Kesi namba 458 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums imeendelea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Habari Wakuu,

Leo katika Mahakama ya Kisutu, inaendelea kesi ya Jamhuri dhidi ya Wakurugenzi wa Jamii Media, ambayo ni kesi namba 458 ya Mwaka 2016.

Katika kesi hii, Maxence Melo na Micke William Wanashtakiwa kwa makosa mawili:

1) Kuendesha mtandao ambayo haujasajiliwa nchini do-tz, yaani .tz (Tanzania domain).

2) Kushindwa 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wake.

SHAHIDI alishaanza kusikilizwa mwezi Mei, unaweza kujikumbusha ilivyokuwa: Kesi namba 458 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums yaanza kuunguruma Kisutu

UPDATE:

IMG_3894.JPG


Leo Shahidi anaendelea kutoa Ushahidi. Mawakili wa Jamii Media ni Mtobesya, Kibatala, Kiangio na Kambole. Jamhuri imewakilishwa na Kishenyi.

Hakimu aanasema kwamba Shahidi anaendelea na Ushahidi wake.

"Shahidi bado upo katika kiapo na Ushahidi Unaendelea"

Tulipoishia: Shahidi Maswali uliokuwa ukiulizwa na Kibatala

Ulisema wewe ni Manager wa Network Information Centre na ukasema hukuwa na kitambulisho na ukasema uwaulize TCRA. Ulisema unashughulika na Domain kama wakala na ukasema mnayo data base.

Ulisema wanaoshitakiwa tayari walikuwa wamejisajili kwa domain mbili.

Ulisema JamiiForums ilisajiliwa na 20 June 2017 ndo usajili ulikuwa una-expire.

Kibatala anaendelea kumuuliza Maswali Shahidi.

Kibatala anampa kielelezo Shahidi na kusema akamwambia amwambie hakimu anaona nini

Shahidi: JamiiForums. Co. Tz

Kibatala: Hapo kuna sehemu imeandikwa Holders, mwambie mheshimiwa hakimu kuna jina mohamed Saleh manaake nini?

Shahidi: Holders inaonesha mwenye domain. Hapa inaonesha mwenye domaini ni Mohamed Saleh.

Kibatala: Huyo holders ndie aliyesajili JamiiForums,

SHAHIDI: Hiyo Domain ni JamioForums. Co. Tz ambaye holder ni Mohamed Saleh.

Kibatala: Mwambie hakimu kama unaona jina Maxence Melo Mubyazi au Mike

Shahidi: Silioni.

Kibatala: Wakati nakuuliza kwenye hiyo holders msajili unayemfahamu ni wa nchi gani

Shahidi: Ni kampuni iliyopo Tanzani anafanya kazi kwa niaba yetu.

Kibatala: Hapa contact Person ni nani?

Shahidi: Mohamed Saleh

Kibatala: Nyie kama watu mnaohusika na kusajili, mliwahi kupata mawasiliano kutoka jeshi la Polisi ili Maxence accomply?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kuna kitu kinaitwa do-tz ni nini?

Shahidi: Hiki sikielewi. Kitu kama hicho hakipo labda ni typing error.

Kibatala anakaa pembeni na kumuachia Wakili Mtobesya aendelee kuuliza Maswali

Mtobesya: Name servers ni nini?

Shahidi : Ni computer ambazo zinahifadhi lile jina lililosajiliwa.

Domaini ni Jf. Co. Tz kwenye kesi hii, zimesajiliwa domain mbili

Ns1. Jamiiforums. Com

Ns2. Jamiiforums. Com

Mtobesya. Unafahamu Maxence Melo alikamatwa tarehe ngapi?

SHAHIDI: Sina kumbukukumbu

Mtobesya. Unafahamu Mike aliongezwa kwenye hii kesi tarehe ngapi?

SHAHIDI: Sina kumbukumbu

Mtobesya. Unaweza kusema kwa uhakika kwamba ni lini JamiiForums. Co. Tz ni lini ziliwahi kutumika?

SHAHIDI: Hizi domaini hazijawahi kutumika ila zimesajiliwa.

Mtobesya: Ukisema zimesajiliwa unaaana gani?

SHAHIDI: Hapa zimesajiliwa ila hazitumiki.

Mtobesya. Ukitembelea JF. Co. Tz, je umewahi kuifungua?

SHAHIDI: Hili ni jina la kikoa, domain huwezi kuitembelea

Mtobesya: Mbali na kuiona hapa, ulishaiona sehemu nyingine?

SHAHIDI: Nlishaiona kwenye data base

Mtobesya. Isaidie mahakama, kuna tofauti gani kati ya kusajili na kutumia.

SHAHIDI: Kusajili ni kuregister na kutumia ni aidha utumie barua pepe au tovuti. Mimi sijapata kuzitembelea

Mtobesya: Mara ya kwanza ulikataa kuzitembea sasa hivi umesema ulitembea. Ulijuaje kama hazitumiki

SHAHIDI: Nlipoitwa kutoa ushahidi ilibidi nitembelee data base nikakuta haya majina. Nikagundua haya mawili yamesajiliwa.

Tobesya: Ulijuaje hazitumiki?

SHAHIDI: Unatype www.jf.co.tz nlipo-type hakuna kilichotokea.

Mtobesya: Wakati unaongozwa na wakili wa Serikali ulipata wasaa wa kuionesha mahakama kwamba ulitype haikuonekana.

SHAHIDI: Sijapata wasaa.

Mtobesya. Sasa ukipata hiyo nafasi ya kufanya hivyo, unaweza kuthibitisha matokeo yale yale uliyosema?

SHAHIDI: Tangu siku hiyo sijawahi kutembelea tena lakini inaweza kuwa tofauti pia ukitembelea

Mtobesya: Tuambie zimesajiliwa lini?

SHAHIDI: Jamiiforums. Co. Tz imesajiliwa 20/06/2016 na imesajiliwa na Extreme Web Technologies na aliyesajili anaitwa Mohamed Saleh.

Jf. Co. Tz. Imesajiliwa 24/11/2016 kupitia wakala IT-Farm aliyesajili ni Jamii Media inc.

Mtobesya: Je kunaweza kuwa na tofauti tangu uitembelee?

SHAHIDI: Inawezekana.

Sasa anauliza Maswali Wakili Jebra Kambole.

Kambole: Kwa uelewa wako, haumjui mmiliki wa JamiiForums.com si ndio?

SHAHIDI: Ni kweli simfahamu.

Kambole: Anaweza kuwa Mike, Max au mtu mwingine si ndio?

SHAHIDI: Kweli sifahamu.

Kambole: Wakati unahojiwa umesema kikoa hakitumiki si ndio? Je mahakamani kuna ushaidi kuonesha kwamba hakitumiki?

Shahidi: Ni kweli hakuna Ushahidi kuonesha kwamba hakitumiki.

Kambole: Kwakuwa ushahidi haujaletwa kama haitumiki, inaweza kuwa inatumika au haitumiki. Si ndio?

Shahidi: Sahihi kabisa.

Kambole amemaliza.

Kesi imeahirishwa hadi Tarehe 17/10 tutaendelea ambapo shahidi ataendelea kutoa ushahidi. Dhamana kwa washitakiwa zinaendelea.
 
Back
Top Bottom