RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Harry Msamire Kitilya (kushoto) na Sioi Graham Solomon (kulia) wakiwa mahakamani leo wakisubiri kesi yao kuanza.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kuwa jalada la kesi inayowakabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwenyekiti wa Enterprise Growth Market Advisors Ltd (EGMA), Harry Msamire Kitilya na wenzake kimsingi bado lipo Mahakama Kuu na kwamba washtakiwa hao wanatakiwa kwenda leo mbele ya Jaji Mfawidhi kwa maelekezo mengine.
Hayo yamesemwa leo na Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru pale kesi ya washtakiwa hao ilipokuja kwa ajili ya kutajwa baada ya mawakili wa pande zote mbili kusema ya kuwa kesi hiyo imekuja leo kwa ajili ya kupata maelekezo kutoka Mahakama Kuu kama ilivyoamuliwa mara ya mwisho.
“Kimsingi jalada la kesi hii bado lipo Mahakama Kuu na leo hii tulitarajia tupate maelekezo ya nini kifanyike lakini washtakiwa wote wanatakiwa kwenda kwa Jaji Mfawidhi leo hii kwa maelekezo zaidi ya nini kitafuata,” amesema Hakimu Mchauru.
Akiahirisha kesi hiyo hadi Mei 18, mwaka huu, Mchauru amesema washtakiwa hao wataendelea kukaa rumande hadi siku kesi hiyo itakapotajwa tena hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Chanzo: HiviSasa Blog