Maxence Melo
JF Founder
- Feb 10, 2006
- 4,196
- 13,187
Ndugu, jamaa na marafiki...
Nachukua fursa hii kukushukuruni kwa support ambayo mmetupa tangu kuanza kwa kesi 3 zinazoendelea mahakamani Kisutu tangu Disemba 19, 2016 hadi leo.
Kuanzia kesho, Disemba 05 hadi Disemba 07 (siku 3 mfululizo) kesi mbili zimewekwa kwenye ‘session’ ili zifike tamati. Mwisho wowote wa kesi hizi bado utakuwa ndio mwisho wenyewe, uwe mbaya au mzuri kwa upande wetu.
Na mnamo Disemba 18-20 (siku 3 mfululizo) kesi ya 3 itaunguruma katika Mahakama ya Kisutu.
Tangu nakamatwa mnamo Disemba 13, 2016 hadi leo, nimepata salaam nyingi za kunitakia kila la heri pamoja na timu yangu na wengine ambao hata hawakunijua physically walijikuta wakisimama nami katika kutetea uhuru wetu wa kujieleza na faragha ya watoa taarifa wenye nia njema!
Kesi tatu zenyewe ni hizi:
1) Kampuni ya Oilcom ilidaiwa kukwepa kodi bandarini, Jeshi la Polisi linataka taarifa za aliyeanzisha mjadala huo; sisi tunaamini chanzo cha taarifa hii kilitakiwa kulindwa na si kukamatwa bali Polisi wangefanya uchunguzi.
2) Kampuni ya CUSNA Investment ilidaiwa kufoji nyaraka bandarini na kuwatesa wafanyakazi wazalendo na kupendelea wageni toka nje ya nchi; Polisi walitaka kumkamata mwanzisha mada lakini sisi tunaamini chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema, tulitarajia iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.
3) Kuwa na Tovuti ambayo ni .COM. Hapa sitii neno...
Yeyote aliyetuunga mkono (kwa namna yoyote) hata bila kujua tunapigania nini nasema ASANTE. Karibuni tujumuike pamoja Kisutu tarehe hizi hadi hatma ya kesi hizi.
Asanteni sana watanzania!