Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Nimeanza kuingiwa na wasiwasi, kutokana na sakata hili la akina Halima Mdee, kwa Kesi yao waliopeleka mahakamani na kinachoendelea, Mahakama inaweza kufanya "delaying tactics" Hadi shauri hilo lije kupata hukumu, itakuwa mwaka 2025, wakati wa uchaguzi mkuu mwingine unaokuja!
Kwa hiyo ninachokiona Mimi hivi sasa, Hawa akina Halima Mdee, wanachofanya kwa kushirikiana na Spika wa Bunge, Tulia Ackson, pamoja na mhimili wa Mahakama, ni kufanya "delaying tactics" Ili Kesi hiyo waicheleweshe Hadi ifike mwaka 2025, tutakapofanya uchaguzi mkuu.
Nayasema hayo nikiwa na ushahidi wa mazingira, kwa yanayotokea hivi sasa, nikifanya utabiri wangu huo.
Inajulikana wazi, hata na Jaji anayesikiliza Kesi hiyo, kuwa hao akina Halima Mdee, wameshapoteza sifa za kuendelea na ubunge wao, kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(e) ambayo inasema hivi nanukuu "Mbunge atakoma kuwa Mbunge litokeapo moja ya mambo yafuatayo, ikiwa Mbunge huyo ataacha kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa" mwisho wa kunukuu.
Sasa nimuulize Spika Tulia Ackson, anaposema kuwa akina Halima Mdee, bado wataendelea kuwa wabunge, Hadi pale mchakato wa mhimili wa Mahakama utakapoamua shauri lao.
Hivi Katika kipindi hicho tunaposubiri uamuzi wa Mahakama, yeye Spika Tulia Ackson, atakuwa anawatambua wabunge hao kuwa wanatoka chama gani?
Kwa kuwa vikao vyote viwili vikubwa vya chama cha Chadema, kile cha Kamati Kuu, kilichokaa mwaka 2020 na hiki cha majuzi cha Baraza Kuu, vimethibitisha kuwa vimewavua uanachama wao hao wabunge 19 wa viti maalum kwa kosa la kukisaliti chama hicho.
Je wabunge hao wataendelea kukumbatiwa na Spika Tulia Ackson, wakiwa wabunge wa mhimili wa Mahakama??
Kwa kuwa hii siyo mara ya kwanza matukio ya kuvukiwa uanachama, yamewahi kutokea, huko siku za nyuma na Bunge hilo hilo limekuwa likitekeleza kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, ambapo mara tu wanapopata taarifa ya kuvukiwa uanachama wao "automatically" pia Bunge linawaua ubunge wao.
Nitoe mifano michache, mwaka 2017, wabunge wa viti maalum wa CUF, chini ya Profesa Lipumba, alimpa taarifa Spika wa wakati huo Job Ndugai, kuwa weshafukuzwa na chama chao cha CUF, Spika Ndugai aliwafukuza ubunge wao papo kwa papo.
Licha ya wabunge hao kukimbilia mahakamani na Mahakama hiyo kutoa "court injunction" ya suala hilo, Hadi pale Mahakama hiyo itakapotoa uamuzi kwa Kesi hiyo ya msingi.
Wengi mnakumbuka kwa yaliyotokea wakati huo, ni kwa Spika Ndugai kuugomea mhimili wa Mahakama, akidai kuwa yeye Spika Ndugai, ndiye atakayeonekana kuwa anavunja Katiba ya nchi, kwa kuwa Katiba hiyo inatamka wazi kuwa kuwa Mbunge yeyote ni LAZIMA atokane na chama cha siasa!
Tukio la pili ni kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa kinamama wa CCM, Sofia Simba, ambaye naye alivuliwa uanachama wake na chama hicho cha CCM, Spika pia hakusita kumvua ubunge wake mara moja!
Swali ninalouliza, hivi kuna "double standards" Katika kutekeleza sheria hizi?
Iweje hivi sasa kwa hili suala la akina Halima Mdee, sheria zitafsiriwe tofauti??
Hivi ni nani yuko sahihi, je ni mwanasiasa mkongwe na Spika mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, aliyetamka wazi kuwa Mbunge yeyote ambaye chama chake, kikimfukuza uanachama wake "automatically" anakuwa hana sifa za kuendelea kuwa Mbunge au ni huyu Spika Tulia Ackson, ambaye anadai kuwa ataheshimu uamuzi wa Mahakama?