Kesi ya IGP Mahita na tuhuma za kuzaa na mtumishi wake wa ndani

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Messages
3,699
Points
1,500

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined May 9, 2007
3,699 1,500
Yule mwanamke anayedai kuzaa na IGP mstaafu Omary Mahita amewaomba wasamaria wema kumsaidia fedha kwa ajili ya kupima DNA ili kumaliza utata kuhusu uhalali wa Mahita kuwa ndiye Baba mzazi wa mtoto, ambaye Mahita anakana kuwa siye baba mzazi. Wana JF hili mnalionaje?
 

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
98,025
Points
2,000

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
98,025 2,000
Mahita akwepa kupima DNA, Ni sakata la mtoto
Tuesday, 12 May 2009 16:36
Na Kulwa Mzee
Majira

ALIYEKUWA Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Omari Mahita amekaidi amri ya Mahakama kwa kukosa kwenda kupima DNA ili kubaini kama mtoto Juma Omari Mahita ni wake au la.

Taarifa ya kukaidi amri hiyo iliwasilishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam ikitokea kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Bw. Mahita alitakiwa kufanya hivyo na mahakama hiyo ili kuondoa utata uliopo kati yake na mama wa mtoto huyo, Bi. Rehema Shabani anayedai kuzaa na Bw. Mahita wakati Bw. Mahita mwenyewe akikanusha madai hayo.

Kwa mujibu wa barua kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bi. Rehema na mwanae Juma walifika katika ofisi hizo Aprili 24, 27 na 30 mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza amri ya mahakama, lakini Bw. Mahita hakufanya hivyo.

Mbali na tarehe hizo pia mlalamikaji katika kesi hiyo Bi. Rehema alifika ofisi za Mkemia huyo Mei 4 na 5 mwaka huu na mdaiwa bado hakuonekana.

Amri ya mahakama ilitolewa Aprili 24 mwaka huu ikiwataka wahusika kwenda kufanya kipimo hicho pamoja na mtoto anayebishaniwa.

Katika kesi ya msingi Bi. Rehema anaiomba mahakama kutamka kuwa Bw. Mahita ndiye baba wa mtoto Juma.

Kesi hiyo ilitajwa Mei 7 mwaka huu na kupangwa kutajwa tena Juni 16 mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuangalia kwa nini mdaiwa hakutekeleza amri ya Mahakama.
 

Shadow

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2008
Messages
2,904
Points
1,225

Shadow

JF-Expert Member
Joined May 19, 2008
2,904 1,225
Kinatolewa kibali cha kumkamata! kwa lugha nyingine angepaswa kuwa amekamatwa ama anatafutwa.. in case haonekani.
Tanzania ni sawa na hadithi ya shamba la wanyama kwamba kuna wanyama walio na haki zaidi kuliko wengine(my literal translation).

Kuna sheria ya kukimbizana na walalahoi wakati wanene wanabembelezwa...hitimisho langu ni kutokana na hiyo habari hapo juu kwa mahakama kushindwa kutoa hati ya kumkamata Mahita kwa kukaidi amri halali ya mahakama unless hakimu hajui wajibu na mamlaka aliyo nayo.
 

Bluray

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2008
Messages
3,456
Points
1,225

Bluray

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2008
3,456 1,225
Kukataa kupima DNA maana yake moja tu, anajua kwamba yeye ndiye baba.

Mtu gani anaweza kumkataa mwanawe mwenyewe? the lowest scum of the earth!
 

Swahilian

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2009
Messages
589
Points
195

Swahilian

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2009
589 195
Tatizo ndo hiloo, iwapo yule mtoto labda angekuwa ndo anatakiwa baba baada ya kuwa na kipawa au umahiri wa kitu fulani basi hakika kina MA HEATER wangejitokeza wengi sana, lakini kwakuwa mama ni house call, dhofu lhali, basi hajaliwi, jamani acheni kabisaa na hata mmoja wetu asije kufanya, walofanya mjirudi ! malipo ni hapahapa! watu kama 2pac,Tyson, Yellowman yaliwakuta haya lakini badaye, watu walitamani damu zao zifanane bt it woz late n' far!
 

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2007
Messages
16,593
Points
1,500

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2007
16,593 1,500
Tena hata huyo mtoto wenyewe inawezekana alipatikana ktk kitendo cha ubakaji au unyanyasaji wa kijinsia..Chances are very high here, sema ndio hivyo huyu mama anachojali ni mstakabali tu wa mtoto wake, mengine anamwachia Mola.the dude is an evil bastard!
 

Kamuna

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2009
Messages
298
Points
195

Kamuna

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2009
298 195
Sheria zinaheshimika USA hata uwe Jemadari siju wa vitu gani, akiboringa unashughulikiwa!Mnaofuatilia habari mnafahamu habari za seneta wa Ilinois Bwana Blagojavic ameshaonja joto ya sheria.Cant we learn something from there!
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,308
Points
2,000

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,308 2,000

Tuesday, July 21, 2009 9:31 AM
KESI ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Omari Mahita ambayo alifunguliwa na hausigeli wake akidaiwa kumtia mimba na kumtelekeza itaanzwa kusikilizwa Julai 29 mwaka huu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ya jijini Dar es Salaam Kesi hiyo ilitakiwa ianzwe kusikilizwa jana kwa utetezi wa kawaida lakini iligonga mwamba kusikilizwa kwa kukosekana kwa wakili wa mshitakiwa mahakamani.

Kesi hiyo iliahirishwa kwa kuwa wakili wa mshitakiwa alikuwa na kesi nyingine Mahakama Kuu hadi kupelekea kuahirishwa kwa kesi hiyo.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Suzan Kihamo alisema kuwa kesi hiyo itarudi Julai 29, mwaka huu, kwa ajili ya kusikiliza utetezi mahakamani hapo.

Awali Omari Mahita alifikishwa mahakamani hapo Septemba 27, mwaka juzi, kwa kufunguliwa mashitaka na aliyekuwa msichana wake wa kazi za ndani Rehema Shabani kwa kumtelekeza na mtoto aliyemzalisha.

Rehema alifungua mashitaka mahakamani hapo akidai kuwa Mahita alimtelekeza na mtoto aliyemzalisha aliyefahamika kwa jina Juma Mahita wakati akifanya kazi nyumbani hapo.

Rehema alifungua mashitaka katika mahakama ya Kinondoni kutaka Mahita amuhudumie yeye pamoja na mtoto ambaye alimpa mimba wakati akifanya kazi za ndani nyumbani kwake.
http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2577738&&Cat=1
 

nkawa

Senior Member
Joined
May 11, 2009
Messages
181
Points
0

nkawa

Senior Member
Joined May 11, 2009
181 0
Kwa mazingira gani huyu msichana wa kazi aliipata mimba? Alibakwa au kwa hiari yake mwenyewe?
Kaenda kufanya kazi za ndani nyumbani ndio hadi za ndani chumbani!!!!
 

Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
3,183
Points
1,170

Junius

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
3,183 1,170
Pengine Mahita hajafanya hasa hayo mambo lakini, Mw'Mungu anamfedhehesha tu kutokana na ubabe na uhuni na mauwaji ya watu wasio na hatia alipokuwa IGP
 

Mtimti

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2008
Messages
934
Points
250

Mtimti

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2008
934 250
Pengine Mahita hajafanya hasa hayo mambo lakini, Mw'Mungu anamfedhehesha tu kutokana na ubabe na uhuni na mauwaji ya watu wasio na hatia alipokuwa IGP
kaka,hiyo kesi haijaanza leo,kwa jinsi ushahidi ulivyokuwa unatolewa na huyo binti pamoja na mahita jinsi alivyokuwa anajitetea utaona kabisa kuwa mahita ndie baba wa mtoto.
mahita aliiomba mahakama iyatupe hayo mashtaka lakini mahakama ilipomwambia achukuliwe DNA ili wakate mzizi wa fitina mahita akachomoa kuchukuliwa,sasa mahita ana uhakika kuwa yule mtoto si wake na anataka hiyo kesi iishe kwanini asikubali kuchukuliwa DNA?TAFAKARI
 

Forum statistics

Threads 1,382,687
Members 526,441
Posts 33,833,874
Top