Kesi ya Halmashauri ya Arusha Mjini Dhidi ya Morris Makoi diwani wa CCM Moshi

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,739
-Kesi ya Halmashauri dhidi ya Moris Makoi(diwani wa Moshi Vijijini)inaendelea katika mahakama ya Ardhi hapa Arusha.

Makoi amefungua kesi akipinga Halmashauri kuchukua jengo lake la ghorofa lililopo stendi ndogo (viyumba 27) pamoja na choo,ambavyo hakuwahi kulipia ushuru wa pango tangu 2005.

Kesi inaendelea hapa Mh Meya,Mh James,Mh Paul na mimi wapo ndani wanafuatilia kesi kwa makini.

- Mwanasheria wao anaomba Interim Injections kwa kuwa walifanya renovations

- Na walijenga maduka kuzunguka choo

- Kwamba mahakama izuie Halmashauri kukusanya mapato (pango) hadi kesi ya msingi isikilizwe

- Pamoja na kuwa mkataba wao wa miaka kumi yaani 2005 hadi 2015 umeshaisha ile eti gharama zao hazijaisha.Licha ya kuwa kwa miaka kumi alikaa bure kabisa

- So mahakama iamuru halmashauri isimsumbue yeye wala wapangaji wake

- Sasa ni mwanasheria wa jiji anaanza kujibu hoja zao

- Kwamba mkataba umeisha Jan 12,mwaka huu.So wakati kesi ikiletwa mahakamani tayari mkataba ulishaisha na choo kipo chini ya halmashauri

- Kwa hiyo halmashauri haina uhusiano wowote wa na mlalamikaji

- Kuhusu renovation; Kwamba kwenye mkataba wake,Wakala hatopangisha,hatofanya ukarabati,au hatompa mtu mwingine yeyote bila kibali cha maandishi kutoka Halimashauri

- Mkataba wa miaka kumi ulimtaka yeye Makoi kuomba upya miezi 6 kabla ya mkataba kuisha

- Lakini halmashauri hailazimiki kumpa yeye bali sheria ya manunuzi ya umma ndio ingefuatwa kwa kutangazwa kwa njia ya tenda

- Hivyo hakuna automatic renewal ya mkataba hivyo Makoi hana chake at all

- Kuhusu injection

-Ni kinyume cha sheria kuzua halimashauri kukusanya ushuru wake kwa ajili ya interest ya individual

-Mwanasheria wetu ananukuu kesi flani hivi

-Interim order will paralyise the municipality
 
Mkataba wake ulikuwa wa 72mil hadi sasa ameshapata zaidi ya 1bil

Moris alikuwa mwenyekiti wa halimashauri ya Moshi vijijini

ana makampuni mengi kama
Mkomilo
Ngulelo
Makumira filling stations
Baraki printers
Aquiliner
Etc
 
Walizoea kula kwa dhuluma mwisho wao umefika huyu Diwani wa CCM alishazoea kula pesa za dhuluma mahakama itatoa hukumu jumanne kuanzia saa mbili asubuhi .Asante kwa taarifa mkuu Crashwise
 
Mkataba wake ulikuwa wa 72mil hadi sasa ameshapata zaidi ya 1bil

Moris alikuwa mwenyekiti wa halimashauri ya Moshi vijijini

ana makampuni mengi kama
Mkomilo
Ngulelo
Makumira filling stations
Baraki printers
Aquiliner
Etc
Aisee kwenye ile list ya matajiri wa kaskazini anapaswa kuwepo
 
Morisi ni diwani wetu wa kata ya okaon moshi vijijini, na sasa kabomoa nyumba yake kapandisha gorofa kali pale kijijin mkomilo.

Jamaa elim yake ni darasa la saba lakini pesa ndiyo imemfanya akawa mwenyekiti wa halmashauri ya ya moshi vijijin 2010-2015 ambapo ndipo alipojipatia mapesa ya kununua mashamba na majumba arusha na moshi.

Jamaa ni jipu ambalo linabidi litumbuliwe
 
Ccm na majipu ni sawa na nzi na kinyesi
 
Mkataba wake ulikuwa wa 72mil hadi sasa ameshapata zaidi ya 1bil

Moris alikuwa mwenyekiti wa halimashauri ya Moshi vijijini

ana makampuni mengi kama
Mkomilo
Ngulelo
Makumira filling stations
Baraki printers
Aquiliner
Etc
Makumira Filling station na Acquline hotel ni mali za Charles Makosi na siyo Moris Makoi
 
Tunataka Arusha yetu....huyu bwana katafuna sana ,halmashauri ndugu yake Gaudence lymo aleyekuwa mayor wa jiji alimkingia kifua... ....
 
Tunataka Arusha yetu....huyu bwana katafuna sana ,halmashauri ndugu yake Gaudence lymo aleyekuwa mayor wa jiji alimkingia kifua... ....
Wewe unapingana na "MKUKUTA"? maana serikali iliamua kubinafsisha ukusanyaji wa mapato kama nja ya kuwainua raia zake kiuchumi, sasa raia wamefanikiwa wewe unasema "wametafuta". Kasome SERA YA MKUKUTA vizuri
 
Nimesoma sera ya MKUKUTA ila sijaona mahali pameandikwa kuwa mtu atumia rasilimali ya,serekali bila kufuata sheria...huyu bwana,alipewa miaka 10 leo mkataba umeisha anataka aendelee kutafuna pesa....ajinufaishe mwenyewe...
 
Huyu jamaa alikuwa anakusanya kodi kituo cha Mwenge, Ubungo stand ndogo, iliyopigwa chini, pia parking za Moshi na Arusha ilikuwa mali yake.. Nadhani mpaka sasa...

Achunguzwe kisawasawa..elimu yake ndogo tu, hana pa kutokea akikutana na wenye shule wakimchanganya-changanya anakaa chini....
 
Back
Top Bottom