Kesi mpya ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Ole Sabaya na wenzake sita yaahirishwa

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Arusha. Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, imeshindwa kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kutokana na hati na ridhaa ya kuruhusu mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo kutokamilika.

Leo Ijumaa Agosti 27, 2021 shauri hilo lilipangwa kwa ajili ya watuhumiwa hao kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo namba 27 ya mwaka huu, mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda.

Katika shauri hilo, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na wakili Felix Kwetukia huku utetezi ukiwakilishwa na wakili Mosses Mahuna.

Wakili Kwetukia aliomba kesi hiyo kusogezwa mbele ili kusubiri nyaraka hizo ambazo zinawezesha kesi hiyo kuendelea katika mahakama hiyo.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Enock Mnkeni maarufu kama Dikdik, Watson Mwahomange maarufu kama Mamimungu, John Aweyo maarufu kama Mike One,Sylvester Nyengu maarufu kama kicheche, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Hakimu Kisinda ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9,2021, huku watuhumiwa wakirejeshwa gerezani kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana.

sabayapic.jpg
 
Back
Top Bottom