Kesi iliyofunguliwa na Wazanzibari uhalali wa Muungano bado yaendelea

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Tanganyika Ndio itayo vunja muungano wetu, kuna kila sababu ya kusema haya, Tanganyika miaka zaidi ya 55 haitaki kuwa sikiliza viongozi wa zanzibar katika kuondoa kero za muungano wala kuwa sikiliza wananchi.

Viburi vikubwa kwa viongozi kwa wananchi wake eti kulinda muungano kwa gharama yoyote, kwa maana hata kuuwa, hiki kizazi sio cha 1960, ni kizazi tofauti kabisa.

Kizazi hiki kina taka mabadiko ya nchi, kisiasa na kijamii, uhuru wa kijieleza na haki za kibinadamu, kizazi hiki hakipendi kabisa kuishi kwa unyonye.

Muungano utavunjika tu, haukuletwa na mungu huu, wala sio chaguo la mungu, mjiandae ki saikolojia.

IMG-20190428-WA0002.jpeg
IMG-20190428-WA0001.jpeg
 
Ndoa ya Tanganyika & Zanzibar ni mpaka kiama, ndoa hii haina talaka dogo
 
Dhambi ya ubaguzi itawaandama hata nje ya muungano tutawakaribisha tu kama wakimbizi ikiwa ndani ya znz yenyewe mnabaguana
 
Yaaani Muungano adheem wa Kipekee Duniani ukavunjwe na kigenge cha Majaji na Mawakili!

Mnachekesha kweli!
 
Mbona Kiingereza kibovu hivyo katika barua hiyo?! Huyu Petitioner ameshashindwa hata kabla kesi haijaanza kusikilizwa!
Mtu anayetaka ku-challenge Muungano wetu lazima awe na akili kubwa na si hawa wanywa kahawa na wacheza dhumna!
 
Huu Muungano ni wa kipekee!
Kulikuwa na Nchi mbili, Majina yake yakaunganishwa tukapata Tanzania.
Kutoka kwa Tanganyika na Zanzibar.

Lakini inashangaza Zanzibar bado ipo na wako watu wanajivunia Nchi yao, wakati Tanganyika wengine tumeisikia Kwenye Historia.
Hatujawahi kujitambua Kama WaTanganyika, lakini wa Tanzania.
Kuna Shida.
Zanzibar inapaswa kubaki Kwenye Vitabu vya Historia Kama ilivyo kwa Tanganyika.
Hakuna namna nyingine.
 
Back
Top Bottom