Kesi ya Dibagula na Uchochezi wa Kidini: Je, Lissu alikuwa na lengo la kumuumiza nani?

ChamaDola

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
3,431
2,804
Kesi ya Ustadhi Hamisi Dibagula v Jamhuri ya 2001 haina tofauti na kesi inayomkabili Tundu Antipas Lissu!

Dibagula Alishtakiwa na Kuhukumiwa Miezi 18 jela kwa kutamka maneno haya:"Yesu si Mwana wa Mungu bali ni la mtu kama lingine tu"!

Mahakama ya Wilaya ya Morogora ilimkuta na hati ila Mahakama ya Rufaa ilibatilisha hukumu hio!

Je, Katika kesi ya Lissu,aliyeumizwa na yale maneno ni nani,na yuko tayari kuwa shahidi wa Jamhuri?

Hukumu ya Kesi ya Haisi Rajabu Dibagula imeambatanishwa hapa chini
 
Attachments

  • Hamisi Rajabu Dubagula Vs Republic.pdf
    546.3 KB · Views: 81
Chachu Ombara kweli kabisa,kama sijakosea ni Chipeta!
Kuna kauli nimeipenda ya Jaji Samata akimunukuu Voltaire:
"I disagree profoundly with every word that you say but I shall defend your right to say it"
Ninachojiuliza ni je,muktadha wa kosa la Lissu unasadifu mazingira ya kauli yake?
Na je nia ya kutenda ilo kosa ilikuwepo?
Na je kuna mtu aliyeclaim kuumizwa na kauli ya Lissu?
Nasubiria mtanange wa Maswali na Majibu!
 
Kuna watu hawana akili...Lisu alisema maneno hayo mbele ya umati wa waislamu Zanzibar hawakureact wewe siro uko dar unawashwa..
Ha ha ha! Nimeelewa. Yale maneno yangekuwa mabaya kihivyo, Lissu angepigwa mawe pale pale jukwaani maana wale jamaa linapokuja suala la imani hawana mzaha. In short hamna kesi hapo.
 
Chachu Ombara kweli kabisa,kama sijakosea ni Chipeta!
Kuna kauli nimeipenda ya Jaji Samata akimunukuu Voltaire:
"I disagree profoundly with every word that you say but I shall defend your right to say it"
Ninachojiuliza ni je,muktadha wa kosa la Lissu unasadifu mazingira ya kauli yake?
Na je nia ya kutenda ilo kosa ilikuwepo?
Na je kuna mtu aliyeclaim kuumizwa na kauli ya Lissu?
Nasubiria mtanange wa Maswali na Majibu!
Nakumbuka kuna moja ya post zako kama sio uzi, ulitoa tahadhari mapema jinsi Republic inavyoelekea kuangukia pua tena.
 
Namsubiri shahidi wa hii kesi.. majibu ya hapana nafikiri yatakuwa mengi.
Jamhuri haitakuwa na nia ya kuendelea na hiyo kesi hivyo itafutwa halafu Lissu atakamatwa tena hapo hapo na kupelekwa Central chini ya ulinzi mkali wa makomandoo. Kama mchezo wa kitoto vile. Nadhani kuna haja ya kuangalia hizi sheria za kuachiwa na kukamatwa hapo hapo. Huu ni utoto.
 
dudus mwendesha mashtaka wa kesi hii atakuwa na kazi ya kuthibitisha:
a)Uwepo wa NIA ovu ya Lissu?
b)Uwepo wa Aliyeumizwa na kauli hio
c)Je muktadha wa kaui ya Lissu inaendana na kosa?Je kauli wa mkutanoni ni sawa sawa kiuzito kama ikisemwa msikitini?
d)Je Jamhuri ina USHAIDI usiyo na MASHAKA juu ya Lissu KUTOA KAULI CHOCHEZI NA ILIYOUMIZA UMMA PALE MKUTANONI!
 
Nimekusoma Kiongozi. Kwa kuzingatia aina na ruling ya kesi ya Dibagula, Lissu hana kesi. Mashitaka yake ni null and void.
 
Hembu tusaidie sisi tulio huku mbali kolomije hatujui lisu alisema nini huko unguja mpaka ikawa kesi.
 
Back
Top Bottom