Kesi namba 457 (Jamhuri vs JamiiForums): Shahidi wa nne atoa ushahidi, kielelezo chake chazua mjadala

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Wakuu,

Kesi namba 457 inayoikabili JamiiForums, kuhusu kampuni ya CUSNA Investment ambayo ilidaiwa kufoji nyaraka bandarini, kukwepa kodi na kuwatesa wafanyakazi wazalendo na kupendelea wageni toka nje ya nchi, imeendelea kusikilizwa leo kwa kusikilizwa shahidi wa nne.

Kesi hii ipo chini ya Hakimu Godfrey Mwambapa. Wakili wa Jamhuri alikuwa Batilda Mushi na mawakili wa Utetezi walikuwa Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya na Jebra Kambole.

Shahidi wa kwanza alishahojiwa hapa: ‪Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai Polisi hawana utaalamu wa kulazimisha kuingilia mawasiliano kimtandao.

Shahidi wa pili alitoa ushahidi pia hapa > KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri dhidi ya JamiiForums) yaendelea - Shahidi wa Pili atoa ushahidi wake

Shahidi wa tatu pia akatoa ushahidi wake hapa > KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri dhidi ya JamiiForums) yaendelea - Shahidi wa Tatu atoa ushahidi wake

Katika kesi hii, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada na mchangiaji mmoja ili waweze kuwakamata na kuwahoji kwani kampuni ya CUSNA ilidai ilichafuliwa; JamiiForums inadaiwa ilikataa kutoa taarifa binafsi za wanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa wahusika na kuelezwa kosa lililofanywa na wahusika.

Fuatilia mlolongo wa shauri hilo ulivyokuwa leo katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu iliyopo Jijini Dar es Salaam.

======

Shahidi huyu wa nne anaitwa Jonas Wilson Mcharo, anafanya kazi CUSNA Investment na amesema kwa dini ni mkristo na kaapa kuwa ataongea ukweli mtupu mbele za mahakama.

Wakili wa Jamhuri, Batilda Mushi ndiye anamuongoza Shahidi katika kutoa ushahidi wake.

Shahidi: Mimi naitwa Jonas Wilson Mcharo na nina umri wa miaka 41.

Wakili: Unafanya kazi wapi?

Shahidi: Nafanya kazi kampuni ya CUSNA investment

Wakili: Toka lini?

Shihidi: Nimefanya kazi hapo tangu mwaka 2009

Wakili: Nafasi gani?

Shahidi: Katika nafasi ya utawala

Wakili: Majukumu yako ni yapi?

Shahidi: Kusimamia wafanyakazi kuajili nk.

Wakili: Kampuni yenu inajihusisha na nini?

Shahidi: Kutoa mizigo bandarini

Wakili: Na nini kingine?

Shahidi: Basi ni hizo tu, hatufanyi kazi nyingine

Wakili: Kwanini upo mahakamani?

Shahidi: Nimeitwa kutoa ushahidi kuhusu kampuni yetu ya CUSNA Investment kama ilivyoandikwa kwenye Mtandao wa Jamii Forum kwamba inakwepa kodi na imetorosha makontena bandarini.

Wakili: Jamii Forum umesema ni nini?

Shahidi: Jamii Forum ni mtandao wa jamii

Wakili: Tuelezee, nini kilitokea?

Shahidi: Tarehe 8 Februari 2015 nliingia kwenye mtandao wa Jamii Forum nikakutana na maandishi (Wakili wa Jamhuri anadakia > Na wewe pia ni member wa Jamii Forums?] hapana.

Shahidi: Nilikutana na maandiko kwamba kampuni ya CUSNA inahusika na wizi wa makontena bandarini na alikuwa ameandika JF Senior member. Yale maelezo yalikuwa yanaichafua kampuni yetu sababu kampuni yetu haijawahi kufanya wizi wa makontena wala haijawahi kukwepa kodi.

Wakili: Andiko lilielezea nini?

Shahidi: Kwamba kampuni inakwepa kodi, hailipi kodi pia alieleza kampuni inahusika na wizi wa makontena bandarini. Na pia walisema kwamba kuna wageni ambao wanafanya kazi ambao wana vibali lakini hawana uhalali wa kufanya kazi pale.

Wakili: Wewe ulifanyaje sasa?

Shahidi: Baada ya kusoma haya maandiko, nilimuonesha bosi wangu, na baada ya kujadiliana kama Uongozi, tarehe 14/12/2015 tuli-print lile andiko na bosi akaniambia niende kuripoti Polisi. Nililiport 15/12/2015. Baada ya kuripoti tulikuwa tunafuatilia mara kwa mara kujua maendeleo ya aliyetuchafua yamefikia wapi.

Wakili: Mlishapata mlichokuwa mnakitafuta?

Shahidi: Hatujapata kwa kweli, tumeshitukia tunaitwa kuja kutoa ushahidi.

Wakili: Ukiliona hilo andiko, unaweza kulitambua?

Shahidi: Naweza kulitambua kichwa cha habari na andishi. Kwa kuwa mimi ndo nili-print. Mwandishi wa hilo andiko ni JF senior member.

(Wakili wa Jamhuri anampa print out shahidi aitambue)

Shihidi anaendelea kuelezea huku ameshika karatasi aliyopewa na Wakili wa Jamhuri: Huyu mwandishi na kichwa cha habari na sehemu niliposaini nimevitambua (anaonyesha aliposaini)

Wakili Batilda: Je, hiki ulichoki-print ulikifanyia nini?

Shahidi: Niliangalia nikaona kipo sawa.

Wakili Batilda: Je, hiki ulichoki-print unapenda kukitoa kama kielelezo hapa mahakamani?

Shahidi: Napenda kukitoa kama kielelezo.

…Hapa mawakili wa utetezi wanaingilia…

Wakili Kibatala:
Tunapinga kupokelewa kwa hiki shahidi alichoita “andiko” sababu hakijakidhi vigezo vya kisheria. Kina electronic elements.

Mheshimiwa Hakimu, upokeaji wa electronic evidence kwa mujibu wa commercial case namba 9 ya 2008 kati ya Razarus Milisho Mafie na mwenzake dhidi ya Gaspar Kilenga alias Moiso Gaspar, Uamuzi wa Jaji Makaramba aliweka vigezo vitano ambavyo vinatakiwa viwe vimetimizwa ili ushahidi wa ki-elektroniki uweze kupokelewa.

Yali-reproduce mahitaji ya lazima ya kifungu cha 18 na 19 cha sheria ya Electronic Transactions Act 2015.

Je, kama shahidi ali-print akapeleka Polisi na kwa bosi wake imemrudiaje yeye? Shahidi kama ambavyo umeona, hajaongozwa kutoa hati ya kiapo ya kipindi ana-print hii anayoita “andiko”.

Na hikikinachoitwa “signature”, inaweza kuwa anything... Haiongezi thamani yoyote kwenye hii nyaraka. Zaidi ya maneno ya shahidi, hakuna ushahidi ambao mahakama inaweza ku-compare.

Bila kukuchosha sana Mhe. Hakimu, tunapinga kupokelewa kwa hii nyaraka.

Hakimu: Wakili wa Jamhuri, umeyasikia hayo maelezo?

Wakili Batilda Mushi: Nimeyasikia maneno ya Wakili Kibatala, but I need to see the case and I need to read it, hivyo ningependa kupewa muda kuja ku-respond.

Hakimu amesema hamna tatizo, tukutane tena baada ya muda mfupi.

===========

Session 2 (baada ya nyaraka kupatikana na Wakili wa Jamhuri kuipitia kesi husika) inaanza…


Wakili wa Jamhuri: Tunapenda kujibu hoja kwa upande wa utetezi kama ifuatavyo;

Kwanza kabisa tunapenda kutoa utetezi wa hoja iliyotolewa kwamba nyaraka iliyowasilishwa hapa mahakamani haijakidhi vigezo vya kisheria. Kwamba hakuna comparison (nothing to compare)

Upande wa mashitaka unasema kwamba utolewaji wa nyaraka hii umefuata vigezo vyote vya kisheria. Shahidi alizungumzia mambo makuu matatu

1. Shahidi ameelezea ni jinsi gani alivyosoma andiko katika mtandao wa Jamii Forums,

2. Ameelezea ni namna gani alivyo-print na kuelezea kile alicho-print kilivyo sawa sawa na kile kilichokuwa kwenye mtandao wa kijamii. Alihakikisha na alikuwa anatazama kama kweli vinafanana kati ya kile anachotaka ku-print na kile kilichopo JamiiForums na alipokuta ni the same ndipo aka-print.

3. Alielezea baada ya kuprint alisaini na kuweka tarehe katika kila kurasa na kisha baada ya kufanya discussion na boss yake alipeleka hiyo doc polisi. Ndilo limesababisha aje kutoa ushahidi hapa makamani

Nikirejea sheria ya mabadiliko namba 15 ya 2017 ambayo ilifanyia marekebisho Sheria ya Ushahidi kifungu cha 33, 40 na 40a ambacho kinasema “in any criminal proceeding, electronic evidence Shall be admissible in court”.

Kifungu hicho hicho nikisoma na kifungu cha 46 cha Electronic Transactions Act 2015(anakisoma)

Kwahiyo, kutokana na fact ambazo nimeshazisema hapo juu, upande wa mashitaka unarudi kwenye kifungu cha 18 cha Sheria ya Electronic Transactions Act.

Kifungu hicho kina-establish Authenticity, Reliability & Admissibility. Na kifungu cha 18a(anakisoma)

Nikianza na reliability: Shahidi alikuja mahakamani aliielezea vizuri mahakama ni jinsi gani alivyoona andiko kutoka JamiiForums na baada ya kufungua akaelezea ni kwa namna gani alivyosoma na ku-print na kwenda kuongea na bosi wake jinsi alivyoona hilo andiko.

Huyu ni mtu wa kwanza aliyegundua hilo andiko. Anafahamu sababu yeye ndo ali-print hivyo yeye ndo anajua kuelezea kama alivyolielezea hilo andiko hapo awali.

Authenticity: Shahidi ameelezea baada ya ku-print na kuona content are the same aliweka signature katika kila page ya andiko hilo na aliweza kuripoti Polisi tukio hilo. Akiwa huyu ndo shahidi pekee anaweza kutuelezea na jinsi alivyotuelezea hii document kwa jinsi alivyoileta mahakamani na sawa na kile alichikiona tarehe 14/12/2015.

Naomba nikurejeshe kwenye kesi ya Kyando. [Hakimu anainglia anakataa asiirejee]

Section ya 18 ya Electronic Transactions Act kifungu d, 18/2b

Katika kifungu hiki, mahakama inapewa...(kaendela kusoma) maelekezo ya Kuukubali ushahidi.

In that manner, this witness has expressed how he generated this Document.

Mheshimiwa, kwenye kifungu admissibility kifungu cha nne. Kinasema for the purpose ... (anakisoma)

Shahidi alikuja hapa mahakamani alielezea jinsi gani alikitoa na baada ya hapo alikipeleka Polisi, Polisi nao as part of this case, watakuja kuileza mahakama ni kwa jinsi gani waliipokea hii Document kwani kuna shahidi mwingine.

Baada ya kauli hii, hakimu anaingilia kidogo…

Hakimu: Kama unategemea mtu kuja kuelezea hili swala unataka tuuweke pending huu ushahidi hadi huyo shahidi atakapokuja?

Wakili wa Jamhuri: Hapana, isiwekwe Pending. Huyu shahidi he is reliable to tender witness to the case.

…anaendelea…

Mheshimiwa nikijibu hoja mbili za mwisho how did document come to the hand of witness…

I said before this is part of other witness which will come to fit. This witness seeks to tender what he worked on and what is knowledgeable about the document.

Kwenye hati ya kiapo, haijaelezea mahali popote mwenye sheria ya Electronic Transactions Act kwamba lazima kuwe na hati ya kiapo ili document hii iweze kupokelewa mahakamani lakini shahidi inampasa kuelezea ni jinsi gani alivyoipata na source alipoitoa ili iweze kupokelewa mahakamani. In this fact, document aliyoitoa mahakamani, yeye ni originator. Na yeye ndo mwenye nguvu ya kuitoa mahakamani.

Nikija kwenye kesi ya Razarius Mafie aliyoisema Wakili Kibatala, it’s true that this case was established five how a document should be admitted to the court. Kipindi kile tulikuwa hatuna hii Sheria ya Electronic Transactions Act. Sheria ya mwaka 2015 ina super power maamuzi ya Mwaka 2008. Na ime-set standards na procedures ya how should be admitted.

Tunaendelea kusema kwamba shahidi ni proper shahidi wa kutoa documents pia na sheria inamruhusu, becomes to the proper. He is originator of Document.

Tunaomba mheshimiwa document hiyo ipokelewe.

Hakimu anampa muda Wakili Kibatala kuongea tena….

Wakili Kibatala: Ni kweli, kesi hiyo ya Mafie katika kitengo cha Biashara ndo ilifanya innovation (waanzilishi) katika hii sheria. Kesi ya Mafie input yake ndo ilitengenezwa kifungu cha 18 na 19 of this law (Electronic transactions Act)

Kwa namna yoyote ile, hajagusia swala la chain of custody ya hii Electronic Evidence ambazo utazikuta kwenye kesi ya Mafie. Tu-assume shahidi ali-print akawakabidhi Polisi na hajasema ilimrudiaje. Ukishakabidhi document Polisi ndio Custodian wa hiyo document anakuwa ni mpelelezi - ndivyo sheria inasema. Sasa huyu shahidi alipatae hii Document?

Katika Chain of custody wanatakiwa wajipange nani anaanza kuja kutoa ushahidi nani afuate. Hatuwezi kusubiri Polisi waje kutoa ushahidi, walitakiwa waje mwanzo, hivyo kwa kushindwa kuleta polisi watoe ushahidi; kwanza mwenzangu amekiri kwamba vigezo vya kisheria havijazingatiwa.

Nini kilikuwa kigumu kwa Polisi kuonyesha kwamba “Ni kweli nimeona, nimeona hiki alichoki-print ndicho hicho kilichopo JamiiForums”. Huyu shahidi tutamuamini vipi? Origination is a question!

Mheshimiwa Hakimu, utakapokuwa unasoma hiyo kesi utaona walikuwa wanazungumzia email. Comparison iliyotakiwa ni comparison by the court sio hiyo yake aliyoisema.

Ni kweli kwamba hizo evidence wakati wa ku-print hazijawekwa kwenye kesi ya Mafie.

Hii ni suspect evidence sababu haijakidhi vigezo vya kisheria hivyo tunasema isipokelewe mheshimiwa Hakimu.

Wakili Kibatala: Nimemaliza mheshimiwa hakimu.

Hakimu Mwambapa: Kesi naiahirisha hadi tarehe 21 Desemba 2017 saa saba mchana.
 
Nimependa Kibatala anavyojua kujenga hoja, nikisoma nyingine ambazo hakuwepo naona kuna kitu muhimu kilikuwa kikikosekana.
 
Kibatala ametulia amejenga hoja ukilinganisha na wakili wa Jamhuri ambaye hajajieleza vizuri
 
Niseme wazi hii kesi naifuatilia kwa karibu sana ,yaani ni kesi inayohuzunisha juu ya uonevu nkali dhidi ya bwana Max ,lakini vituko wanavyojibu mashahidi wa jamhuli nadhani inachekesha kuliko kuhuzunisha...
 
Back
Top Bottom