Kesi Idara ya Kazi (CMA) Arusha haziishi kwa wakati

Chunda

Senior Member
Apr 7, 2016
188
251
Kuna tatizo kubwa sana la kusikiliza na kutoa uamuzi katika Idara ya kazi Arusha. Wafanyakazi wengi wenye kesi za kazi katika Idara hiyo wamekuwa wakilalamika. Kuna Muamuzi anayeitwa Mnzava kesi zake huchukua hadi miaka mitatu kutoa uamuzi. Muamuzi huyu hujipa kesi nyingi hasa pale anapohisi kesi hizo zitampa chochote.

Muamuzi huyo ni mkuu wa Idara hivyo anayo mamlaka ya kujipangia kesi yoyote anayoona itakuwa na manufaa kifedha kwake. Kwa sasa anazo kesi nyingi ambazo zilikwisha kukamilika katika hatua ya kusikilizwa lakini ni zaidi ya mwaka hajaweza kuandika na kutoa hukumu/uamuzi wa kesi hizo.

Kitendo cha Muamuzi huyu kukalia hukumu/uamuzi kwa muda mrefu hivyo, si tu kinalazimisha rushwa ila kinanyima haki, kwa kuwa haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyonyimwa.

Mheshimiwa Jenister Muhagama anaombwa kutupa macho kwa Mnzava CMA-Arusha
 
Back
Top Bottom