Kesi iliyoko mahakamani; tahadhari inahitajika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi iliyoko mahakamani; tahadhari inahitajika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 19, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,999
  Likes Received: 37,703
  Trophy Points: 280
  Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa wanasheria kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuelimisha umma wa watanzania ili tuelewe nini mantiki ya jambo lilliloko mahakamani kwa maana ya kutolijadili jambo hilo.Tunahitaji kuelewa ni nini hasa kisichostahili kujadiliwa na ni ktk mazingira gani ili tuepuka kudanganywa.
  Tusipochukua tahadhari kuna hatari ya serikali kutumia kisingizio hicho kuzima mijadala kwa manufaa ya watu wachache.Wanasheria na wadau wengine mna wajibu wa kupaza sauti kwani si dhani kama sheria hii inatumika sawa sawa.Mkiendelea kukaa kimya itakuwa ni mazoea na itazuia haki kutendeka na itakuwa na mbinu chafu ya kuficha uovu.
  Binafsi ingawa mimi si mwanasheria, napata shida sana kuamini kama hata kuelezea tukio lilivyotokea kwa maana ya kutoa taarifa nako ni kuingilia uhuru wa mahakama.
  Wadau jambo hili si la mzaha na kuna umuhimu wa kuchukua hatua kabla mambo hayajaharibika zaidi.Ipo siku tutajuta kama taifa endapo jambo hili litaendelea kupuuzwa.
   
 2. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kaka nakuunga mkono 100%.kwel bwana ni wakati wa kujua mipaka ya hayo mambo mawili.wanasheria okoeni jahazi.
   
 3. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  Wanasheria wenyewe ndo wapindua sheria,Limtu kama werema linafaa kupigwa viboko..halina uchungu wa hii nchi kabisa linawaza tumbo lake....
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,999
  Likes Received: 37,703
  Trophy Points: 280
  Mkuu unahitaji kuungwa mkono kwani hii issue sasa inaelekea kuwa janga la kitaifa.
   
Loading...