Kesi namba 458(Jamhuri v JamiiForums): Hakimu afiwa, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao ashindwa kutoa ushahidi

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
590
1,000
Kesi namba 458 ya Jamhuri vs Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na mwanahisa wa kampuni hiyo inayohusu kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kutumia Kikoa cha do.TZ na Kuzuia Upelelezi wa Polisi imeendelea leo Februari 20, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Shauri hili linalosikilizwa mbele ya Hakimu Huruma Shaidi, leo limeletwa mbele ya Hakimu Augustine Rwizile baada ya Hakimu Shaidi kupata matatizo ya msiba(Amefiwa).

Upande wa Utetezi leo umewakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Faraji Nguka.

Wakili Nguka ameieleza Mahakama kuwa shauri hilo lililetwa mbele ya Mahakama leo kwa ajili ya kusikilizwa na walikuwa na Shahidi ambaye ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka Kitengo cha Uhalifu wa Mtandao, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Joshua Mwangasa.

Hata hivyo, shauri hilo limeshindikana kuendelea kusikilizwa leo kwa kuwa Hakimu muhusika hakuwepo na hivyo Hakimu aliyekuwa akisikiliza kwa niaba yake, Hakimu Rwizile alisema anaaihirisha shauri hilo hadi Machi 19, 2019 ambapo litasikilizwa tena.

Kujua kilichotokea mara ya mwisho shauri hili liliposomwa, fuatilia hapa Naibu Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao kutoa ushahidi katika Kesi namba 458 dhidi ya JamiiForums - JamiiForums

Kujua zaidi kuhusu kesi zote zinazomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na mwanahisa mwenzake, fuatilia hapa Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom