Kesi wizi wa mtandao ‘yaiva’

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
Monday, 08 November 2010 21:16

Tausi Ally
UPELELEZI wa kesi mbili za kula njama, kuiba na kutakatisha fedha haramu ikiwemo yenye thamani ya Sh3.8 bilioni, inayomkabili Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Justice Katiti na wenzake watatu umekamilika.

Hayo yameelezwa jana na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Fredrick Manyanda, akishirikiana na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincoln, mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Ilvin Mgeta, wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, hakimu Ilvin Mgeta, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 22, mwaka huu, kwa upande wa mashtaka kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao. Kesi hiyo inasikilizwa na hakimu, Ritha Tarimo.

Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo yenye mashtaka zaidi ya 11 yakiwamo ya kula njama, kuiba na kutakatisha fedha haramu zenye thamani ya zaidi ya Sh3.8 bilioni ni Samwel Renju, Haggay Mwatonoka na Hope Lulandala.
Kwa pamoja washtakiwa hao, wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mei na Novemba mwaka 2008 jijini Dar es Salaam.
Wanadaiwa kula njama na kuiba fedha za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuzihamishia kwenye akaunti za kampuni mbalimbali za watu binafsi huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Pia, wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa katika ofisi za umma Juni 6, mwaka 2008, waliiba Sh960,148,290.15, Septemba 18, 2008 waliiba fedha nyingine Sh1,426,450,684.05 na Novemba 20, mwaka huo huo waliiba tena Sh1,415,418,801.37 mali ya TRA.
Wanadaiwa kuwa kati ya Mei na Novemba, 2008 walikula njama kwa kushirikiana na watu wengine wasiojulikana kutakatisha fedha haramu kinyume cha sheria.

Wanaendelea kudaiwa kuwa kati ya Mei na Juni, 2008 walihamisha Sh960,148,290.15 kutoka akaunti namba 07410300033 ya Benki ya NBC kwenda akaunti namba 074103000112 ya NBC ya Kampuni ya Express Booking Enterprises na akaunti namba 074103000276 ya NBC ya Kampuni ya TAC Traders Limited na akaunti namba 074103000100 ya NBC ya Daima Pharmaceuticals na watu wengine.

Kati ya Septemba na Oktoba, washtakiwa hao walihamisha kutoka akaunti namba 07410300033 ya NBC Sh 1,426,450,684.05 kwenda akaunti 074103000112 ya NBC ya Kampuni ya Express Booking Enterprises na akaunti namba 074103000276 ya NBC ya Kampuni ya TAC Traders Limited na akaunti namba 074103000100 ya NBC ya Daima Pharmaceuticals na watu wengine.

Katika shtaka lingine washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Oktoba na Novemba, walihamisha fedha kutoka kwenye akaunti namba 07410300033 ya NBC Sh 1,415,418,801.37 kwenda akaunti 07410300033 ya NBC ya Kampuni ya Express Booking Enterprises, kwenye akaunti namba 074103000276 ya NBC ya TAC Traders Limited na akaunti namba 07410300033 ya NBC ya Kampuni ya Daima Pharmaceutical na watu wengine.
Katika kesi nyingine, upelelezi wa kesi ya wizi wa zaidi ya Sh3.3 bilioni kwa njia ya mtandao inayowakabili watu saba wakiwemo wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TCCL) na Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) umekamilika.

Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya, jana alidai mbele ya Hakimu Mgeta kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba kupangiwa tarehe ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali. Hakimu Mgeta alipanga Novemba 22, mwaka huu.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Marcus Masila ambaye alikuwa mhasibu wa TCCL, Dickson Maila na Robert Mbekwa.

Wengine ni Joyce Mwamagema aliyekuwa karani wa Tucta, Fortunatus Muganzi, Mariam Hostine na Gideon Uthuro kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 45 ya kughushi hundi na kuiba fedha za Tucta kwa nyakati tofauti mwaka 2008.
Kwa pamoja wanadaiwa kuiba Sh671,212,379.92 na Sh3,392,812,190 kwa kutumia njia ya mtandao wa kompyuta.

Chanzo. Gazeti la Mwananchi
 
Tatizo electronic evidence tanzania bado inasumbua sana, usishangae hao jamaa wakachomoka
 
Kuna wataalam upande wa upelelezi-polisi ambao anapata mafunzo maalum ku-deal na fraud za mitandao. Askari hao watakuwa na kikosi chao maalum ambacho makao makuu yao yatakuwa wizara ya fedha, na tayari mkuu wa kikosi/kitengo hicho amechaguliwa,toka CID kwa afande Manumbu.
Kwa hiyo in future wezi wa mtandao kama walio katika habari hii watapata shida sana
 
Mwenye update ya hukumu ya katiti ambayo ilikuwa itolewe leo please atuwekee hapa!
 
Nilishaisahau hii...ila hii miaka miwili kama unaiendesha kesi jua lazima ufilisike.
 
Back
Top Bottom