Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,577
Nimekuwa nikiifuatilia kesi hii kwa karibu sana na jambo la kukatisha tamaa na kusikitisha ni kuwa mashahidi wa CCM wamepeleka ushahidi wa uongo mahakamni.
Hapa ni mchezo wa kumfanya Dr. Slaa awe bize muda wote na haswa wakati huu ambapo ripoti ya BOT inafanyiwa kazi.... ili kupunguza kelele za mjadala wake ,
Nafikiri kama shahidi anakiri kuwa vielelezo vimepikwa hakuna haja ya kupoteza muda wa slaa any more,
Someni hapa , source mwananchi.
Posted Date:12/4/2007
Hapa ni mchezo wa kumfanya Dr. Slaa awe bize muda wote na haswa wakati huu ambapo ripoti ya BOT inafanyiwa kazi.... ili kupunguza kelele za mjadala wake ,
Nafikiri kama shahidi anakiri kuwa vielelezo vimepikwa hakuna haja ya kupoteza muda wa slaa any more,
Someni hapa , source mwananchi.
Posted Date:12/4/2007
Shahidi akiri kuwasilisha vielelezo vya kugushi
Na Mussa Juma, Arusha
SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya kupinga matokeo ya Jimbo la Karatu, Joseph Haimu(3, amebanwa na wakili wa upande wa utetezi, Tundu Lissu na kukiri kuwa baadhi vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo vimegushiwa.
Haimu alidai, fomu za matokeo ya uchaguzi zilizowasilishwa na mahakamani hapo na upande wao, zina baadhi ya vipengele ambavyo vimefutwa.
Akihojiwa na Lissu, anayemtetea mlalamikiwa wa pili, Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Wilbroad Slaa, shahidi huyo alidai hatambui aliyegushi matokeo hayo kwani, fomu walizokuwa wanatumia kama ushahidi wao walipata kutoka kwa mawakala wa CCM.
Haimu alikiri kuwa hata fomu zilizokuwa na alama za siri katika matokeo hayo ambazo zimewasilishwa mahakamani hapo kama vielelezo baadhi vina upungufu.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya wakili Lissu na shahidi huyo:
Lissu: Je, unatambua fomu hii kama kilelelezo P 39 ambacho mlikiwakilisha mahakamani ambayo ni matokeo ya Kituo cha Ngiting na unaweza kutusomea?
Shahidi: Najua. Mgombea wa ubunge wa CCM alipata kura, 124, CHADEMA 69, NCCR 1 na CUF 0.
Lissu: Je, hii fomu ina upufungu unaouona?
Shahidi: Ndio, kwenye matokeo ya Chadema inaonekana kama namba moja imefutwa kabla ya 69.
Lissu: Kwa hiyo unaithibitishia mahakama kuwa kuna kufutwatutwa hapo?
Shahidi: Ndio, ila naomba nitoe ufafanuzi kidogo.
Jaji Robert Makaramba anayesikiliza kesi hiyo anaingilia kati na kusema: "Wewe jibu swali la wakili kama hataki maelezo".
Lissu: Mimi sitaki ufafanuzi huo nataka ujibu ndio au hapana!
Shahidi: Ndio.
Lissu: Naomba usome kielelezo P 43 cha fomu 21B matokeo ya kituo hicho yanasomekaje?
Shahidi: CCM 124, CHADEMA 109 na NCCR 1
Lissu: Je, kuna tofauti ya kura ngapi za Chadema ambazo hazipo katika kielelezo p 39?
Shahidi: Kura 40.
Lisssu: Je, ni nani aliyefuta namba moja na kuifanya sifuri kuwa sita, ni wewe au ni nani?
Shahidi: Sijui!
Pia, wakili huyo alitoa fomu nyingine mbalimbali ambazo zimewasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka ambazo matokeo yake yanatofautiana na matokeo ya Tume ya
Uchaguzi na matokeo ya kumbukumbu za Chadema.
Awali, shahidi huyo alisema fomu za matokeo ambazo wamekuwa wakizilalamikia zilikuwa hazina alama ya siri, hivyo ni rahisi kugushiwa, ingawa alidai hata hizo zenye alama ya siri pia zina upungufu.
Baada ya mahojiano hayo yaliyochukua takriban saa 4:00, Jaji Makaramba aliahirisha kesi hadi leo na shahidi huyo anatarajia kuendelea kuhojiwa na upande wa utetezi.
Katika kesi hiyo, mshtakiwa wa kwanza ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anayetetewa na Patience Mgwina na mshtakiwa wa pili ni Dk Slaa, ambaye awali hakuwepo kwenye kesi hiyo baada ya kuomba kujumuishwa.