Kesi iliyofungua Tundu Lissu akipinga kuvuliwa Ubunge na Spika wa Bunge Job Ndugai, imepangwa kuanza kusikilizwa Agosti 15, 2019 Mahakama Kuu

T

The Wakanda Panth3r

Senior Member
Joined
May 22, 2018
Messages
145
Points
225
T

The Wakanda Panth3r

Senior Member
Joined May 22, 2018
145 225
Muda wa kufungua kesi wanao, na wameweza. Ila muda wa chama kama taasisi kusimamia mbunge wao kujaza na kurudisha au kuwasilisha zile fomu hawakuwa nao...?!

Siasa za huruma hizi zina mwisho.
 
P

Pythagoras

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Messages
5,837
Points
2,000
P

Pythagoras

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2015
5,837 2,000
View attachment 1180614

Mahakama Kuu ya Tanzania imemwita mahakamani Alhamisi ya Agosti 15, 2019 aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ikiwa na vielelezo vyote ambavyo anakusudia kuvitumia, katika kesi yake ya kupiga kuvuliwa ubunge na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa hati ya wito wa kufika mahakamani kwa mbunge wa zamani Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa ajili ya shauri la maombi yake kuanza kutajwa.

Wito huo kwa Lissu umetolewa leo Jumanne, Agosti 13, 2019 na kusainiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Lssu amefungua maombi mahakamani hapo chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.

Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka 2019, Lissu anaomba kibali cha kufungua shauri dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, kupinga kuvuliwa ubunge wake.

Shauri hilo ambalo litasikilizwa na Jaji Sirillius Matupa limepangwa kutajwa keshokutwa Alhamisi, Agosti 15, 2019.

Katika hati hiyo ya wito wa kufika mahakamani, Mahakama hiyo imemtaka kufika mahakamani tarehe hiyo bila kukosa na pia awasilishe vielelezo vyote ambavyo anakusudia kuvitumia, katika kesi hiyo.

Mwanasheria huyo Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yuko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Lissu ambaye pia alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni amekuwa nje ya nchi kwa matibabu baada ya kunusurika katika jaribio hilo la mauaji kwa takribani miaka miwili, tangu Septemba 7, 2017, aliposhambuliwa.

Uamuzi wa kumvua ubunge ulitangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai Juni 28, 2019 wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge huku akitaja sababu mbili.

Spika Ndugai alizitaja sababu hizo ni kushindwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu bila kumjulisha Spika kwa maandishi mahali aliko na sababu ya pili ikiwa ni kutokuja taarifa za mali na madeni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Lissu alifungua shauri la maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu, Dar es Salaam, dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiomba kibali cha kufungua shauri la kupinga uamuzi huo.

Kwa mujibu wa hati ya shauri hilo la maombi namba 18 la mwaka 2019, Lissu anaiomba mahakama hiyo, impe kibali cha kufungua kesi ili mahakama hiyo itoe amri ya kumtaka Spika Ndugai ampe (Lissu) taarifa yake ya kumvua ubunge.

Pia, anaiomba mahakama hiyo impe kibali cha kufungua kesi ili mahakama hiyo iite taarifa ya uamuzi wa Spika wa kumvua ubunge na kisha itengue na kutupilia mbali uamuzi huo wa Spika Ndugai kumvua ubunge.

Vilevile Lissu anaomba Mahakama hiyo impe kibali afungue shauri ili mahakama itoe amri ya kusimamisha kuapishwa kwa mbunge mteule wa jimbo hilo, Miraji Mtaturu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Songa mbele kaka Lissu Mungu yuko pamoja nawe.
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
45,524
Points
2,000
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
45,524 2,000
Nyani Ngabu Your boy is not giving up the gun!
 
Kitaturu

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
4,973
Points
2,000
Kitaturu

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2013
4,973 2,000
moot court............a mock court at which law students argue imaginary cases for practice.
Wooh...

That Law student was so good to select his/her characters to create his/her imaginary law judgemental practice writing....!!
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
18,580
Points
2,000
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
18,580 2,000
Wooh...

That Law student was so good to select his/her characters to create his/her imaginary law judgemental practice writing....!!
I guess you have never seen the inside of a law class making a reference from your argument! His/her moot court had a lot to be desired!
 
Kitaturu

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
4,973
Points
2,000
Kitaturu

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2013
4,973 2,000
I guess you have never seen the inside of a law class making a reference from your argument! His/her moot court had a lot to be desired!
Of course, I never....

However, I agree with the last. She/he tried to pick one of the most current incident to practice his/her moot court.....

I agree, it is so desirable....
 
D

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Messages
3,001
Points
2,000
D

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2011
3,001 2,000
Kwa mujibu wa hati ya shauri hilo la maombi namba 18 la mwaka 2019, Lissu anaiomba mahakama hiyo, impe kibali cha kufungua kesi ........
Bado kesi haijafunguliwa mahakama kuu. Hivyo heading ya topic yako si sahihi. Kwa hatua hii ya mwanzo Lisu anaomba kibali cha kufungua kesi hiyo. Mahakama imemtaka afike mwenyewe mahakamani hapo kesho tarehe 15/8/2019 kuwakilisha ombi hilo akiwa na supporting documents za ku justify ombi lake.

Kipi ambacho hakijaeleweka hapo? Kesho kama hajafika hapo mahakamani basi ombi lake linaishia hapo.
 
B

bibinnaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2017
Messages
1,387
Points
2,000
B

bibinnaa

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2017
1,387 2,000
Bado kesi haijafunguliwa mahakama kuu. Hivyo heading ya topic yako si sahihi. Kwa hatua hii ya mwanzo Lisu anaomba kibali cha kufungua kesi hiyo. Mahakama imemtaka afike mwenyewe mahakamani hapo kesho tarehe 15/8/2019 kuwakilisha ombi hilo akiwa na supporting documents za ku justify ombi lake.

Kipi ambacho hakijaeleweka hapo? Kesho kama hajafika hapo mahakamani basi ombi lake linaishia hapo.
Sometimes some people..............
(I reserve.....)
 

Forum statistics

Threads 1,326,257
Members 509,458
Posts 32,215,955
Top