Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums): Wakili wa Jamhuri abadilishwa. Shauri lapigwa kalenda...

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar imeendelea leo Mei 16, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Thomas Simba.

Katika shauri hili, Washtakiwa wanatuhumiwa kwa kukataa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kuzuia kupatikana kwa taarifa binafsi za wateja wa JamiiForums walioandika tuhuma hizo.

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Sylivia Mitanto huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Jeremiah Mtobesya.

Wakili wa Jamhuri, Sylivia Mitango ambaye ni mpya katika shauri hili, ameiomba Mahakama isogeze shauri hili kwa ahirisho la tarehe fupi ili apate wasaa wa kukaa na kupitia jalada zima ili aweze kuendelea na kesi kutokana na kuwa yeye ndio kwanza amekabidhiwa kuendelea na kesi hiyo.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Hakimu Simba alieleza kuwa hili litakuwa ni ahirisho la mwisho na anatamani kesi hii isivuke mwezi Julai iwe imetolewa hukumu.

Aidha, Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana na hoja ya kuahirisha kesi hiyo kwa tarehe fupi na karani wa Mahakama akatamka kuwa kesi hiyo itaitwa tena kwaajili ya kusikilizwa tarehe 03 Juni 2019
 
Back
Top Bottom