Kesi namba 456 (Jamhuri v JamiiForums): Washtakiwa washindwa kuanza kujitetea. Hakimu ataka kesi kusikilizwa siku nzima Agosti 05

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo Kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar, imetajwa tena leo Julai 03, 2019

Katika kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar chini ya Hakimu Mwandamizi Thomas Simba, washtakiwa wanatuhumiwa kutotoa ushirikiano kwa Polisi walipotakiwa kutoa taarifa za aliyeandika kuhusu OilCom

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Silvia Mitanto huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala

Wakili wa Jamhuri, Mitanto ameiambia Mahakama kuwa shauri hilo lilikuja mbele ya Mahakama kwa ajili ya upande wa utetezi kuanza kujitetea ambapo Washtakiwa wanatakiwa kuanza kujitetea baada ya kukutwa na kesi ya kujibu mnamo Mei 16, 2019.

Hakimu Thomas Simba ameomba kuahirisha shauri hilo kwa kuwa leo anatakiwa kusikiliza kesi ambayo Watuhumiwa wanatoka sehemu mbalimbali nje ya Dar.

Amesema “Leo nina shauri ambalo Watuhumiwa wanatoka nje ya Dar, wapo ‘scattered’ bora ninyi mpo hapa hapa Dar. Naomba tutafute siku nyingine ambapo tutasikiliza shauri hili siku nzima, siku ambayo haina kesi nyingine kabisa.”

Baada ya Hakimu kusema hayo upande wa Jamhuri na ule wa Utetezi ulikubaliana na Hakimu bila pingamizi na kutafuta siku nyingine ya shauri hilo kusikilizwa

Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo hadi Agosti 05, 2019 ambapo litakuja tena kusikilizwa kwa Washtakiwa kuanza kujitetea

Kujua shauri hili lilipotoka awali tembelea:

https://www.jamiiforums.com/threads...i-abadilishwa-shauri-lapigwa-kalenda.1584699/

Pia, kujua mashauri yote ya JamiiForums yanavyoendelea tembelea:

https://www.jamiiforums.com/threads...kesi-za-jamhuri-dhidi-ya-jamiiforums.1395392/
 
Back
Top Bottom