Kesi ya DECI imewagusa Wachache Huku Chimbuko la Wahusika Serikalini Wameachwa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya DECI imewagusa Wachache Huku Chimbuko la Wahusika Serikalini Wameachwa!!!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KING COBRA, Sep 2, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kesi ya DECI imewagusa Wachache huku Wahusika Kamili kutoka Serikalini wameachwa na Viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na Wachungaji waliohamasisha Watu kupitia TV na Radio zao wameachwa na Kwa sasa wanafanya kazi ya kunadi CCM. Wafuatao walihusika moja kwa moja lakini hadi leo wapo mitaani na wamehusika kikamilifu kuunga mkono CCM 2010: 1. Askofu Mwasota 2.Askofu Gamanywa 3.Getrude Rwakatare 4.Alphonce Temba n.k . Kesi nyingine ikifunguliwa inaweza kuwaleta wote hawa bila kujali CCM
  P.O.BOX 9937,
  DAR-ES-SALAAM.
  6 Juni, 2009
  ATTN: ASKOFU DAVID ANDULILE MWASOTA
  KATIBU MKUU (TAIFA)
  PENTECOSTAL COUNCIL OF TANZANIA (PCT)
  P.O.BOX 62535
  DAR-ES-SALAAM.

  YAH: ULEZI, USHAURI, UTETEZI NA UTANGAZAJI WA KAMPUNI YA KITAPELI DECI (T) LTD.

  Kichwa cha habari hapo juu chahusika. Mnamo tarehe 08/04/2009, kamati ndogo iliyoundwa na PCT ikiongozwa na Mwenyekiti Askofu Bartholomew Sheggah ilitoa tamko kuwa wao ndio waanzilishi, walezi na washauri wa Kampuni ya DECI na kwamba matatizo yote yakitokea kwenye kampuni hiyo yapelekwe kwao na si kwa viongozi wa DECI. Kabla ya tamko hilo, ofisi yako ilitoa matangazo mazito sana kwenye vituo mbalimbali vya redio, hususan RADIO PRAISE POWER, WAPO RADIO, RADIO MLIMANI, RADIO TIMES FM, UPENDO FM n.k. kwa kumtumia Mch. ALPHONCE TEMBA ambaye alijitambulisha kama Mwinjilisti wa Kimataifa. Kitendo cha kutumia radio za Kikristo na kuwatumia Wachungaji kupigia debe kampuni ya DECI kilifanya umati mkubwa kufurika kwenye mkutano huo na wengi wao wakawa wamepata imani kubwa na kampuni ya DECI. Viongozi wa makanisa wamehusika kwa kiasi kikubwa kupora fedha za wananchi kupitia mchezo huo kwa njia ya kuhamasisha. Kitendo cha viongozi wa dini kuacha kazi ya kiroho na kuhubiri ujasiriamali kwa njia ya upatu kimewafanya watu wengi kujiunga na mchezo huo wakiamini kwamba wataokoka na umaskini, na vijana wengi waliookoka waliacha kazi ya kuhamasisha mambo ya kiroho na kuihubiri DECI huko mikoani. Ajira za wengi zimepotea kwa kukimbilia ajira za DECI, ambazo sharti lake mojawapo lilikuwa lazima mtu awe ameokoka. Hii ni dalili mojawapo ya kutimia kwa Unabii ulionenwa na Nabii Daniel, kwamba ‘Chukizo la Uharibifu Limesimama Mahali Patakatifu’ na ni dalili tosha kwamba ‘siku za mwisho zimekaribia’, kwa sababu kitendo cha kuchanganya Neno la Mungu na Kamari ni LAANA! Uchunguzi wetu umebaini kuwa uhamasishaji wa watu makanisani ulifanyika na Wachungaji kwa kutumia Maandiko Matakatifu na wengine walifikia kuwaambia watu kuwa Rais Jakaya Kikwete angekuwa mgeni rasmi na angetoa msimamo wa serikali kuhusu hatma ya DECI, jambo ambalo lilikuwa la uongo. Pia inaeleweka kwamba, tamko la PCT lilikuwa limekuja baada ya serikali kupitia BOT kuonya wananchi kwamba DECI ni kampuni ya kitapeli. Tamko lililotolewa katika ukumbi wa PTA Saba Saba lilikuwa linalenga kupotosha wananchi na kuongoza uvunjifu wa sheria ambao kwa sasa amani ipo mbioni kutoweka kutokana na watu wengi, wakiwemo wajane, yatima na walemavu kutapeliwa na DECI. Ikumbikwe kwamba Mch. JACKSON MTARESI ni Mwanzilishi wa kanisa la JESUS CHRIST DELIVERENCE CHURCH ambalo limesajiliwa na PCT chini ya Mwenyekiti wa kipindi hicho Askofu Sylvester Gamanywa ambaye alitumia Wapo Radio kutangaza kwa nguvu zote kampuni ya DECI. Viongozi hawa wa DECI walimtumia sana Bw. Arbogast Francis Kipilimba (Meneja Uendeshaji wa shughuli za DECI na aliyeongoza wateja wa ELIMIKA), ambaye ni mzee wa kanisa linaloongozwa na Askofu Bartholomew Sheggah ambaye ndiye aliyesimama kutoa tamko la PCT. Uchunguzi wetu umebaini kuwa Mchungaji Dakta Getrude Rwakatare (Mikocheni B Assembles Of God), Askofu Mgullu Kilimba, Askofu David Mwasota, Askofu Bartholomew Sheggah, Askofu Sylvester Gamanywa n.k walikuwa ni wadau wakubwa na wengine kupitia huduma maalumu ya ELIMIKA. Taarifa zilizothibitishwa na viongozi wa DECI zinasema kwamba wateja wote wa ELIMIKA wamesha rejeshewa fedha zao wakati maelfu kwa malaki ya walalahoi bado hawajapata na hawajui hatma yao, jambo ambalo ni ubaguzi na dhambi kubwa! Tafsiri ya upatu ya kuwarejeshea fedha vigogo hawa ni kwamba, pesa hiyo imetokana na ile iliyopandwa na watu wengine, wakiwemo wajane na yatima walioshawishika na tamko la wachungaji la PTA Saba Saba. Kamati yetu imekuwa ikipata shida kubwa sana kuwatuliza wajane na yatima waliotapeliwa kutokana na baadhi ya Wachungaji na Maaskofu kurejeshewa fedha hizo kinyemela na hivyo ubaguzi wa matabaka umeonekana ukitenda kazi kwa wazi mno! Pia imebainika kuwa Alhamisi ya wiki iliyopita (May 28, 2009), Mch. Getrude Rwakatare ameonekana akiwabeza waumini waliopanda mbegu zao DECI na kutapeliwa kwa tafsiri kwamba wamepoteza fedha zao kwa ujinga wakati yeye mwenyewe alishawishi watu kupitia RADIO PRAISE POWER. Ikumbukwe kwamba, wananchi wengi waliamua kuingia kwenye upatu huo baada ya kuona watu kama Mchungaji Rwakatare, ambaye ni Mbunge (Viti Maalum CCM) na kiongozi wa dini, pamoja na viongozi wengine wa dini, wakishiriki upatu huo na hivyo kuhisi kwamba hakukuwa na mashaka yoyote. Leo anapoibuka na kusema watu waliopanda mbegu zao ni wajinga, anawahukumu kimakosa kwa sababu walifuata mahubiri yake na washirika wake, vinginevyo aseme leo kwamba hata mahubiri ya wokovu anayoyatoa kila siku na kushuhudia umati wa watu wakiokoka, watu wasiyafuate kuanzia sasa kwa maana wakiyafuata watakuwa wajinga! Aidha, kitendo cha maaskofu wote waliohusika na DECI kujificha katika kipindi hiki kigumu kwa wanachama wa DECI, pengine wakiogopa aibu ya utapeli uliofanyika na kuitupia lawama serikali, si cha busara kwa sababu wao ndio waliokuwa mstari wa mbele kuwashawishi kondoo hawa maskini kuingia kwenye kamari hii ya DECI. Hii inaonyesha pia kwamba, huenda viongozi hawa wa kiroho hawajali madhira yaliyowakumba wananchi wengi, bila kujali tofauti zao za kiimani na kiitikadi. Ipo mikakati mikubwa ya viongozi wa DECI wakishirikiana na baadhi ya Wachungaji ambao wanajaribu kushawishi watu waliotapeliwa kuilaumu serikali ili kuepuka aibu inayokuja hivi karibuni. Napenda kuweka bayana kwamba, lawama zote zinazotokana na utapeli wa DECI zielekezwe kwa washauri, walezi, waanzilishi na wapambe wa kampuni hiyo kwa sura ya tamko la PTA Saba Saba sawasawa na Andiko la kitabu cha Mithali 11: 18, 21. Mungu amekuwa akionya Kanisa lake kupitia BOT na Waziri Mkuu lakini PCT imekuwa ikikaidi na kumwinua ‘mungu’ wa DECI, jambo ambalo linamhuzunisha Mungu. Kitendo cha viongozi wa DECI kuchukua fedha kwa watu kwa kisingizio kwamba wanachangia chama ambacho hakipo wala kusajiliwa kinahatarisha imani ya Ukristo nchini na dunia nzima. Pia napenda wananchi watambue kwamba viongozi wa DECI hawakuwa wakweli tangu mwanzo, kwani walijua kabisa kwamba shughuli zao hazijasajiliwa na kwamba ni kinyume na sheria za nchi, lakini walithubutu kuidanganya PCT ambapo sasa Wakristo wengi ndio waathirika. Hii ni kwa sababu wanajamii ni wepesi sana kuamini kile kinachohubiriwa na viongozi wa kiroho kuliko hata wanasiasa. Nakushauri uitishe mkutano wa dharura wa Maaskofu na Wachungaji ili kueleza bayana hali inayokabili PCT kwa sasa kwani waathirika wanaelekeza lawama kwako na kamati yako. Tunaiomba serikali ichukue hatua haraka kuwakamata viongozi na kupelekwa mbele ya vyombo vya kisheria bila kujali itikadi za kidini ili kuepusha machafuko yanayoweza kutokea kama Kenya endapo viongozi wa DECI wataachwa wakitembelea magari ya kifahari mitaani, huku wananchi wakihaha kusaka mbegu zao!; Yapo baadhi ya mawazo yaliyotolewa hivi karibuni na Wabunge yakilenga kuishauri serikali kuacha kuishughulikia DECI kwa kuhofia uchaguzi 2010, tunasema mawazo hayo yanalenga kujinufaisha matumbo yao na sio maslahi ya Wananchi waathirika. Hatua ya viongozi wa DECI kumtuhumu Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo, kwamba anawakandamiza Wakristo si ya kweli kwa sababu DECI si chombo cha Kikristo wala Ufunuo kama wanavyodai wao, bali ni chombo cha kitapeli. Tunaamini kwamba, hata haya maandamano ambayo wadai wanataka kuyafanya inabidi yaelekezwe PCT na siyo serikalini, kwa sababu PCT ndio waliowaita mkutano na kuwahubiria kuhusu DECI, leo wanakwenda serikalini kufanya nini? Mwisho, nachukua fursa hii kuvishukuru sana vyombo vya habari, hususan magazeti ya KULIKONI, THISDAY, NIPASHE, MAJIRA, MWANANCHI, TANZANIA DAIMA, ITV, TBC1 na mengineyo kwa kufichua uozo huu wa upatu wa DECI na kubainisha kwamba kumbe ilikuwa ni kamapuni ya kitapeli ambayo ilishindwa huko Kenya na kuamua kukimbilia Tanzania. Hakika mchango wa vyombo vya habari katika suala hili ni mkubwa sana na sisi wananchi hatuna budi kuvipongeza kwa sababu vinaendelea kufichua uovu wa DECI ya Kenya ambayo ni sawa na Kaka na Dada na DECI hii ya Tanzania. Pia tunapongeza viongozi wa kidini,vyama vya siasa pamoja na wa serikali waliokemea utapeli huu na kuwaonya wananchi wasiendelee kupanda mbegu zao kwani hivi sasa kilio kingekuwa kikubwa zaidi ya hapa tulipofikia. ……………………………………………………. MAKAMU MWENYEKITI NA MSEMAJI WA KAMATI. Nakala: Ofisi ya Rais (IKULU) Spika wa Bunge Waziri Wa Fedha Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) DECI Makao Makuu Vyombo vya habari Mtandao wa Makanisa
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  WACHUNGAJI na maaskofu zaidi ya 30, wa Kanisa la Pentekoste, wametoa tamko zito na kumtaka Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuingilia kati kuinusuru Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), ili iweze kuendelea na kazi yake ya kuondoa umasikini kwa Watanzania. ​
  Maaskofu hao walitoa tamko hilo jana katika Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam, walipokuwa wakitoa msimamo wao kuhusu sakata hilo. Baadhi ya maaskofu hao ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati maalum waliyoiunda, Askofu Bartholomeu Sheggah, Katibu wa Kamati, Bernard Kung'unde na Askofu David Mwasota ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT)......ifate hapa​
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa taasisi hiyo inayoundwa na Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), walisema tasisi hiyo ilianzishwa baada ya kubaini kuwa vyombo vingi vya kuinua uchumi vilivyoanzishwa nchini vilikuwa vikijali faida kubwa kuliko kuwatetea wanyonge. Akisoma tamko la Deci kwa niaba ya wenzake, maaskofu hao, Bathromeu Sheggah, alisema inasikitisha na inakatisha tamaa kuona kwamba kwa kipindi cha miaka isiyopungua mitatu ya huduma ya taasisi hiyo, Benki Kuu (BoT) inatangaza katika vyombo vya habari kuwa taasisi yao haitambuliki. Alisema tangu waanzishe taasisi hiyo, Serikali imefanikiwa kupata zaidi ya Sh120, 674,497 milioni kama kodi ya mapato na kuwa wafanyakazi 400 wa taasisis hiyo wamekuwa wakilipiwa kodi ya mapato ‘PAYE' na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Alisema ikiwa serikali italazimisha kusitisha kwa huduma za taasisi yao, wananchi wapatao 3,500,000 toka kwa washiriki wao 700,000 wataathirika kiuchumi, kiafya, kielimu na kijamii na hatimaye kuchangia vunjivu kwa amani ya nchi.
  Habari Leo lasemaje?
  ......Wakati viongozi hao wakizungumza na wadau hao, hakuna kiongozi wa DECI aliyehudhuria mkutano huo na baadaye Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Timoth ole Loiting'ye, aliiambia HabariLeo kwa simu kuwa hana taarifa ya mkutano huo, na kwamba maaskofu hao waliuandaa mkutano kwa utashi wao. "Sisi hatujawatuma wameamua wenyewe kuzungumzia suala hili, kwa sababu wamekuwa ni wateja wetu wa muda mrefu na tumewahudumia vizuri," alisema na kuongeza kuwa DECI itatoa tamko lao.


  Tanzania Daima yasema....


  ..........HATIMAYE siri imefichuka kuwa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), inayojishughulisha na biashara ya kupanda na kuvuna pesa, ilianzishwa nchini mwaka 2007, baada ya kampuni yenye mfumo kama huo kufa huko nchini Kenya na kuwadhulumu maelfu ya wanaupatu wake waliokuwa wamejiunga nayo.
  Vyanzo mbalimbali vya kuaminika, vimelitaarifu gazeti hili kuwa, raia mwema mmoja, jina tunalo, ndiye anayedaiwa kufichua siri ya DECI, kupitia barua pepe yake aliyoiandika kwenda kwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana nchini (CMSA), akieleza kuwa kampuni hiyo inaendesha biashara haramu kwa mfumo unaoitwa piramidi au upatu.
  na huko kenya ilikuwaje?  YOOOOOTE HAYA NNA SWALI MOJA TU.  JE DECI NI WAZO LA NANI HASA?

  JE NI LA MAASKOFU AU KINA Mtaresi na Timoth Ole Loutingaye??


  Baba Askofu Shegah na Mwasota je ni wazo lenu hili?
  You might also like:
   
 3. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=1]Bernard Madoff gets maximum 150 years in prison[/h]

  [​IMG]


  NEW YORK – Convicted swindler Bernard Madoff was sentenced to 150 years in prison Monday for fraud so extensive that the judge said he needed to send a symbolic message to those who might imitate his fraud and to victims who need relief.
  Applause broke out in the crowded Manhattan courtroom after U.S. District Judge Denny Chin issued the maximum sentence to the 71-year-old defendant, who said he sought no forgiveness and knew he must live "with this pain, this torment, for the rest of my life."
  Chin rejected a request by Madoff's lawyer for leniency and said he disagreed that victims of the fraud were seeking mob vengeance.
  "Here the message must be sent that Mr. Madoff's crimes were extraordinarily evil and that this kind of manipulation of the system is not just a bloodless crime that takes place on paper, but one instead that takes a staggering toll," Chin said.
  The judge said the estimate that Madoff has cost his victims more than $13 billion was conservative because it did not include money from feeder funds.
  "Objectively speaking, the fraud here was staggering," he said.GET MORE
   
 4. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=3]Mamia walizwa na DECI kwa Mzee Madiba[/h]

  • At least 200 investors involved
  • Purchase orders for AIDS drugs allegedly faked
  • *Could be S.Africa's biggest corporate fraud
  • Investors from U.S., Australia, Germany, S.Africa


  JOHANNESBURG, June 11, Hundreds of investors have lost money in what could be South Africa's biggest corporate fraud, worth up to 10 billion rand ($1.24 billion), a private investigator and lawyer said on Thursday.  The fraud was spearheaded by Barry Tannenbaum, the South African son of one of the founders of pharmaceuticals firm Adcock Ingram, and is still unravelling, they said.
  Investigator Specialised Services Group (SSG), hired by investors to look into Tannenbaum, said he persuaded investors to plough money into a pharmaceutical ingredient import business and faked purchase orders from firms including Africa's biggest generic drug maker, Aspen.
  Products included ingredients for life-prolonging anti-retroviral AIDS drugs, and Tannenbaum offered annual returns of up to 200 percent, said SSG, which published documents and emails related to the scheme on its website.
   
 5. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Labels: BONDENI, DECI

  [h=3]Viongozi DECI waburuzwa mahakamani.[/h]
  [​IMG]
  Viongozi wa DECI Arbogast Kipilimba, Jackson Mtares, Samwel Mtares,Dominick Kigedi na Timotheo Saiguran ole Loiting'ye, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka mawili ya uendeshaji wa mradi wa upatu.  You might also like:
   
 6. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=3]DECI (Desimali?) KENYA, KONDOO WALIINGIZWA MKENGE??[/h]
  Clergy admits to misleading flock over schemes. [​IMG]Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Pentecoste, Askofu David Mwasota kulia, Katibu wa Kamati ya maandalizi (DECI), Mchungaji Bernard Kun'gunde (kati) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati, Askofu Batholomew Sheggah wakisaini baadhi ya taarifa walizozitoa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Maonyesho vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo hii.

  Some religious leaders have admitted misleading their flock into joining pyramid schemes.​

  Members of the clergy yesterday told a taskforce into the operation of pyramid schemes that con artists, masquerading as religious organisations, took advantage of the Church's influence.
  SOMA MWENYEWE HAPA
  JE WATUMISHI HAWA AU WACHUNGA KONDOO WETU WAYAJUA YA LIYOIPATA DECI HUKO KENYA?
   
 7. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145


  Labels: DECI


  [h=3]DENSI LA DECI MAELEZO[/h]
  [​IMG] [​IMG] ilibidi mkutano ufanyike nje. [​IMG]" Sasa nitafikishia wapi ujumbe wangu?" [​IMG] "kweli bora tutoke" [​IMG] "Hatunyamazi bora tutoke" [​IMG] Afisa mwingine aingilia kati kumtuliza mmoja wa washiriki Mch Temba. [​IMG] Mabishano kidogo, [​IMG] Afisa Habari akimtaka kufuta kauli na kufuata press release yake.
  a
  [​IMG]Alianza vyema akiwa na mwenyekiti wa wastaafu wa EAC  Leo ilikuwa ni patashika pale MAELEZO baada ya anayejiita mwenyekiti wa kamati ya dharura ya washiriki DECI Isaac Kalenge kusema kuwa Pinda karopoka, alitakiwa na uongozi TIS kufuta kauli yake lakini hakuwa tayari ilibidi mkutano uishie hapo na kuamia nje ya ofisi za idarahiyo. ​  You might also like:

  Mshidi wa fyatua choo huyu hapa


  Da famous BONGA BAR.


  Mgao wa Umeme kuwa historia????   
 8. j

  jjj2be Member

  #8
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 5, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kesi hii bado inaendelea .... Au imetiwa kapuni ....
   
Loading...