Kesi namba 458 (Jamhuri v JamiiForums): Shahidi kutoka CRDB akosekana, kesi kuendelea Oktoba Mosi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Kesi ya Jinai namba 458 ya mwaka 2016 ya Jamhuri dhidi ya Maxence Melo na mwenzake Micke William kuhusu kuendesha mtandao nchini bila kutumia Kikoa cha do.TZ na Kuzuia Upelelezi wa Polisi imeshindwa kuendelea na ushahidi leo Agosti 26, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu baada ya shahidi wa upande wa Jamhuri kutofika Mahakamani kwa mara ya 3 sasa

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Daisy Makakala akiambatana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Saimon huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala mbele ya Hakimu Huruma Shahidi

Wakili wa Jamhuri ameiambia Mahakama kuwa shauri hilo lilikuwa mbele ya Mahakama kwa ajili ya kusikilizwa lakini kutokana na kukosekana kwa shahidi ambaye ni Tully Esther Mwambapa kutoka CRDB aliomba tarehe nyingine ambapo ameihakikishia Mahakama watakuja na jibu kuhusu shahidi huyo na mwendelezo kuhusu shauri

Hakimu Huruma Shahidi ameutaka upande wa mashtaka kuleta mashahidi Mahakamani hapo ili kesi hiyo iweze kumalizika kwa kuwa imeshachukua muda mrefu sana na ameahirishwa tena kesi hiyo hadi Oktoba 01, 2019 itakapoendelea na ushahidi.

Katika shauri hilo lililofunguliwa Desemba 2016 na kuanza kusikilizwa Februari 2017, tayari mashahidi zaidi ya Watatu kutoka upande wa Jamhuri wameshasikilizwa na shahidi wa mwisho kusikilizwa ilikuwa mnamo Novemba 07, 2018. Baada ya hapo shauri limekuwa likiahirishwa huku sababu kadhaa zikitolewa na kubwa ikiwa ni kukosekana kwa shahidi.
 
Back
Top Bottom