Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Yaani wakati habari za oilcom na CRDB zinaandikwa (2012/4) kipindi hicho ndo kilikuwa cha mwishomwisho Humu cha mijadala yenye tija kwa taifa.

Ila sasa sijui imekuaje humu. Yani mtu akishakula bamia zake kavimbiwa. Anakuja kuanzisha uzi.


uishi miaka mingi Melo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi issue za kusema where we dare to talk openly halafu kuna wakati tunaandika habari za uwongo au uzushi kwa nia za kisiasa au kuchafua watu si sahihi. Inafaa anayeandika habari awe na uhakika. Sio kuchafua tu watu au taasisi. Tunaharibu wenyewe.

Simple, mtu akiandika uongo facts za kupinga alichoandika zinawekwa na ukweli unajulikana.
Shida iko wapi?
 
Wana Jamii Forum,

Wengi mtakuwa mmeshasikia au kusoma juu ya hukumu katika kesi ya Jamii Forum, ambapo Maxence Mello amehukumiwa kulipa faini ya Tshs 3m au kifungo cha mwaka mmoja. Faini imelipwa.

Wengi wameshindwa kuelewa athari za hii hukumu, na wanaiona katika mapana ya hukumu au faini ya Stsh 3 tu, ambayo hata wengine wameita pesa ya mfukoni.

Lakini suala la kujiuliza ni kama tunaelewa athari za hukumu hii kwa JF hapo mbeleni. Kimsingi, hukumu hii inaweza kuweka precedent kwamba kila wakati serikali isipofurahishwa na thread au post ya mwana JF, inawataka JF kutoa taarifa za mtu aliyeanzisha hiyo thread au kuweka hiyo post.

Sasa najua JF ilianzishwa kwa namna ambayo ilitaka kuzuia suala la JF kulazimishwa kutoa taarifa binafsi za wana JF. Lakini hukumu haitambui hili, kitu ambacho kinamweka Maxence na Jamii Forums katika hali mbaya sana.

Sasa hii ni vita ya Watanzania waote katika kupigania uhuru wa kutoa maoni, hatupaswi kuwaachia JF na Mexence peke yao. Kama kuna uwezekano wa kuikatia rufaa hii hukumu tufanye hivyo, na ikiwezekana utaratibu uwekwe wale wote wenye mwamko wa uhuru wa kutoa maoni tuchangie gharama za kuhakikisha uhuru wa Watanzania kutoa maoni kupitia JF haukomeshwi na watawala wachache wanaopenda kukandamiza uhuru wa kutoa maoni.

JF imekuwa mwiba mchungu sana kwa nia dhalimu za wale wote wenye mwelekeo wa kufinya haki za binadamu, unyanyasaji wa watu, utawala wa mabavu na kutofuata sheria, ufisadi, dhuruma na ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza. Hatuwezi kukaa kimya dhidi ya vita hii, ni vita yetu, sio vita ya Macence Mello na JF, ni vita ya Watanzania wote wenye kupenda maendeleo na utandawazi. Hii ndio nafasi nzuri ya kuonyesha loyalty yetu kwa JF. IKiwezekana, tungependa kupata mwongozo toka JF wa nini wana JF tunaweza kufanya kusaidia katika hili.

Naunga mkono hoja.
 
Kichekesho hata mawaziri wanalitumia ili jukwaa kutukanana na raia wa kawaida.

Ukiwa kiongozi lazima uwe tayari kukosolewa ni wajibu hata kukashifiwa ni kawaida Trump watu wanamkashifu hata wa nje ya marekani pale twitter lakini hajamkamata mtu yeyote

Bongo kuna uchochezi gani? unaweza kuchochea nini hapa wakati nchi haina ugaidi wala haujamtishia rais au raia yeyote? kama kweli serikali ipo serious iwe inawakamata hata wanaowakashifu wapinzani na kuandika uzushi juu yao upinzani kama ni usalama uwe pande zote.

Ukiwa hauna kifua ni bora usiwe kiongozi uzuri jf wameshaweka utalatibu habari ikiwa haieleweki uwa wanafuta faster sasa tatizo lipo wapi mnataka mfanye ufisadi mkwepe kodi tunyamaze?

Rufaa inahitajika
 
Hapo Zaman kidogo JF palikuwa mahala pazuri sana kwa kutoa mawazo huru ya aina yoyote lakini Sasa kuna hii limetwa la kuingilia shughuli za serikali ama kupotosha umma ama kuchochea upotevu wa amani, tujifunze kusoma alama za nyakati tujue ni Kipindi gani Tupo na changamoto tulizo nazo kisiasa ili tusijingize matatizoni.

sisemi kuwa wanaharakati waache kupambana ila tu wawe tayari kwa lolote watazame vizuri ni nani wanamuona adui wa maendeleo na wanamkabili kwa namna gani.

hiki ni kipindi cha kuwa makini na muangalifu wakati unatoa maoni kuhusu chochote hasa pale maoni yanapoihusu serikali moja kwa moja.
 
Ni habari njema Kwetu Wadau kama Kesi hii imeisha salama na Faini imeshalipwa kwani ilikuwa inatuweka roho juu juu na angalau sasa wengine tunaweza hata Kuagiza ' Kichuri ' na Kukilia kwa Ugali wa Udaga na Ulezi kwa amani kabisa huku tukiamini kwamba Mtandao Wetu huu ambao kwa Sisi wengine akina GENTAMYCINE ndiyo Kilevi chetu Kikubwa na Starehe yetu iliyotukuka.

Poleni sana Uongozi mzima wa Jamii Media Company kwa Changamoto zote za hii Kesi na poleni hasa Wadau Wakuu Maxence Melo na Mike Mushi ila Washukuriwe mno wale Wadau wote ambao muda mwingi walikuwa wakiipambania JamiiForums kwa namna moja au nyingine juu ya hii Kesi yao hadi leo hii imemalizika rasmi.

Mwenyezi Mungu awatie nguvu, Maisha yaendelee na JamiiForums izidi Kuchanja Mbuga katika Mapambano ya Uhuru wa Habari.
 
Back
Top Bottom