Kesi ya akina Mbowe ina manufaa gani kwetu CCM, mbona haitupi any political mileage?

mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
20,367
2,000
kaka, hii kesi ina manufaa kwa CCM mwendazake - tatizo maza anataka kurithi kila kitu hadi matatizo binafsi ya marehemu kitu ambacho ni kosa kubwa kibinadamu hata katika ulimwengu wa kiroho.

Maza apewa ushauri huu muhimu, kama marehemu alikuwa hampendi A, B, C D basi ni yeye na wala asitake sisi wana CCM wote tuendelee kuyaachukia ambayo yeye aliyona hayamfani wakati yeye hayupo duniani na hawezi kurudi tena.

Hata kama marehemu aliapa kutotoa katiba mpya basi ni yeye, sasa kwani sisi tulibaki hapa duniani tukisema katiba mpya ni ajenda yetu leo ni kosa ? arudi basi kama ana uwezo huo.

Narudia tena, maza ashauriwe - adui wa mtangulizi wako si wa kwako, principal ya maisha ni kwamba tengeneza marafikio wengi kuliko maadui.

Nitamweshimu wana CCM YEYOTE atayetamka kwamba katiba mpya ni ajenda yetu ya leo, regardless !!
Mkuu Hatutaki Katiba Mpya!; Tunataka Mkutano wa Katiba!
Ukisema Katiba mpya bunge hili linaweza likakaa hata leo Wakafanya ya kufanya kisha wakasema Katiba mpya mlio itaka hiyo hapo!
 

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
993
1,000
Wana CCM mliopo mtandaoni.

Ni kweli wapinzani hawana ajenda na bawajawahi kuwa nayo zaidi ya blah blah tu.

Lakini, nasema lakini sisi wana CCM kupitia CCM Maslahi ndio tunawapa hawa wapinzani cha kutusumbua nacho.

Mfano: Hii kesi ya kijinga ya Mbowe ina manufaa gani sasa ki siasa kwetu CCM?

Sawa, ni kweli Mbowe ni tishio kwetu lakini sisi ni wakubwa zaidi ya Mbowe tungeweza kum contain kisayansi tu. Ona sasa badala ya sisi kupata political mileage kwa kumtia gerezani yeye ndo anapata political mileage nyingi mno!

CCM Maslahi wataizika hiki chama muda si mrefu then wanahamia kwingine. Time will tell!
Bora umeona. Inasababisha hata mimi ninaichukia mno CCM kwa sasa! Basi tu huwa sio muumini wa kuhama hama!
 

eliasmisinzo

JF-Expert Member
Aug 13, 2021
301
500
CCM inahusika vipi na hii kesi ya Mbowe?
CCM inahusiana na Mbowe kwenye Ubunge- walimtoa akiwepo jimboni hai
CCM inahusiana na Mbowe kwenye Urais- walimshinda akiwa hayuko jela
CCM haihitaji Mbowe afungwe ndiyo ipate inachokitaka kwa sababu imekuwa ikipata akiwepo
CCM inapata unachotaka kupitia TISS na Polisi, Hilo ndo sanduku lao la kura. Sanduku la kura halisi, CCM wanaliogopa Kama ukoma.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
15,965
2,000
Mbowe anastahili umaarufu alio nao, anaijua siasa vizuri sana na ni muumini halisi wa katiba na utawala wa sheria.
Umeona sasa huyu ameandika jambo la maana hapa

Jana kuna mtu nimemwambia mimi ni CCM akaanza kushangaa kisa ameona nikipinga baadhi ya mambo ya kijinga serikali inafanya ikiwemo hii kesi ya Mbowe

Wanampa Mbowe umaarufu ambao hata hakustahili sababu ya upumbavu wao
 

maruudaniel

JF-Expert Member
Dec 19, 2020
404
500
Umeona sasa huyu ameandika jambo la maana hapa

Jana kuna mtu nimemwambia mimi ni CCM akaanza kushangaa kisa ameona nikipinga baadhi ya mambo ya kijinga serikali inafanya ikiwemo hii kesi ya Mbowe

Wanampa Mbowe umaarufu ambao hata hakustahili sababu ya upumbavu wao
Hii kesi imenifanya kutowaelewa viongozi wangu. Kwani wamemwongezea Mbowe umarufu zaidi na sasa mbowe kufungwa au kutofungwa limeshakuwa ni ushindi kwa Mbowe
 

Biggs

JF-Expert Member
May 3, 2014
1,073
2,000
🤔🤔🤔🤔🤔 So you're trying to tell us that it has no merit at all (meaning ni ya KUBUMBA) and that's why it's backfiring as there're things that shouldn't have been exposed to the public. Or I'm missing a point from you !!!
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,417
2,000
Yaani hadi unaona aibu kujiona mCCM
Ukitaka kujua CCM haina imepoteza ushawishi, nenda huko ngorongoro kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo kampeni zilivyododa. Baada ya wapinzani kususia hasa cdm, CCM imebaki na vyama vyake vya mfukoni wakifanya kampeni choka mbaya. Sasa kama mpaka Wamasai wameshtuka nani kabaki?
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,417
2,000
Wewe ndio wale tunawaita CCM limbukeni

Sasa nitoke niende wapi? Huko kwenu nako hamueleweki njaa inawasumbua sana

Kimsingi hakuna anayekutaka huku upinzani maana utaleta mawazo ya kizee yaliyofeli huko ccm. Ww baki huko huko ili usaidie kuwaambia wenzako kuwa CCM sio chama cha kizazi hiki, hivyo kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti ni kukaribisha machafuko. Sasa hivi mmeachiwa mshiriki peke yenu chaguzi na vile vyama vyenu pandikizi lakini hamna ushawishi tena, na idadi yenu halisi ya wapiga kura inajionyesha.
 

CCM Music

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
1,035
2,000
Kimsingi hakuna anayekutaka huku upinzani maana utaleta mawazo ya kizee yaliyofeli huko ccm. Ww baki huko huko ili usaidie kuwaambia wenzako kuwa CCM sio chama cha kizazi hiki, hivyo kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti ni kukaribisha machafuko. Sasa hivi mmeachiwa mshiriki peke yenu chaguzi na vile vyama vyenu pandikizi lakini hamna ushawishi tena, na idadi yenu halisi ya wapiga kura inajionyesha.
Sawa
 

Pinetech Way

Member
Feb 19, 2021
27
45
Jitafakalini wanaccm hapo mlipofika pamewatosha tulishawaambia kuwa Mbowe sio gaidi nanyi mmekazana kuleta ushahidi,hii kesi itawaumbua huko mwisho wa safari I furahieni kwakuwa jaji anapokea maelekezo na mungu huwa hawaachi watesi wanaodhurumiwa haki zao,Kama kiss Ni siasa muingie uwanja wa fisi kutokana kihoja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom