Kesi namba 458 kutotumia kikoa cha .TZ(Jamhuri vs JamiiForums) yasikilizwa na kuahirishwa hadi Novemba 20, 2017

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Wakuu, katika kesi hii ya JamiiForums kutotumia kikoa cha .TZ tunaendelea na shahidi tuliyeanza naye ambaye ni Mtendaji mkuu wa Rajisi ya kikoa cha .TZ (TZnic).

Upande wa Jamhuri unamhoji kwa mara ya mwisho shahidi (re-examination) na upande wa utetezi hautapewa nafasi ya kuhoji tena.

Tulikoishia: Kesi namba 458 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums imeendelea

Leo ni re-examination

Wakili wa Jamhuri (Kishenyi) anauliza: Shahidi uliuzwa maswali mengi mara ya mwisho ulivyokuja. Sasa ni wapi kunaonyesha matumizi ya kikoa cha dot TZ?

Shahidi: Kwenye kielelezo hicho matumizi ya kikoa hayaonekani kinaonyesha usajili tu ila sio matumizi

Kishenyi: Mpaka unakuja kutoa ushahidi ni kikoa kipi kilikuwa kinatumika?

Shahidi: Kwanza nilijiridhisha kama kuna kikoa chochote juu ya jamiiforums ambacho kimesajiliwa kwa dot tz. Nilikuta majina mawili ambayo ni jamiiforums.co.tz na jf.co.tz lakini kuhusu matumizi ‘by then’ hayo majina yalikuwa hayatumiki.

Wakili wa Jamhuri (Kishenyi): Unasemaje na unaweza kusema kama hayatumiki by then?

Shahidi: Nilienda kwenye tovuti nikaandika www.jf.co.tz sikupata kitu pia www.jamiiforums.co.tz pia sikupata kitu. Nikaridhia kuwa hayatumiki. Mbali na hivyo matumizi mengine ya tovuti unaweza kutumia kwa barua pepe niliangalia kwenye data base MX Record kwa ajili ya barua pepe, lakini ‘by then’ nayo yalikuwa hayatumiki

Wakili wa Jamhuri (Kishenyi): Mara ya mwisho uliulizwa iwapo polisi wamewahi kuwasiliana na wewe kuhusu Maxence kwenye compliance ya kesi?

Shahidi: Polisi hawajawahi kuwasiliana nami isipokuwa tu kuitwa kutoa ushahidi.

Wakili Kishenyi Wigo wa kazi yako au kazi yenu ninyi kama TZnic ?

Wakili wa utetezi, Mtobesya: (Anaingilia swali la wakili Kishenyi) Mheshimiwa Hakimu, wakili anarudia maswali ya kipindi cha nyuma

Wakili Kishenyi anaachana na swali lake na kwenda kwenye swali lingine.

Wakili wa serikali (Kishenyi): Kwenye Role ya TZnic, maswala ya usajili yanaishia wapi?

Wakili Mtobesya: Mhe. Hakimu, napinga swali. Role inaenda mbali sana, maana ya neno Role ni pana.

Hakimu Nongwa: Hapana, acha aulize. Jibu swali shahidi

Shahidi: Sisi tuna manage registry (rajisi), halafu tuna mawakala wao ndio wanatoa huduma za usajili.

Wakili Kishenyi: Mahakamani mara ya mwisho kuja hapa, uliulizwa sana maswali kuhusu jamiiforums.co.tz na jf.co.tz. Mashtaka yaliyoletwa hapa yanahusiana na nini?

Hakimu Nongwa: Unamuuliza tena shahidi mashtaka yanahusiana na nini? Nyie si ndio mmeleta mashtaka yeye atajuaje? Haya, shahidi jibu swali kama unajua.

Shahidi: Siwezi kuyakumbuka in details. Ila ni kuhusu kwamba jamiiforums inasemekana wanatumia .com badala ya .TZ

Wakili mwingine wa Jamhuri, Batilda: Mashtaka ni kutokutumia kikoa cha dot tz. Mara ya mwisho kuwa hapa; Kwa kipindi hicho wewe kama TZnic uli-verify nini?

Shahidi: Waliniuliza kuhusu usajili wa .TZ nikasema yamesajiliwa, ila mwishoni nikasema yalikuwa hayatumiki.

Mawakili wa Jamhuri wanasema hawana maswali mengine.

Hakimu Nongwa: Shahidi naomba ufafanunuzi, ulisema kwamba ulitumia MX record ili kujua kama zinatumika kwenye barua pepe?

Shahidi: Nilisema matumizi yapo ya aina mbili, kutumika kama website au kutumika kwenye barua pepe. Kwa ajili ya barua pepe niliangalia kwenye data base MX Record nikaona ilikuwa haitumiki. MX Record inasaidia kuonyesha kama tovuti hiyo ilikuwa inatumiaka kwenye barua pepe.

Wakili wa Jamhuri (Kishenyi): Mheshimiwa tunaomba tupate siku nyingine ya kusikilizwa kwa kesi hii na hati za kuita mashahidi wengine.

Hakimu Nongwa: Tarehe nyingine ya kusikilizwa ni tarehe 20 Novemba 2017. Dhamana inaendelea...
 
Duh! Kwenye kesi hii jamuhuri itapigwa dana dana mpaka basi... Ni bora tu wangeifuta kwa kuwa hii kesi jamuhuri haina uwezo wa kushida.
Sheria inataka mtu asajiliwe kwa .tz lakini sheria hailazimishi kutumia .tz peke yake. Unaweza ukasajili .tz lakini pia ukawa na .com kwa wateja wako wa nje.
Sheria hii ni sawa na ndoa ya Kiisalm. Ukiwa na mke mmoja (.tz) haukatazwi kuongeza mke wa pili (.com) nakadhalika...
 
Hivi kuwa shahidi unapewa posho?
Ni kazi kubwa jomoni...
Ndiyo... Sisi tushawahi kuishi kwa pesa za ushaidi. Kuna kipindi wazazi wangu hawakuwa na kazi na nyumbani hatukuwa na pesa za kula, ila siku hiyo mama aliitwa atoe ushahidi kwenye kesi fulani na baada ya hapo alilipwa kama sh mia saba hivi kwa hiyo siku hiyo tukala wali nyama wakati nyumbani hakukuwa na kitu chochote cha kula. Mungu ni mwema kwa kweli, alitulisha kwa pesa za ushahidi mahakamani!
 
Jamhuri,bila mkono wa Serikali,haijawahi shinda kesi yoyote ya maana.

Na hata hii watagaragazwa,DPP asipojitoa kuendelea na kesi!
 
Kwa sarakasi za Takukuru tunazozishuhudia tuzidishe maombi pia.

Jf imesajiliwa kwa kikoa cha tz.
mahakama imeshaambiwa na mashahidi wa upande wa mashtaka.
 
And unless and until we remove this dictatorial regime in power, we won't be safe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuna watu humu wanatumia majina bandia kama vile "kibatari" na Maxence Melo na Jamiiforums kwa ujumla wamekula kiapo cha kuwalinda. Lakini hii kesi ni kama vile hawaijui wakati inatuhusu sisi sote.

Kama tunataka Jamiiforums iendelee kuwa hivi ilivyo tuifuatilie hii kesi na kuwasaidia kina Maxence melo kwa kila hali. Ushindi wao ndiyo ushindi wetu lakini ni salama yetu sisi kuliko wao!
 
Na jinsi jamaa Alivyo na hasira na social media, sidhani anaweza akaacha JF iende hivihivi, labda kama wanamakubaliano na mmiliki wa JF.
Nina wasiwasi sana kuna makubaliano kama wali weza mnyang'anya Manji mashamba yake, washindwe kupata wanachokitaka kwa Memo.
Ni lazima wanamakubaliano, na hii kesi itakuja kufutwa nayo
 
Back
Top Bottom