Kesi dhidi ya JF: Mahakama ya Kisutu yabariki Jamhuri kubadilisha hati ya mashtaka! Ni kesi ile ya Oilcom

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Wakuu,

Leo Mahakama ya Kisutu imetoa maamuzi madogo (ruling) ya Kesi namba 456 inayoikabili JamiiForums (inayohusiana na Oilcom na Uchakachuaji mafuta bandarini/Ukwepaji kodi) na Hakimu amesema kubadilishwa huko kwa hati amejiridhisha hakutapelekea haki kutotendeka.

Kesi hii ambayo ipo chini ya Hakimu Thomas Simba, imepangwa kusikilizwa tena tarehe 06 na 07 Disemba na hakimu amewasisitiza upande wa Jamhuri kuja na mashahidi wote siku hiyo. Kesi hii itasikilizwa na kutolewa hukumu kabla ya mwaka kuisha.

photo_2019-12-05_10-39-27.jpg

photo_2019-12-05_12-12-35.jpg


Kupata kujua ilikotokea, soma Kesi dhidi ya JF: Jamhuri yasisitiza kutaka kubadili hati ya mashtaka! Ni ile ya Oilcom... Uamuzi kutolewa Oktoba 30
 
Haya mambo ya Kubadili hati ya mashtaka inamaana wanabadili mashtaka. Sasa hawa Jamhuri wakati wanaenda kushtaki mara ya kwanza walikuwa wanajaribu kwanza au ndo kutokujielewa kwenyewe huku!

Nadhani hiki kipengele cha kubadili mashtaka hakina maana kabisa, hata kama hakileti injustice kwa mshtakiwa.

Live long JF
 
Katika hali ya kawaida max haendi jela wala hatapigwa faini.
Mwaka utaisha na kuanza salama.
 
Back
Top Bottom