Kesi ya Halima Mdee: Mkuu wa Upelelezi Ilala (RCO) Davis Msangi, adai hajui breki

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Heshima kwenu wakuu,

Leo Mahakama ya Kisutu kuliendelea kusikilizwa mwendelezo ya Mahojiano kati ya Kibatala na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Ilala (RCO), Davis Msangi.

Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa kuwa alifanya kosa hilo Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni. Anadaiwa kumtukana Rais John Magufuli kuwa “anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

kesi ya Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa kuwa alifanya kosa hilo Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.

Leo ilikuwa ni siku ya kumaliza Cross Examination hivyo RCO aliendelea kihojiwa.

Kibatala: Mara ya mwisho ulisema hufahamu msimamo wa bunge kuhusiana na kauli ya rais magufuli kuhusu mimba za mashuleni, je hadi leo hujafahamu?

Shahidi; Sifahamu

Kibatala: Tuchukulie alitamka hivo, je alirejea alichosema bungeni au ni maneno yake mwenyewe?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu kuhusu haki na wajibu wa bunge

Shahidi: sifahamu

Kibatala: Unafahamu mshitakiwa ni mbunge

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kama sehemu shughuli za kipelelezi aliwasaliana na spika wa Bunge kumjulisha kama Mdee amekamatwa?

Shahidi. Ndio kuhusu kukamatwa, Mkuu wa pelelezi wa mkoa wa kinondoni ndo alinipa barua nimpelekee spika.

Kibatala: Wewe ndo ulikiwa na
Mshtakiwa, je alikaa chini ya ulinzi kwa muda gani?

Shahidi: Masaa 48. Alifika tarehe 4.7. 2017 hakukaa zaidi ya masaa 48.

Kibatala: Mtuhumiwa anatakiwa apelekwe mahakamani baada ya muda gani?

Shahidi: Upelelezi ukikamilika.

Kibatala: Unafahamu mtuhumiwa anatakiwa apelekwe mahakamani ndani ya masaa 48

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Kama upelelezi haujakamilika polisi wanatakiwa waje waombe extension mahakamani ya kutomfikisha mtuhumiwa mahakamani, unafahamu?

Shahidi: Nafahamu.

Kibatala: Uliomba extension mahakamani?

Shahidi: Sikuomba

Kibatala: Sheria za polisi zinakuruhusu kumruhusu mtuhumiwa aende sehemu yoyote bila kujua anaenda kifanya nini?

Shahidi: Zinaniruhusu

Je kuna makabidhiano?

Ndio

Kibatala: Mshtakiwa alikamatwa saa kumi na mbili jioni, maelezo mlichukua saa ngapi?

Kuanzia saa mbili na nusu na kuendelea. Baadae alisema hatachukuliwa maelezo hadi wakili wake aje. Tukasubiri hadi kesho Wakili wake alipokuja.

Kibatala: Mulisema Halima Mdee amemuassault Magufuli, je ni assault kumtukana?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Unafahamu magufuli anaishi wapi?

Ndio, anaishi Ikulu.

Kibatala: Uliwahi kwenda kumhoji kama hili ni tusi au kama haya maneno yalimuuliza?

Shahidi: Sijawahi kwenda kumhoji.

Kibatala: Polisi mlishawahi fuata protokali ya kwenda kumhoji Magufuli ili kupata uhakika kama haya maneno yalimuumiza na kumkera?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Uliwahi kuandika barua ya appointment ya kuonana na rais juu ya hii kesi?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu Magufuli anajisikiaje kuhusu haya maneno

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu katiba ya tanzania inasema nini kuhusu haki ya elimu na kwamba Tanzania imeingia makubaliano ya kuwawezesha watoto wa kike kielimu

Shahidi:Ndio.. Kila mtu ana haki ya kupata elimu.

Kibatala: Kuna sehemu kwenye katiba imesema mtu akipata ujauzito asirudi shuleni?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Unafahamu hapa tanzania kuwa kuna watu wanaongea hovyo hovyo maswala ya kisheria kinyume na sheria?

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Abdul wa Clouds TV alipowapa huo ushahidi wa maneno, je Abdul na polisi mlifuata utaratibu wa makabidhiano ya clip?

Shahidi: Ndio tulifuata.

Hekima Mwasipu: Neno breki unafahamu lina maana gani?

Shahidi: Sifahamu.

Hekima Mwasipu: Ukiambiwa shika breki unajua maana yake?

Shahidi: Sijui hayo mambo ya breki anajua Dereva.

Hekima Mwasipu: Tafsiri ya neno hovyo hovyo unafshamu?

Shahidi: Ndio.

Hekima Mwasipu: Wewe ulikabidhiwa nini na Abdul kama ushahidi?

Shahidi: Nlikabidhiwa laptop

Hekima Mwasipu: Kwahiyo hiyo laptop ndo walitumia kurecord maneno?

Shahidi: hapana, walitumia tep recorder ila tulitumia laptop kuona kilicholekodiwa.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba:

Mpaka jana hii kesi ilikuwa imetimiza mwaka mmoja 10.7.2017 ndo ilifunguliwa. Tupo nyuma. Tujitahidi hii kesi iishe, upande wa jamhuri leteni mashahidi wote tumalize hii kesi hukumu itolewe. Sera ya mahakama ni kumaliza viporo mapema.

Naahilisha hii kesi hadi tarehe 7 na 9.08.2018 ndo kesi ya Halima itasikilizwa tena saa nne na nusu..

Mwisho.

Maelezo ya mahojiano ya kwanza kabla ya haya. Huu ulikuwa muendelezo.

Maelezo ya awali ilikuwa hivi;

Dar es Salaam. Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Ilala (RCO), Davis Msangi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alibaini maneno yaliyotamkwa na mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ni ya jinai wakati akiangalia mtandao wa kijamii wa you tube kupitia simu yake.



Msangi ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka aliyaeleza hayo Ijumaa Juni 29, 2018 wakati akitoa ushahidi katika kesi ya kutoa lugha ya matusi inayomkabili Mdee.



Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa kuwa alifanya kosa hilo Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.



Anadaiwa kumtukana Rais John Magufuli kuwa “anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.



Halima alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Julai 10, 2017.



Akiongozwa na wakili wa Serikali, Patrick Mwita kutoa ushahidi, Msangi amedai kuwa Aprili 2017 hadi Januari 2018 alikuwa mkuu wa upelelezi wilaya ya Kinondoni.



Shahidi huyo wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai kuwa Julai 4, 2017 alikuwa ofisini kwake na kupitia simu yake katika mtandao wa you tube aliona kichwa cha taarifa iliyoandikwa Magufuli afungwe breki.



Msangi amedai aliifungua na kuisikiliza maudhui ya ndani na kwamba yeye kama mlinzi wa amani aliona kuna jinai, kwamba alimuona Mdee akizungumza maneno hayo na alifuatilia na kutambua kuwa alikuwa katika mkutano na waandishi wa habari.



Alibainisha kuwa maudhui yalikuwa ni maneno kuongewa kwa sauti na kwamba kilichomfanya aone kuna jinai ni maneno yaliyoongelewa kuwa rais ana mambo ya ovyo ovyo anatakiwa afungwe breki.



Amebainisha kuwa baada ya kupata kipande cha video ya Mdee katika mkutano huo kutoka kwa Abdul, akatambua kuwa alichokiona you tube hakikuwa cha kutengeneza, hivyo kufungua jalada la uchunguzi.



Alidai kuwa baada ya kuipata video hiyo, aliituma kwa mtaalam wa matukio kutoka maabara ya kisayansi polisi makao makuu.



Msangi alihojiwa maswali na wakili wa Mdee, Peter Kibatala juu ya alichokieleza mahakamani.



Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 11, 2018 siku ambayo mashahidi wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi katika kesi hiyo.
 
Kibatala-je unafahamu kwamba magu yeye anachukulia poa tu na wala hana time na halima yeye yupo busy kuwashunghulikia wanaoikosoa ndege yake?
RCO-nafahamu Hilo jukumu kakabidhiwa Bashite mkuu wa kitengo cha watu wasiofahamika.

Kibatala-je unadhani hii kesi inatija kwa taifa?

RCO-Sifahamu.

Kibatala-unafkili ni kwanini wapinzani wamelundikiwa mashtaka mengi ya hovyo hovyo mahakamani?

RCO-Ni maagizo kutoka juu,maana tunajaribu kutumia mbinu za kagame.

Kibatala-unadhani watanzania wanafurahia wawakilishi wao kulundikiwa kesi na kushitakiwa kila Leo?

Rco-nadhani hawapendi ila ndio hivyo tena.

Kibatala-ukiwa kwenye gari yako,oficin na nyumbani kwako ni nyimbo gani hupendelea zaidi kuisikiliza?

RCO-CCM mbele kwa mbele.

kibatala-asante sana shaidi.

Rco-you're welcome.
 
Kibatala-je unafahamu kwamba magu yeye anachukulia poa tu na wala hana time na halima yeye yupo busy kuwashunhhulikia wanaoikosoa ndege yake?
RCO-nafahamu Hilo jukumu kakabidhiwa Bashir.

Kibatala-je unadhani hii kesi inatija?

RCO-Sifahamu.

Kibatala-unafkili ni kwanini wapinzani wamelundikiwa mashtaka mengi ya hovyo hovyo mahakamani?

RCO-Ni maagizo kutoka juu,maana tunajaribu kutumia mbinu za kagame.

Kibatala-unadhani watanzania wanafurahia wawakilishi wao kulundikiwa kesi na kushitakiwa kila Leo?

Rco-nadhani hawapendi ila ndio hivyo tena.

Kibatala-ukiwa kwenye gari yako,oficin na nyumbani kwako ni nyimbo gani hupendelea zaidi kuisikiliza?

RCO-CCM mbele kwa mbele.

kibatala-asante sana shaidi.

Rco-you're welcome.
Haaaaahaaaa
 
Ila wakishinda kesi mnasema mahakama inewapendelea
Twende taratibu jamaa anaulizwa : unamfahamu mshitakiwa kama ni mbunge? Anajibu sifahamu... Anaulizwa tena Unafahamu taratibu za kuwasiliana na bunge na mlizifuata wakati wa kumkamata mshitakiwa? Kwa kuwa amekariri swali la kwanza tuu hili la pili anajibu ndiyooo ....halafu ni afisa wa polisi huyo....
 
Kibatala-je unafahamu kwamba magu yeye anachukulia poa tu na wala hana time na halima yeye yupo busy kuwashunhhulikia wanaoikosoa ndege yake?
RCO-nafahamu Hilo jukumu kakabidhiwa Bashir.

Kibatala-je unadhani hii kesi inatija?

RCO-Sifahamu.

Kibatala-unafkili ni kwanini wapinzani wamelundikiwa mashtaka mengi ya hovyo hovyo mahakamani?

RCO-Ni maagizo kutoka juu,maana tunajaribu kutumia mbinu za kagame.

Kibatala-unadhani watanzania wanafurahia wawakilishi wao kulundikiwa kesi na kushitakiwa kila Leo?

Rco-nadhani hawapendi ila ndio hivyo tena.

Kibatala-ukiwa kwenye gari yako,oficin na nyumbani kwako ni nyimbo gani hupendelea zaidi kuisikiliza?

RCO-CCM mbele kwa mbele.

kibatala-asante sana shaidi.

Rco-you're welcome.
Hahahaha
 
Back
Top Bottom