 hakuwa na mtumishi wa ndani kwa kuwa mlalamikaji Rehema alikuwa amekwishaacha kazi kwake tangu mwishoni mwa mwaka 1995.

Kwa mujibu wa hati ya utetezi huo, Mahita anadai kuwa, Rehema alikuwa mtumishi wake wa ndani kuanzia mwanzoni mwa mwaka 1995 hadi mwishoni mwa mwaka huo wakati alipokuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro.

Alidai kuwa mwaka 1996 alihamishiwa mkoa wa Arusha, na kwa kipindi hicho hakuwa na msichana wa kazi za ndani, kwani mlalamikaji alikuwa ameshaacha kazi mwishoni mwa mwaka 1995.

Utetezi huo unaeleza kuwa kwa kipindi hicho tangu mwaka 1995, hakuwahi kufanya mawasiliano na mlalamikaji, na kwamba ilipofika mwaka 2003 akiwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, mlalamikaji alikwenda kufanya fujo nyumbani kwake barabara ya Bongoyo, Oysterbay, Dar es Salaam, kwa madai kuwa amemzalisha, hivyo aliwaamuru askari wamfukuze.

Aliendelea kudai kuwa baada ya kufukuzwa, Rehema alikwenda Ukonga kwa dada wa Mahita na kumbwaga mtoto huyo bila ya kujitambulisha wala kutoa maelezo yoyote.

Kwa mujibu wa hati ya utetezi, Mahita alidai kuwa baada ya kuona hivyo alipatwa na huruma kama wengine dhidi ya mtoto, hivyo alimchukua na kumpeleka kwa Sheikh Yahya Kinondoni, Mkwajuni, ili ajifunze Kuran Tukufu, na si kwamba alikubali kuwa wake na wala si kwa lengo la kumficha, kama ilivyodaiwa na mlalamikaji.

Rehema alifungua kesi hiyo ya madai Agosti 10, mwaka huu, akidai kupewa ujauzito na Mahita kisha kumtelekeza ambapo katika madai ya msingi anaiomba mahakama itamke kuwa Mahita ni baba halali wa mtoto huyo.

Pia, anaiomba mahakama itoe amri ya kumtaka Mahita kulipa sh. 100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto.

Pia, mahakama imwamuru kulipa kiasi hicho cha fedha tangu mtoto huyo alipozaliwa mwaka 1997 hadi kesi hiyo itakapomalizika, sambamba na gharama za kufungua kesi hiyo. Kesi hiyo inatarajia kuanza kusikilizwa leo.
 
Wooow! I mean busara inakataa kuwa something is not right, pamoja na Mzee Mahita kujaribu kujitetea na kujaribu kuwa convincing lakini damn! yaani mwanamke anaweza tu kukurupuka na kudai kuwa anmempa mimba?

Hapana Mzee Mahita, na power yote ya polisi aliyokuwa nayo then ya kuvuruga maanadamano akashindwa kuwaaamuru polisi wamrudishe mtoto huyo kwa mama yake? Mbona haaingiii akilini?

Hivi jamani vipi huku bongo hatuna DNA test, ili kukata mzizi wa fitina?
 
Kupenda ngono huko - hata na mahouse girl mnaotakiwa kuwaona kama ndugu kama si watoto wenu. Hizi ni laana. Je Mahita yu peke yake kwenye hili au ni kuwa tu wengine hawajashikwa kama yeye?
 
Huo ndo ukweli Jizalendo hii tabia imezidi mpaka kupitiliza.Tumtumie Mahita km mfano kwa wengine km yeye ambao ni wengi! Hana pa kukimbilia mambo hadharani!
 
Mahita uzinzi ulianza zamani hivi kama ungalizaa na yule mdada wa Diamond Motors naye ungalikataa mtoto ama kwa vile huyu ni Yaya na wa Diamond motors ni Sec ?Ukipenda ngono pende pia madhara yake ambayo sasa mdhara kwako ni mtoto hata kuangalia masiko kama sungura yamesimama na sura lako baya kwa mtoto huyu umeliacha .
 
Ninachoweza kusema hapa hii kesi imeshaisha. Kuna vitu viwili lazima vieleweka haki na sheria. Kwenye hati ya kiapo alisema kwamba uhusiano wa kimapenzi kati ya Mahita na yeye ulianza Mei 1996 hadi Oktoba 1996, wakati huo Mahita akiwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Kilimanjaro. Don't you think this case is over hata kama kweli huyu ni mtoto wa Mahita? Je mahakama zetu zinachukua vipimo vya DNA? Mahita aliteuliwa kuwa IGP Mei 1996 akitokea Arusha siyo Kilimanjaro. Labda aishawishi mahakama kuwa alikuwa na mimba ya miaka miwili. Na hao watu wanaomsaidia huyo mama kwenye kesi naona vichwa vyao na siyo vizuri hata kufikiri hawawezi jinsi ya kuitengeneza kesi. Unapo mshitaki mtu mwenye status ya Mahita lazima uwe na ushahidi ulioenda shule. Inawezekama kweli mtoto ni wa Mahita kama anavyoonekana kwenye picha anafanana naye lakini kesi imeishaisha
.
 
Mliiona picha ya yule mtoto? Masikio ni copy cat ya Mahita, hata umbo la kichwa. Hawezi kumkana.
 
Yule mtoto ni Mahita mtupu.

Na kama si mtoto wake kule kwa Yahaya Hussein alimpeleka akafanye nini.

Mnakataa watoto halafu wakiwageuka wanapokuwa watu wazima mnajitia kuwaachia radhi!!
 
Back
Top Bottom