Kesi namba 457: Jamhuri v JamiiForums - Serikali yafunga ushahidi, uamuzi kutolewa Mei 03, 2018

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Kesi namba 457 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums inayohusu kampuni za Cusna Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi bandarini Dar na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania imeendelea leo Machi 26, 2018 katika Mahakama ya Mkazi, Kisutu mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa.

Jamhuri, kupitia Wakili wake Nassoro Katuga, imeiambia mahakama kuwa inafunga ushahidi katika shauri hili na hivyo kuomba mahakama ipitie ushahidi na kuona kama kuna kesi ya kujibu au la.

Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya amemwomba hakimu muda wa kuweza kupitia ushahidi ili kuonyesha kuwa hakuna kesi ya kujibu. Mahakama imetoa hadi tarehe 09 Aprili, 2018 upande wa washtakiwa uwe umewasilisha ombi lake na upande wa Jamhuri umepewa hadi Aprili 23, 2018 uwe umejibu (counter-reply).

Mahakama itatoa uamuzi kama kuna kesi ya kujibu au la siku ya tarehe 03, Mei 2018.

Ili kujua kesi ilipotokea, soma Kesi namba 457(Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa. Jamhuri yaomba muda wa kupitia upya jalada la kesi
IMG-20180313-WA0019.jpg
 
Mimi sijawahi ielewa hii kesi yaani jambazi analindwa kwa nguvu zote huku watoa habari ndio wanaobanwa tena...wao wanatangaza kuwa kuna wizi unafanyika kwa kutoweka mita ya kusoma mafuta ila mkiendelea kujadili na kutoa maovu ninyi ndio mnashtakiwa tena..
 
Tuombe sana Mungu aingilie kati ili maamuzi ya Mahakama yasiingiliwe na mhimili uliyojichimbia chini, maana JF inawanyima usingizi. Naamini tutashinda.

Tujitokeze kwa wingi mahakamani siku hiyo.
 
Kesi namba 457 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums inayohusu kampuni za Cusna Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi bandarini Dar na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania imeendelea leo Machi 26, 2018 katika Mahakama ya Mkazi, Kisutu mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa.

Jamhuri, kupitia Wakili wake Nassoro Katuga, imeiambia mahakama kuwa inafunga ushahidi katika shauri hili na hivyo kuomba mahakama ipitie ushahidi na kuona kama kuna kesi ya kujibu au la.

Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya amemwomba hakimu muda wa kuweza kupitia ushahidi ili kuonyesha kuwa hakuna kesi ya kujibu. Mahakama imetoa hadi tarehe 09 Aprili, 2018 upande wa washtakiwa uwe umewasilisha ombi lake na upande wa Jamhuri umepewa hadi Aprili 23, 2018 uwe umejibu (counter-reply).

Mahakama itatoa uamuzi kama kuna kesi ya kujibu au la siku ya tarehe 03, Mei 2018.

Ili kujua kesi ilipotokea, soma Kesi namba 457(Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa. Jamhuri yaomba muda wa kupitia upya jalada la kesiView attachment 725742

Mwezi na wiki sahihi ya Kushinda Mateso.
 
whistle blower anaposhikishwa adabu
eti wanapambana na ufisadi..ovyo kabisa
 
Back
Top Bottom