‪Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai Polisi hawana utaalamu wa kulazimisha kuingilia mawasiliano kimtandao‬

Duh Kuna Tatizo la Muingiliano wa Kazi Idara ya Upepelezi kuna vitu vinakosewa sana either hawajui Sheria au Elimu dot com unaionaje?

Wapelelezi wadogo wanayumbishwa na Mabosi wao na wao wanatambua kabisa makosa yapo ila jeshi ni Amri hapo ndipo utata so Mahakamani lazima uchemshe...

Ndio Maana Masamaki yuo Huru Japo nasikia kila siku anashinda Takukuru Kuna viyoyozi lakini analowa Jasho.. Takukuru kumbe sio pa Mchezo mchezo...
Fafanua hapo kwenye Kushinda
Takukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna haja ya kubadilisha mtaala wa mafunzo ya polisi. Wawe na walau miezi 6 ya ziada ya kusoma sheria kwa utulivu wanapokua kwenye mafunzo ya awali. Na waendelee kufundishwa kadili wavyozidi kupata uzoefu.

Haipendezi watu wanopaswa kulinda sheria hawaijui vizuri hiyo sheria yenyewe. Na ndio maana wanapenda kutumia nguvu na ukorofi kama migambo vile!!
Huo mda bado sana kupambana na mtu alosomea shahada ya sheria(bachelor of laws) miaka 3/4 pamoja na law school au bar exams
 
Jamani mnakumbuka jinsi FBI walivyoshindwa "kubreak in" Kwenye simu ya gaidi wakaiomba Kampuni ikakataa ili kutunza usiri wa wateja? Walifanikiwa tu walipompata jamaa mbadala tu aliyewasaidia.

Sioni ajabu hilo kutokea Tanzania pia. Tuwe "fair" wakati mwingine JF Great Thinkers!
 
Yaani nilitegemea kusikia objections kadhaa kutoka kwa mawakili wa Serikali...kama mbinu za kupunguza maswali kwa shahidi wao, kwa mfano lile swali la kasuku...ingepigwa objection pale...lakini daah ...hawa ndio mawakili wetu wanaotuwakilisha kwenye kunegotiate mikataba wanaobakia kusema yes yes yes...yah yah yah...kwi kwi kwi kwi
Objection kivipi? Kasuku anakariri,kukopi na kupesti. Monica na mabosi wake wamefanya hivyo hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibatala huwa napishana nae tu katika itikadi zetu za Kisiasa ila ' Kiutendaji ' hasa wa masuala ya ' Kisheria ' huyu Jamaa ni moto wa kuotea mbali. Kuna Watu wameenda huko Vyuoni Kusoma tu na kupata Vyeti ila kwa Wakili ' Msomi ' Kibatala ama hakika alienda Kuelimika na ' ametukuka ' Kisheria.

Uongozi wa Jamii Media anzeni tu kuandaa ' Sherehe ' tujipongeze kwani kwa aina hiyo ya utiririkaji na usererekaji wa Wakili Msomi Peter Kibatala tayari mmeshashinda Kesi hivyo tembeeni tu Kifua mbele. Huyo Wakili Kibatala nataka kumfananisha na Kiuongo mpya na mahiri kabisa wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi huku ' Mtaalam ' wangu Tundu Lissu nikimfananisha na ' midfield maestro ' Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima.

Wote mnaosoma Sheria huko Vyuoni hakikesheni role models wenu wanakuwa ni akina Lissu, Kibatala na ' Brazameni ' Msando kwani wameiva Kisheria hadi raha.
Ulipocompare na timu ya Ndala sports club tu, basi post yako yote imenajisika. Sikupi Like

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Jamani mnakumbuka jinsi FBI walivyoshindwa "kubreak in" Kwenye simu ya gaidi wakaiomba Kampuni ikakataa ili kutunza usiri wa wateja? Walifanikiwa tu walipompata jamaa mbadala tu aliyewasaidia.

Sioni ajabu hilo kutokea Tanzania pia. Tuwe "fair" wakati mwingine JF Great Thinkers!

mkuu.. hiyo fair haipo... maana hamna demokrasia

inachekesha pale inspekta msaidizi kuulizwa swali la kuingilia migumo ... akajibu mifumo ina mipaka... yaani hajui IT wala mipaka ya mamlaka yake...
 
Back
Top Bottom