Kesi iliyofungua Tundu Lissu akipinga kuvuliwa Ubunge na Spika wa Bunge Job Ndugai, imepangwa kuanza kusikilizwa Agosti 15, 2019 Mahakama Kuu

W

Wazo Kuu

Member
Joined
Oct 21, 2018
Messages
38
Points
150
W

Wazo Kuu

Member
Joined Oct 21, 2018
38 150
1-jpg.1180614


Mahakama Kuu ya Tanzania imemwita mahakamani Alhamisi ya Agosti 15, 2019 aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ikiwa na vielelezo vyote ambavyo anakusudia kuvitumia, katika kesi yake ya kupiga kuvuliwa ubunge na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa hati ya wito wa kufika mahakamani kwa mbunge wa zamani Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa ajili ya shauri la maombi yake kuanza kutajwa.

Wito huo kwa Lissu umetolewa leo Jumanne, Agosti 13, 2019 na kusainiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Lssu amefungua maombi mahakamani hapo chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.

Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka 2019, Lissu anaomba kibali cha kufungua shauri dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, kupinga kuvuliwa ubunge wake.

Shauri hilo ambalo litasikilizwa na Jaji Sirillius Matupa limepangwa kutajwa keshokutwa Alhamisi, Agosti 15, 2019.

Katika hati hiyo ya wito wa kufika mahakamani, Mahakama hiyo imemtaka kufika mahakamani tarehe hiyo bila kukosa na pia awasilishe vielelezo vyote ambavyo anakusudia kuvitumia, katika kesi hiyo.

Mwanasheria huyo Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yuko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Lissu ambaye pia alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni amekuwa nje ya nchi kwa matibabu baada ya kunusurika katika jaribio hilo la mauaji kwa takribani miaka miwili, tangu Septemba 7, 2017, aliposhambuliwa.

Uamuzi wa kumvua ubunge ulitangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai Juni 28, 2019 wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge huku akitaja sababu mbili.

Spika Ndugai alizitaja sababu hizo ni kushindwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu bila kumjulisha Spika kwa maandishi mahali aliko na sababu ya pili ikiwa ni kutokuja taarifa za mali na madeni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Lissu alifungua shauri la maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu, Dar es Salaam, dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiomba kibali cha kufungua shauri la kupinga uamuzi huo.

Kwa mujibu wa hati ya shauri hilo la maombi namba 18 la mwaka 2019, Lissu anaiomba mahakama hiyo, impe kibali cha kufungua kesi ili mahakama hiyo itoe amri ya kumtaka Spika Ndugai ampe (Lissu) taarifa yake ya kumvua ubunge.

Pia, anaiomba mahakama hiyo impe kibali cha kufungua kesi ili mahakama hiyo iite taarifa ya uamuzi wa Spika wa kumvua ubunge na kisha itengue na kutupilia mbali uamuzi huo wa Spika Ndugai kumvua ubunge.

Vilevile Lissu anaomba Mahakama hiyo impe kibali afungue shauri ili mahakama itoe amri ya kusimamisha kuapishwa kwa mbunge mteule wa jimbo hilo, Miraji Mtaturu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
 
Kitaturu

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
4,973
Points
2,000
Kitaturu

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2013
4,973 2,000
Si kuna uzi ulifunguliwa asubuhi hii ukidai kuwa mahajama imekwisha kutoa uamuzi na kesi ya maombi hayo imetupiliwa mbali....?

Hii ni nini tena? Mbona mnatutuchanganya sana JF? Tena taarifa hiyo ya asubuhi ilionesha source yake ni hawahawa www.mwananchi.co tz....!!
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
18,589
Points
2,000
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
18,589 2,000
Si kuna uzi ulifunguliwa asubuhi hii ukidai kuwa mahajama imekwisha kutoa uamuzi na kesi ya maombi hayo imetupiliwa mbali....?

Hii ni nini tena? Mbona mnatutuchanganya sana JF? Tena taarifa hiyo ya asubuhi ilionesha source yake ni hawahawa www.mwananchi.co tz....!!
That was a student moot court!
 
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
6,669
Points
2,000
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
6,669 2,000
Aug 9, 2019
KAKA WA TUNDU LISSU: MAWAKILI NGULI KUUPAMBANIA UBUNGE WA LISSU, NI KAZI RAHISI
Ni kazi rahisi, jopo la mawakili wasomi kusimamia Tundu Lissu kupata haki yake ya kutambulika ni mwakilishi halali wa jimbo la ubunge la Singida Mashariki nchini Tanzania. Hii inatokana na Mh. Spika Job Ndugai kulitangaza jimbo la Singida Mashariki halina mbunge kutokana na 'utoro' na kutojulikana Tundu Lissu alipo.

 
M

muheza2007

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2010
Messages
330
Points
500
M

muheza2007

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2010
330 500
Kuna kijana alikuwa anajaribu shule yake kwenye mahakama ya chumbani kwake. Haikuwa mahakama ya kweli. Ni mtu alikuwa anaipima. Shule yake.
Si kuna uzi ulifunguliwa asubuhi hii ukidai kuwa mahajama imekwisha kutoa uamuzi na kesi ya maombi hayo imetupiliwa mbali....?

Hii ni nini tena? Mbona mnatutuchanganya sana JF? Tena taarifa hiyo ya asubuhi ilionesha source yake ni hawahawa www.mwananchi.co tz....!!
 
Sakasaka Mao

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Messages
4,185
Points
2,000
Sakasaka Mao

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2016
4,185 2,000
Hizi kesi ndiyo mimi nitapenda kuzisikiliza!

Ipo hii na ile ya Musiba vs Membe.

Hizi kesi hizi, ninatabiri zitatoa matokeo yatakayoacha vinywa vya watu wazi!

Na tukae tusubiri.
 

Forum statistics

Threads 1,326,267
Members 509,458
Posts 32,216,449
Top