Kesi ‘Kifaru cha Jeshi’ yapigwa kalenda

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
UPELELEZI wa kesi inayowakabili Musa Mkama, Mhariri wa Gazeti la Dira na Prince Newton, mwandishi wa gazeti hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeahirishwa, anaandika Faki Sosi.

Wanahabari hao wanatuhumiwa kuandika habari za uongo na kudaiwa kuzua mtafaruku kwa jamii. Habari hiyo ilipewa kichwa cha habari ‘Kifaru cha kivita cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), chaibwa.’

Easter Martn, wakili wa serikali amedai kuwa, upelelezi wa kesi haujakamili hivyo ameimba mahakama kuahirisha shuri hilo.

Hakimu Respicius Mwijage, amehairisha kesi hiyo hadi tarehe 10 Julai Mwaka huu.

Watuhumiwa wa kesi hiyo wanadaiwa kutenda kosa hilo 20 Juni mwaka huu katika eneo la Kinondoni Biafra, jijini Dar es Salaam.

Na kwamba, washtakiwa hao waliandika na kuchapisha habari za uongo katika gazeti hilo toleo namba 424 la tarehe 20 hadi 26.
 
Vipi ndugu yangu wa kule HQ hajapatiwa nafasi ya kumaliza jambo hili haraka haraka maana tulihadiwa kuwa adhabu ya mateso / ukatili haviepukiki.
 
Waache kutisha watu bana, kesi si kweli ilikuwa mahakamani? sasa wao waliandika kama charge ilivyopelekwa mahakamani dhidi ya washtakiwa!
 
Back
Top Bottom