Kesi inayomkabili Maxence Melo yapigwa kalenda hadi Mei 2, 2017

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,270
MAX.jpg


Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media, Maxence Melo ya Kuzuia upelelezi iliyokuwa isikilizwe Jumatatu hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirishwa hadi Mei 2, 2017.

UPANDE wa Mashtaka umewasomea maelezo ya awali Wakurugenzi wa JamiiForums baada ya kukamilisha upepelezi katika Kesi inayowakabili ya kushindwa kutoa taarifa za kiuchunguzi wa Jeshi la polisi.

Salumu Mohamedi wakili wa Serikali mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliwasomea maelezo watuhumiwa hao.

Katika maelezo hayo wakili Salumu Mohamedi alisoma kuhusu umiliki wao wa mtandao wa JamiiForums, makazi yao, majukumu yao na kuhusu mashtaka yao.

Washtakiwa wote walikubali maelezo hayo.

Katika kesi hiyo namba 456 yenye shitaka moja ambapo inadaiwa kuwa tarehe Mosi Aprili , tarehe 13 Desemba mwaka huu, huko Mikocheni wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii media inayoendesha mtandao wa JamiiForums alishindwa kutoa taarifa za kiuchunguzi zilizochapishwa kwenye mtandao huo kwa Jeshi la polisi.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 2 mei mwaka huu.
 
Back
Top Bottom