ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Shauri la Kikatiba Na.12 la mwaka 2020 lililofunguliwa na Asasi ya Civic and Legal Aid Organization dhidi ya Mhe. Spika, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Cecil Mwambe ili kupinga ubunge wa Mwmbe imetupiliwa mbali Leo tarehe 15 Juni,2020 na Mahakama Kuu.
Hii ni mara ya pili ambapo Mahakama Kuu inaiondoa kesi hiyo Mahakamani kwa kukosa msingi.
Akitoa uamuzi wake kwenye hoja za Pingamizi dhidi ya shauri hilo zilizowasilishwa na upande wa Serikali, Mhe Jaji Stephen Magoiga amesema kuwa, hakuona hoja za msingi za Mahakama kuendelea kusikiliza kesi hiyo ambayo maudhui yake yanafanana na Shauri la Kikatiba Na. 10 la 2020 lililofunguliwa awali Mahakamani hapo na Wakili Paul Revocatus Kaunda kuhusu Mbunge huyo huyo.
Katika shauri hilo la awali, Mahakama ilitupilia mbali kesi kwa kuwa ilionekana haina msingi na ililenga
katika kuleta usumbufu na kuvuruga taratibu za kimahakama.
Kwa uamuzi huo, Mhe. Cecil Mwambe bado ni Mbunge wa Jimbo la Ndanda.
Kwenye shauri hilo la Kikatiba Na. upande wa Civic and Legal Aid Organization uliwakilishwa na Wakili wa kujitegemea John Seka na Mwambe aliwakilishwa Bw. Dismas Raphael wakati Serikali iliwakilishwa Mahakamani na Wakili wa Serikali Mkuu, Bw. George Mandepo na Erigh Rumisha.