Kesi kuhusu kujiuzulu Spika: Mbatia atabezwa, lakini ana hoja

Rais kushinikiza spika kujiuzulu yenyewe tu inavunja katiba, kwani inaondoa dhana nzima ya kujitegemea kwa mihimili kiutendaji ili kuleta checks and balance.............the only way forward ni rais kuvunja bunge nchi irudi kwenye uchaguzi.
Kweli tupu
 
kupoteza sifa kutokana na haya madaraka ya kisiasa
1. kujiudhulu
2. kifo
3. magonjwa ya afya ya akili
4. kutenguliwa wazifa wako na mahakama
5. kuondolewa uanachama kama wale wanaitwa uviko19
6. kuondolewa udhamini na chama chako
7. kuwa muajiriwa ktk utumishi wa umma
8. kushitakiwa kwa makosa au kosa la jinai
9. kifungo cha maisha au hukumu ya kifo
10. kukosekana ktk kipindi fulani etc
etc

kuna sababu kibao zinawezav muondolea wazifa wake mtu kama yeye au anaye fanna na yeye....

NB:
katiba pia imetoa mwanya ktk sheria zingine... kwa maana na sheria zingine zitatumika ikitokea jambo husika na ndio maana kuna sheria mbalimbali miongozo, kanuni nk kwa maana katiba sio kila kitu
 
Labda tusaidie what outcome from the will please Mbatia? And what will change given the circumstances kuzuia Dr Tulia kuwa speaker.

Hapa ndipo nilipokuwa nampendea Magufuli ujinga ujinga kama huu alikuwa aupi nafasi kabisa zaidi ya kucheleweshana kwenye kazi tu kwa tafsiri yake.
Basi tuachane na katiba na sheria tuendeshe nchi kwa mapenzi ya kila mtu na logic.
 
Kila kitu kinawezekana nchi hii
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.

Nimekuwa nikifuatilia maoni ya watanzania na wasio watanzania kwenye mitandao ya kijamii, mitaani, runingani na redioni kuhusu kesi iliyofunguliwa na Mbatia. Wengine wanamuona Mbatia akitaka Ndugai abaki kuwa Spika wa Bunge kwa njia ya Mahakama. Wapo wanaomuona Mbatia kama anayepoteza muda na 'fedha' zake kwa jambo lisilo na maana na kuwa jambo hilo limeshapitwa na wakati. Wapo wanaompongeza. Lakini, wengi wanambeza.

Suala la utetezi wa Katiba ni suala kubwa na la muhimu kwa kila mmoja wetu. Kila Mtanzania, kwakuwa Katiba ni sheria yetu mama, anapaswa kuilinda na kuitetea katiba yetu. Katiba inapotoa masharti ya kufuatwa, lazima yafuatwe. Katiba imetoa masharti ya kufuatwa na Spika anayetaka kujiuzulu. Ni lazima yafuatwe. Mbatia ameona hayakufuatwa. Amekwenda mahakamani kuitetea na kuilinda Katiba yetu iliyotoa masharti ambayo ameona yamekiukwa. Ni haki yake na anafanya jambo jema.

Viongozi wetu, wanapoapishwa, huapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria zote nyinginezo (zinazotungwa na Bunge na zile Ndogondogo) hazipaswi kukinzana na Katiba. Pale zinapokuwa kimya, Katiba hutumika. Haipendezi kushabikia viongozi ambao hawaifuati Katiba yetu kwa minajili ya kuilinda na kuitetea kama walivyoapa. Tena, viongozi wenyewe ni wale wanaotokea kwenye Bunge ambalo ndilo linalotunga sheria.

Si sawa Athumani, aliyedhaminiwa na Musa kupata kazi kwa Ally, kuandika barua yake ya kuacha kazi akiielekeza kwa Musa huku akitoa nakala tu kwa Ally-mwajiri wake. Hapo, aliyepaswa kuandikiwa barua husika ni mwajiri ambaye ni Ally na nakala inaweza kuelekezwa kwa Musa ikimpendeza Athumani. Kimsingi, Mbatia ana haki na hoja za kufungua shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania kupata tafsiri ya kikatiba juu ya suala hilo. Atabezwa lakini atabaki na hoja yake.
 
Katika hayo maelekezo yao awawezi mlazimisha Ndugai kuwa speaker tena kama ataki. If anything ataandika hiyo barua wanavyotaka kama hakuna manufactured copy to date huko bungeni.

Na awawezi lazimisha CCM kurudia mchakato wao wa kupendekeza jina la speaker kwa sababu it internal process.

So regardless of the court decision in the end the whole thing is waste of time.
Ndugai hawezi kulazimishwa kuwa Spika na mchakato wa CCM wa kumpata mgombea uspika siyo suala la kikatiba au sheria za nchi. Kitendo cha Ndugai kuondoka kienyeji bila kufuata katiba na sheria za nchi kunaweza kutafsiriwa kama ame-abscond na hivyo kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa na pamoja na kufukuzwa kazi na kukosa stahiki zake zote za uspika!
 
Katika hili, mimi naona kama Mh. Mbatia amekosea focus, kama kweli nia yake ni hiyo. Yeye alitakiwa akafungue kesi ya kuzuia mchakato wa kumpata spika mpya, kama anaona yule wa zamani hajajiuzulu, na si kwenda kumtaka aliyejiuzuru ajiuuzulu kisahihi; akigoma je? Huyu mtu ameshaachia ngazi na hiyo post haihitaji, kama amekosea utaratibu wa kujiuzulu basi anaweza akaamua atakavyo.

Iwapo Mbatia angefungua kesi ya kuzuia mchakato wa kumpata spika mpya, mamlaka husika zingemgeukia yule aliyejiuzulu na kumtaka ajiuzulu kulingana na utaratibu. Mh. Mbatia hana mamlaka yoyote kisheria ya kumlazimisha Mh. Ndugai ajiuzulu kwa kufuata Katiba. Unless kama anatarjia hukumu ya Mahakama ya kumlazimisha Mh. Ndugai ajiuzulu kwa kufuata utaratibu, asuming kweli utaratibu haukufuatawa
Viongozi wetu wameapa kuilinda katiba ya nchi na si vinginevyo, akikiuka Katiba anakuwa mhaini na anaweza kushtakiwa na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.
 
Huwa namuelewa sana Mbatia na najua anajua anachokitetea ni haki na wanaopingananae wanajua yupo sahihi kikatiba kwakuwa imekiukwa lakini ccm wapo tayari wauwe mtu wakishaamua jambo lao, siku zote wao wapo sahihi iwe utataka meza ya maridhiano au ulingo wa mapigano kote mtaenda sawa ila mwisho wa mchuano ushindi ni wao halina kupingwa.
 
Katiba inasemaje kuhusu yeye kugombea akiwa ndiye naibu spika ambaye kwa sasa ndiye Spika wa mpito??
amechukua fomu ya kugombea u-spika?
hiyo hoja itakua na nguvu kama akichukua fomu ya kugombea, kwa sasa yeye bado amekaimu nafasi ya spika......
 
Suppose speaker akufuata katiba kwenye kujiudhuru. What outcome is Mbatia seeking iwapo Ndugai hana interest ya kuwa speaker tena?

Anataka Ndugai aandike barua kwa taratibu sahihi? and then what?

The only logical explanation of going through all this trouble iwapo Ndugai angekuwa interested.

Otherwise maamuzi yoyote ya mahakama speaker atakuwa Dr Tulia mwisho wa siku I do not see CCM kurudia mchakato wa kupendekeza jina la speaker, hakuna mtu atafukuzwa kazi, hakuna sheria itabadilishwa, and so forth it changes nothing in the end. Zaidi ya speaker kujiudhuru kama wanavyotaka.

Now that is a waste of court time and resources kusikiliza case kama hizo.
Ndo wasomi wa Tanzania mlivyowajinga.awe/asiwe spika tulia,lkn katiba ifuatwe.ndo logic ya ya mtoa mada
 
Wake wanaombeza Mbatia Ni watu wasioelewa katiba vizuri,na ndio haohao wanasema katiba inafaa ileile,ndio maana mataifa mengine yatushangaa kwa kushindwa kudai haki yetu kwa vitu ambavyo vinatuumiza,mf hizi tozo za miamala zinapigwa mchana kweupe na hazionyeshi exp date,watu wanajiuzulu tu bila kufuata utaratibu.
 
Suppose speaker akufuata katiba kwenye kujiudhuru. What outcome is Mbatia seeking iwapo Ndugai hana interest ya kuwa speaker tena?

Anataka Ndugai aandike barua kwa taratibu sahihi? and then what?

The only logical explanation of going through all this trouble iwapo Ndugai angekuwa interested.

Otherwise maamuzi yoyote ya mahakama speaker atakuwa Dr Tulia mwisho wa siku I do not see CCM kurudia mchakato wa kupendekeza jina la speaker, hakuna mtu atafukuzwa kazi, hakuna sheria itabadilishwa, and so forth it changes nothing in the end. Zaidi ya speaker kujiudhuru kama wanavyotaka.

Now that is a waste of court time and resources kusikiliza case kama hizo.
Interest anayo ndio maana aliomba msamaha Ila vishoka wakaibuka kumshambulià.
 
Hivi endapo job kesi akashinda na hapo hapo ikawa kushapatikana supika mwingine ambae ameshaapishwa inakuwaje hapo
 

2878995_images_9.jpeg
 
Back
Top Bottom