Kesi dhidi ya JamiiForums, namba 458: Jamhuri yafunga Ushahidi baada ya Tully Mwambapa kutoa Ushahidi. Kesi itaendelea 20 Agosti 2020

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums na Mwanahisa wa Jamii Media) inatajwa tena leo, Julai 30, 2020 majira ya saa 3 asubuhi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar

Mara ya mwisho iliposikilizwa Juni 25, 2020 Jamhuri iliiomba Mahakama iruhusu kukamatwa kwa Shahidi Tully E. Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma (CRDB) kufuatia kesi hiyo kuahirishwa kwa takriban mara 9

Katika shtaka la kwanza, Mkurugenzi wa Jamii Forums anatuhumiwa kuendesha mtandao (JamiiForums.com) ambao haujasajiliwa Tanzania na vile vile hautumii Kikoa cha do-TZ

Katika shtaka la pili la Shauri hili, Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa Jamii Forums kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums.com waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea katika Benki ya CRDB

Taarifa zilizotakiwa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Pia ilitakiwa zitolewe post zote zinazohusu Uhalifu unaofanyika CRDB kitu ambacho Polisi wanadai Mkurugenzi huyo aligoma kuwapa

Taarifa zilizotakiwa ni za Wanachama walioanzisha mijadala inayosomeka "Charles Kimei (CRDB) jiuzulu, kashfa ya kontena, tiketi TFF, wanafunzi na ujambazi CRDB" mjadala unaodaiwa kuanzishwa tarehe 18 Januari 2016 pamoja na "Wizi wa Banki ya CRDB - Part II" unaodaiwa kuanzishwa Machi 11, 2015.

Soma namna Mahakama ilivyoridhia ombi la Jamhuri la Shahidi kukamatwa: ‪Kesi namba 458 dhidi ya JamiiForums: Jamhuri yaomba Hati ya kukamatwa Shahidi, Mahakama yaridhia!‬

Shauri hili ni mojawapo ya mashuri matatu yaliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya JamiiForums. Kufahamu mashauri mengine ambayo tayari yamemalizika, soma Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums

- UPDATES -

IMG_20200731_110920_862.jpg

Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums na Mwanahisa wa Jamii Media) imetajwa tena leo, Julai 30, 2020 majira ya saa 3 asubuhi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar

Mara ya mwisho iliposikilizwa Juni 25, 2020 Jamhuri iliiomba Mahakama iruhusu kukamatwa kwa Shahidi Tully E. Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma (CRDB) kufuatia kesi hiyo kuahirishwa kwa takriban mara 9

Baada ya kusubiriwa kwa zaidi ya mwaka aje kutoa Ushahidi, leo Shahidi Tully Esther Mwambapa, amefika Mahakamani Kutoa Ushahidi. Ameanza kuulizwa Maswali na Wakili wa Jamhuri Faraja Nguka

Wakili wa Jamhuri: Tukumbushe umetuambia unaitwa nani?

Shahidi: Tully Esther Mwambapa

Wakili wa Jamhuri: Unaishi wapi?

Shahidi: Mbweni, Mbezi Beach

Wakili wa Jamhuri: Unafanya kazi gani?

Shahidi: Sasa hivi ni Mkurugenzi wa mahusiano wa benki ya crdb
Wakili wa Jamhuri: Hiyo inaitwaje kwa lugha ya kiingereza?

Shahidi: Director of Corporate Affairs

Wakili wa Jamhuri: Nimesikia umesema sasa hivi, kwani before hapo ulikuwa unafanya kazi gani?

Shahidi: Nilikuwa Director of marketing, research and customer services

Wakili wa Jamhuri: Hauwezi ukumbuka ilikuwa lini mpaka lini, kupata hiyo title, au ilikoma lini hiyo title

Shahidi: Ilikoma mwaka mmoja uliopita baada ya changes za kupata new management

Wakili wa Jamhuri: Tusaidie kituo chako cha kazi kilikuwa wapi?

Shahidi: Makao Makuu ambayo sasa sasa hivi yako Azikiwe, Azikiwe stree

Wakili wa Jamhuri: Umetumia neno ‘sasa yako Azikiwe’ kwani sasa hivi yako hapo

Shahidi: Tunategemea kuhama, kuhamia kwenye jengo letu jipya so..

Wakili wa Jamhuri: Sio kwamba before hamkuwa hapo?

Shahidi: No! Tulikuwa hapo

Wakili wa Jamhuri: Katika kazi yako, mimi interested na ile kazi yako ya mwanzo ambayo umetuambia ni Director of marketing, research na customer services niko sawasawa?

Shahidi: Ndio

Wakili wa Jamhuri: Hebu tuambie moja ya majukumu, Majukumu yako yalikuwa ni nini kama mkurugenzi

Shahidi: Moja ya majukumu yangu ilikuwa ni kuprotect brand ya bank, meaning ku-manage all the... kusimamia kila kitu ambacho bank inazungumziwa nje na kuhakikisha bank inakuwa na image nzuri kule nje, ni total brand management into it

Wakili wa Jamhuri: As a director, +nini jukumu lako, responsibilities as a director+

Shahidi: Labda nielezee nnaposema total brand management end to end, ni pamoja na kuangalia jinsi bank inavyokuwa perceived inapotokea media tofauti tofauti, na kuripoti kwenye TIS ambyo baada ya kuripoti inanipa guidance ya next step za kuchukua. Kwa hiyo kito chochote kinachotokea ndani ya bank, whether positive or negative, tunakiripoti na hizi comittee ni sheria ya Benki kuu ambayo inatu-guide kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tuna-complete goals

Wakili wa Jamhuri: Hebu tukumbushe, napenda niendelea kukuita miss Tully, bi Tully, tukumbushe Bi Tully hii, kuhusiana na shauri hili ambalo leo liko mbele ya mahakama, unaweza kukumbuka Tarehe 18 mwezi wa kwanza mwaka 2016, wewe ulikuwa wapi na nini kilitokea kuhusu shughuli

Shahidi: Aahh! Mmmh! Ninachokumbuka tarehe 18 mwezi wa kwanza nililetewa ripoti na afisa wangu wanaohusika na ku-manage social media. Kwamba bank tumeandikwa mle ndani na kilichoandikwa ni negative, tukapresent kwenye riski comittee na tunachotakiwa kufanya baada ya kupresent kwenye risk committee, ni ku-adhere to ile directive ambayo inatoka ambapo tuliambiwa turipoti polisi

Wakili wa Jamhuri: Unatuambia uliletewa taarifa na afisa wako wa Social media kuripotiwa bank negatively as you said, tuambie social media hii ilikuwa ipi?

Shahidi: JamiiForums

Wakili wa Jamhuri: Na unaweza kumkumbuka hao watu wa JamiiForums waliripoti kitu gani, ambacho kama bank au nyie kama bank mliona kitu kama negative?

Hakimu: Hiyo haihusiani na mwenendo wa shauri, umesema ulipewa taarifa na afisa wako

Wakili wa Jamhuri: Unaweza kumkumbuka afisa aliyekuletea hiyo taarifa anaitwa nani?

Shahidi: Anaitwa Willy Kamwele ambaye sasa hivi amehamishiwa Dodoma, na ile ilikuwa ni jukumu lake yake ni majukumu ya kazi, kwa hiyo yeye alikuwa ana-compile, ndio alikuwa ana-manage that section, kwa hiyo yeye kazi yake ni ku-compile, unfortunately nafikiri pia kwenye organization nyingi kuna hierarchy, kwo information zinaletwa mpaka zinafika kwangu nasaini

Wakili wa Jamhuri: Bwana Wile aliyekuletea taarifa, alikuwa na majukumu gani?
Shahidi: Jukumu lake lilikuwa public relations senior officer, ambaye kazi yake ndio ilikuwa hiyo ku-manage all the social media

Wakili wa Jamhuri: Baada ya bwana Wile kukuletea, I mean baada ya kwamba bwana Wile amekuletea hiyo taarifa, unasema ilikuwa negative..unakumbuka hiyo taarifa iliongelea kitu gani

Shahidi: Nakumbuka kuna mambo matano, Moja ilikuwa kwamba Bank ya CRDB inashirikiana na TPA na TRA kuikosesha Serikali mapato, ya pili ilikuwa ni ishu ya TFF ile get for ... ya tatu ilikuwa mabasi ya wanafunzi. Ya nne ilikuwa uanzishwaji wa benki ya crdb Burundi ni wa hasara, Benki ya crdb inashirikiana na majambazi kuwaibia wateja

Wakili wa Jamhuri: Sasa umetuambia, kuwa wewe ulikuwa ni director wa marketing, research na customers services, tunataka utuambie tuhuma hizi zilikuwa na ukweli wowote

Shahidi: Hapana

Wakili wa Jamhuri: Na desturi ya position yako, wewe baada ya kupata taarifa, au kuziona habari hizi ambazo ziko published na jamiiforums, ulichukua hatua gani?

Shahidi: Kama nilivyoelezea mwanzo kwamba kuna requirements kabisa ambazo zimekuwa set na bank, unajua sisi tuko regulated na benki kuu especialy kuhakikisha kwamba bank zinabaki stable na tuna-build trust to the customers kwa hiyo linapotokea kama hivyo kwenye risk management, tuna kitu tunaita operational risk kwa hiyo tunatakiwa kuripoti kwenye operational risk kwenye risk committee kwa hiyo risk Committee inakupa guidance, guidance iliyotolewa ni kwamba tulipoti polisi, kwa kuwa BoT wanapokuja kufanyia auditing wanatakiwa kujua ni action gani imefanyika, tuliporipoti polisi sisi tulikuwa tumemaliza. Kilichofuatia baada ya hapo kwa kweli sifahamu

Wakili wa Jamhuri: Hebu tuambie siku ile Wile anakuja kwako, nikurudishe nyuma kidogo, unaweza kukumbuka kwamba taarifa hiyo yeye ali-access kwa kutumia chombo kipi?

Shahidi: Wanaponiletea ripoti huwa nauliziaga links kwa hiyo huwa wanatuma links kwenye simu, ila sikuangalia ni kitu gani na kuangalia gravity ya ishu yenyewe, as I have said kila kitu mbacho kinaandikwa lazima ukirekodi, kwa hiyo walinitumia links kwenye simu yangu, nikakamilisha ripoti na kuattach ile ripoti to the committee

Wakili wa Jamhuri: Kwa hiyo ulitumia kitu gani kuzi-access hizo links

Shahidi: Kuzisoma?

Wakili wa Jamhuri: Ndio kuzisoma

Shahidi: Nilitumia simu ya mkononi

Peter Kibatala Wakili Upande wa Utetezi, anamuuliza Maswali Shahidi aliyeletwa na Jamhuri.

Kibatala: Kwanza ni sahihi kwamba, originally ambaye aliyeziona hizo posts, links or whatever sio wewe ni mtu mwingine?

Shahidi: Mmh!

Kibatala: Na hizo posts au links leo kaka angu anakuuliza maswali, hakukuonyesha uzitambue yaani kwamba zile ambazo niliziona nimeletewa na huyo uliyemtaja, hajakuonyesha wakili uzitambue hapa mahakamani

Shahidi: Hapana hajanionyesha

Kibatala: Simu pia, ulisema kwamba uliiangalia hizo links/posts kwa kupitia simu yako ya mkononi, hiyo simu haujademostrate chochote kuhusu vile namna ulivyofanya ili kuzifikia hizo linkis ili na sisi tuweze ku-cross check? Haujafanya lolote si ndio

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wakati wakili anakuongoza alitaja tarehe fulani, sasa kwa taratibu zetu wewe sio shahidi, sasa wewe uniambie kumbukumbu zako, ulisema tarehe 18 January, ulisema tarehe 18 january mwaka gani au ulisema tu tarehe 18 January?

Shahidi: Nilisema tarehe 18 Januari

Kibatala: Hukutaja mwaka si ndio?

Kibatala: Ni sahihi pia kwamba kitu kilichoisukuma bank kwenda kuripoti, ilikuwa ni risk management yaani kuprotect the bank, the image of the bank. Protection of Image of the bank, inahusiana na profitability of the bank

Shahidi: Aah..!

Kibatala: Is it true kusema kwamba the more clean the image the more profitable is the bank?

Shahidi: If I put it Technically, Not neccessary, lakini what bank sells to customers ni trust kwa hiyo. It is not neccessary kwamba, inategemea pia mtu royalty yake anavyoitaka, kwa hiyo it is hard to say it is clear part that the image of the bank, lakini image inasaidia not only one bank but industry

Kibatala: Aaah! Mimi nazungumzia crdb, kwani unatoa ushahidi kuhusu industry nzima au kuhusu bank yenu

Shahidi: Kuhusu crdb bank

Kibatala: Hivi Tawi la CRDB Burundi bado linafanyakazi?

Shahidi: Ndio! Na burundi sio tawi ni full subsidiary na ina matawi manne chini yake

Kibatala: Unaongozwa kusema chochote kuhusu profitability ya hiyo Burundi subsidiary

Shahidi: Samahani sijaelewa swali

Kibatala: Nasema wakati kaka yangu wakili, anakuongoza alikuuliza chochote, kwa sababu moja wapo ya post ambazo uliziona au taarifa ambazo uliripoti kwenye risk Committee, ni kwamba crdb burundi subsidiary ilikuwa inatengeneza losses. Ndio nakuuliza, wakati kaka anakuongoza alikuambia useme chochote kuhusu crdb burundi subsidiary ku-make loss au profit?

Shahidi: Wakati ananiuliza leo asubuhi! Hapana

Kibatala: Amekuuliza ufafanue chochote au umezungumza chochote kuhusu ukweli ama uwongo wa collision kati ya crdb na TFF kuhusiana na .... au role yoyote ambayo either crdb as institution au afisa wa crdb ambaye anaweza kuiplay katika kuathiri mapato ya TFF game collection

Shahidi: Sijaulizwa hilo swali

Kibatala: Pia bila shaka haujasema chochote kuhusu ukweli au kutokuwa ukweli kwa crdb kushirikiana na majambazi, yaani haujasema kama taarifa hizi ni za ukweli au sio za ukweli. Haujasema chochote

Shahidi: Sijaulizwa hilo swali

Kibatala: Pia kuhusu mabasi

Shahidi: Nilichoulizwa nii..

Kibatala: Aaah, wewe nisikilize tu ninachokuuliza, alikuuliza chochote kuhusu mabasi ya wanafunzi au ulizungumzia chochote maana wewe ndio unatoka CRDB na inakuwa reported kwako ndio maana nakuuliza angekuja kaka Wile, nani Kamwela naye ningemuuliza lakini kwa kuwa wewe ndio taarifa imekuja kwako ndio maana nakuuliza

Shahidi: Asubuhi hii sikuulizwa

Kibatala: aliyekwenda kuripoti polisi ni wewe au ni mtu mwingine

Shahidi: Kisheria ni mimi ndio nilitakiwa kuripoti kwa hiyo niliripoti mimi

Kibatala: Kwa hiyo wakati unaongozwa ulimwambia muheshimiwa wakili kwamba ni mimi ndio niliyeripoti

Shahidi: Nafikiri nilielezea process...

Kibatala: Ah, sitaki process. Alikuuliza kwamba wewe ndio uliyeripoti au la

Shahidi: Hakuniuliza

Maswali mzunguko wa pili kutoka kwa Wakili wa Serikali.

Jamhuri: Dada Tully nitakuuliza mambo machache sana, nilisikia wakili alikuwa akikueleza kuhusu tarehe 18 January, amesema kwamba wewe haukusema mwaka. Hebu tuambie mwaka huo

Kibatala: Objection! Muheshimiwa hawezi kuuliza mwaka huo hivi sasa labda aulize ni kwa nini hakutaja mwaka

Wakili wa Jamhuri: Muheshimiwa na-rephrase swali langu!, unasema uliambiwa, unasema niliyokuwa nakuuliza tarehe ile, unaweza kukumbuka swali langu nilivyouliza

Shahidi: Uliuliza...

Wakiliwa Jamhuri: Specific katika siku ambayo katika siku ambayo..

Shahidi: Uliuliza tarehe 18 mwezi wa kwanza na mimi nika-respond

Wakili wa Jamhuri: Unakumbuka mimi niliuliza kuhusu mwaka

Kibatala: Objection Mheshimiwa

Hakimu: Uli-respond vipi? Kuhusiana na tarehe 18

Shahidi: Nili-respond kwamba tarehe 18 mwezi wa kwanza ndipo nilipopewa ile ripoti ambayo ndiyo tulitumia kuripoti kwenye risk committee na baadae kuripoti polisi

Wakili wa Jamhuri: Na wakili alikuuliza kuhusu kitu kilichokusukuma, au kitu kilichoisukuma benki kwenda kuripoti tukio hili na akakwambia kuhusu profit ya bank. Sasa hebu tusaidie kama bank itachafuliwa kama abavyo wewe umesema. Kama taarifa hizo ambazo zilikuwa negative, kama zingeachwa kwenda open, je faida ya bank ingebaki kuwa sawa

Hakimu: Swali liko wide sana, hebu rephrase

Wakili wa Jamhuri: Umeulizwa kuhusu profitability ya bank baada ya bank kuwa imechafuliwa si ndio?
Shahidi: Ndio

Hakimu: Amesema ni procedures za BoT

Wakili wa Jamhuri: Kama bank imechafuliwa ni ile profitability...

Hakimu: Sasa wewe una-conclude kwamba bank imechafuliwa, lakini hicho ni kitu, labda itakuwa ishu ya ku-decide, alimuuliza kwamba baada ya hizo posts zinaweza kuwa zimesababisha profit au loss?

Wakili wa Jamhuri: Hebu tuambie kuhusiana na hizo posts ambazo kulingana na wewe umesema zimechafuliwa, kwa posts hizo ambazo ni negative

Kibatala: Mheshimiwa hakusema bank imechafuliwa

Wakili wa Jamhuri:
Ni post negative right!

Kibatala: Hata negative hakusema, mwenyewe yupo hapa

Hakimu: Alisema ni kutokana na BoT kwa hiyo ali-comply na BoT

Wakili wa Jamhuri: Hebu tuambie, hivi suala hilo lingeachwa likaenda wazi, kwa uzoefu wako will the profit remain the same

Shahidi: Muheshimiwa suala hilo nimekaa kimya kwa sababu hilo swala ni probability na sijui kisheria probability inakaaje. It is yes and No, inadepend na gravity

Hakimu: Labda mimi niseme, did you note any negative baada ya hizo post?

Shahidi: No!

Wakili wa Jamhuri: Umetueleza kuhusu branchi ya Burundi ambayo umetueleza sio Branch ni subsidiary, tawi hili la Burundi limeendeshwa kwa hasara au

Kibatala: Objection, swali niliuliza hivi, uliongozwa kusema chochote kusema kuhusu profitability au loss banking ya CRDB

Wakili wa Jamhuri: Your honor to save the court time, maybe let me rephrase my question, kwa nini hamjafunga tawi la Burundi, nilisikia umeulizwa kama mmefunga au bado mnaoparate

Hakimu: Nafikiri hilo swali liliulizwa na alijibu nilipouliza kama alinote any negative

Wakili wa Jamhuri: Nasikia umeulizwa kuhusu habari ya mabasi ya CRDB, ambayo moja kati ya vitu ambavyo nyie au wewe, au moja kati ya kitu ambacho kiliwapeleka nyie kuripoti hii kitu. Wakili aliuliza kama niliuliza kuhusu ukweli wa hii kitu. Hebu ikumbushe mahakama sasa, nilipokuuliza kuhusu ukweli wa taarifa ilizokuwa zimeripotiwa na JamiiForums

Shahidi: Ishu ya mabasi ya wanafunzi

Wakili wa Jamhuri: In general nilipokuuliza kuhusu ukweli wa hizo taarifa

Shahidi: Kulikuwa na misinformation

Wakili wa Jamhuri: Nijibu tu kile ulichokisema nilipokuuliza kama taarifa hizi zilikuwa na ukweli au hazikuwa na ukweli
Shahidi: Hazikuwa na, I don’t know how you say misinformation kwa kiswahili, sijui kama naruhisiwa kuelezea kwa sababu

Hakimu: Charge inasemaje?

Wakili wa Jamhuri: Ni kusajili kikoa, na kuzuia uchunguzi

Wakili wa Jamhuri: Kwa hiyo niambie nilipokuuliza kuhusu hizo taarifa kwamba zilikuwa na ukweli au hazikuwa na ukweli?

Shahidi: Nilisema hapana, sijui labda ni-clarify kwamba niliposema hapana kwamba bank ya CRDB kama part ya social responsibility tulinunua magari matano ili kuwasafirisha wanafunzi wa Dar es Salaam na kuwapa UDA. Baada ya UDA kuwa privatised, UDA wakasema hawawezi kufanya..

Kibatala: Where are we heading? I mean this road leads you, maana sasa tunapoelekea tutaulizana kuhusu hayo mabasi

Wakili wa Jamhuri: Swali langu la msingi, muheshimiwa ni alipoulizwa kuhusiana na ukweli kuhusu mabasi haya. Sasa mimi ninamuuliza, generality nilivyomuuliza kuhusu ukweli wa maswala haya yaliyoandikwa na jamiiforums

Hakimu: Kumbuka I don’t mean kwamba unaweza ukaruhusiwa

Wakili wa Jamhuri: Muheshimiwa ni hayo

Hakimu: Kuna Shahidi mwingine?

Wakili wa Jamhuri: Hapana, tunafunga Ushahidi.

Hakimu kesi inaahirishwa. Tarehe ya Utetezi ni tarehe 20 Agosti 2020. Dhamana kwa Washitakiwa inaendelea...
 
WanaJF wenzangu.

Haitoshi tu kufuatilia hii kesi humu pekee, tujitahidi tulio karibu kufika mahakamani kumpa moyo ndugu yetu Maxence na staff wenzake.

Mungu atajibu maombi yetu na tuonyeshe kumuunga mkono Maxence kivitendo.
 
Hata ikiwezekana tutoa na mchango apate hela ta mafuta ya kwenda mahakamani
 
Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums na Mwanahisa wa Jamii Media) inatajwa tena leo, Julai 30, 2020 majira ya saa 3 asubuhi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar

Mara ya mwisho iliposikilizwa Juni 25, 2020 Jamhuri iliiomba Mahakama iruhusu kukamatwa kwa Shahidi Tully E. Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma (CRDB) kufuatia kesi hiyo kuahirishwa kwa takriban mara 9

Katika shtaka la kwanza, Mkurugenzi wa Jamii Forums anatuhumiwa kuendesha mtandao (JamiiForums.com) ambao haujasajiliwa Tanzania na vile vile hautumii Kikoa cha do-TZ

Katika shtaka la pili la Shauri hili, Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa Jamii Forums kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums.com waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea katika Benki ya CRDB

Taarifa zilizotakiwa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Pia ilitakiwa zitolewe post zote zinazohusu Uhalifu unaofanyika CRDB kitu ambacho Polisi wanadai Mkurugenzi huyo aligoma kuwapa

Taarifa zilizotakiwa ni za Wanachama walioanzisha mijadala inayosomeka "Charles Kimei (CRDB) jiuzulu, kashfa ya kontena, tiketi TFF, wanafunzi na ujambazi CRDB" mjadala unaodaiwa kuanzishwa tarehe 18 Januari 2016 pamoja na "Wizi wa Banki ya CRDB - Part II" unaodaiwa kuanzishwa Machi 11, 2015.

Soma namna Mahakama ilivyoridhia ombi la Jamhuri la Shahidi kukamatwa: ‪Kesi namba 458 dhidi ya JamiiForums: Jamhuri yaomba Hati ya kukamatwa Shahidi, Mahakama yaridhia!‬

Shauri hili ni mojawapo ya mashuri matatu yaliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya JamiiForums. Kufahamu mashauri mengine ambayo tayari yamemalizika, soma Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums

- UPDATES -
View attachment 1522348
Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums na Mwanahisa wa Jamii Media) imetajwa tena leo, Julai 30, 2020 majira ya saa 3 asubuhi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar

Mara ya mwisho iliposikilizwa Juni 25, 2020 Jamhuri iliiomba Mahakama iruhusu kukamatwa kwa Shahidi Tully E. Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma (CRDB) kufuatia kesi hiyo kuahirishwa kwa takriban mara 9

Baada ya kusubiriwa kwa zaidi ya mwaka aje kutoa Ushahidi, leo Shahidi Tully Esther Mwambapa, amefika Mahakamani Kutoa Ushahidi. Ameanza kuulizwa Maswali na Wakili wa Jamhuri Faraja Nguka

Wakili wa Jamhuri: Tukumbushe umetuambia unaitwa nani?
Shahidi: Tully Esther Mwambapa
Wakili wa Jamhuri: Unaishi wapi?
Shahidi: Mbweni, Mbezi Beach
Wakili wa Jamhuri: Unafanya kazi gani?
Shahidi: Sasa hivi ni Mkurugenzi wa mahusiano wa benki ya crdb
Wakili wa Jamhuri: Hiyo inaitwaje kwa lugha ya kiingereza?

Shahidi: Director of corporate affairs
Wakili wa Jamhuri: Nimesikia umesema sasa hivi, kwani before hapo ulikuwa unafanya kazi gani?

Shahidi: Nilikuwa Director of marketing, research and customer services
Wakili wa Jamhuri: Hauwezi ukumbuka ilikuwa lini mpaka lini, kupata hiyo title, au ilikoma lini hiyo title

Shahidi: Ilikoma mwaka mmoja uliopita baada ya changes za kupata new management

Wakili wa Jamhuri: Tusaidie kituo chako cha kazi kilikuwa wapi?

Shahidi: Makao Makuu ambayo sasa sasa hivi yako Azikiwe, Azikiwe stree

Wakili wa Jamhuri: Umetumia neno ‘sasa yako Azikiwe’ kwani sasa hivi yako hapo
Shahidi: Tunategemea kuhama, kuhamia kwenye jengo letu jipya so..

Wakili wa Jamhuri: Sio kwamba before hamkuwa hapo?
Shahidi: No! Tulikuwa hapo

Wakili wa Jamhuri: Katika kazi yako, mimi interested na ile kazi yako ya mwanzo ambayo umetuambia ni Director of marketing, research na customer services niko sawasawa?
Shahidi: Ndio

Wakili wa Jamhuri: Hebu tuambie moja ya majukumu, Majukumu yako yalikuwa ni nini kama mkurugenzi

Shahidi: Moja ya majukumu yangu ilikuwa ni kuprotect brand ya bank, meaning ku-manage all the... kusimamia kila kitu ambacho bank inazungumziwa nje na kuhakikisha bank inakuwa na image nzuri kule nje, ni total brand management into it

Wakili wa Jamhuri: As a director, +nini jukumu lako, responsibilities as a director+
Shahidi: Labda nielezee nnaposema total brand management end to end, ni pamoja na kuangalia jinsi bank inavyokuwa perceived inapotokea media tofauti tofauti, na kuripoti kwenye TIS ambyo baada ya kuripoti inanipa guidance ya next step za kuchukua. Kwa hiyo kito chochote kinachotokea ndani ya bank, whether positive or negative, tunakiripoti na hizi comittee ni sheria ya Benki kuu ambayo inatu-guide kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tuna-complete goals

Wakili wa Jamhuri: Hebu tukumbushe, napenda niendelea kukuita miss Tully, bi Tully, tukumbushe Bi Tully hii, kuhusiana na shauri hili ambalo leo liko mbele ya mahakama, unaweza kukumbuka Tarehe 18 mwezi wa kwanza mwaka 2016, wewe ulikuwa wapi na nini kilitokea kuhusu shughuli

Shahidi: Aahh! Mmmh! Ninachokumbuka tarehe 18 mwezi wa kwanza nililetewa ripoti na afisa wangu wanaohusika na ku-manage social media. Kwamba bank tumeandikwa mle ndani na kilichoandikwa ni negative, tukapresent kwenye riski comittee na tunachotakiwa kufanya baada ya kupresent kwenye risk committee, ni ku-adhere to ile directive ambayo inatoka ambapo tuliambiwa turipoti polisi

Wakili wa Jamhuri: Unatuambia uliletewa taarifa na afisa wako wa Social media kuripotiwa bank negatively as you said, tuambie social media hii ilikuwa ipi?
Shahidi: JamiiForums

Wakili wa Jamhuri: Jamiiforums
Wakili wa Jamhuri: Na unaweza kumkumbuka hao watu wa JamiiForums waliripoti kitu gani, ambacho kama bank au nyie kama bank mliona kitu kama negative?

Hakimu: Hiyo haihusiani na mwenendo wa shauri, umesema ulipewa taarifa na afisa wako

Wakili wa Jamhuri: Unaweza kumkumbuka afisa aliyekuletea hiyo taarifa anaitwa nani?

Shahidi: Anaitwa Willy Kamwele ambaye sasa hivi amehamishiwa Dodoma, na ile ilikuwa ni jukumu lake yake ni majukumu ya kazi, kwa hiyo yeye alikuwa ana-compile, ndio alikuwa ana-manage that section, kwa hiyo yeye kazi yake ni ku-compile, unfortunately nafikiri pia kwenye organization nyingi kuna hierarchy, kwo information zinaletwa mpaka zinafika kwangu nasaini

Wakili wa Jamhuri: Bwana Wile aliyekuletea taarifa, alikuwa na majukumu gani?
Shahidi: Jukumu lake lilikuwa public relations senior officer, ambaye kazi yake ndio ilikuwa hiyo ku-manage all the social media

Wakili wa Jamhuri: Baada ya bwana Wile kukuletea, I mean baada ya kwamba bwana Wile amekuletea hiyo taarifa, unasema ilikuwa negative..unakumbuka hiyo taarifa iliongelea kitu gani
Shahidi: Nakumbuka kuna mambo matano, Moja ilikuwa kwamba Bank ya CRDB inashirikiana na TPA na TRA kuikosesha Serikali mapato, ya pili ilikuwa ni ishu ya TFF ile get for ... ya tatu ilikuwa mabasi ya wanafunzi. Ya nne ilikuwa uanzishwaji wa benki ya crdb Burundi ni wa hasara, Benki ya crdb inashirikiana na majambazi kuwaibia wateja

Wakili wa Jamhuri: Sasa umetuambia, kuwa wewe ulikuwa ni director wa marketing, research na customers services, tunataka utuambie tuhuma hizi zilikuwa na ukweli wowote
Shahidi: Hapana

Wakili wa Jamhuri: Na desturi ya position yako, wewe baada ya kupata taarifa, au kuziona habari hizi ambazo ziko published na jamiiforums, ulichukua hatua gani?
Shahidi: Kama nilivyoelezea mwanzo kwamba kuna requirements kabisa ambazo zimekuwa set na bank, unajua sisi tuko regulated na benki kuu especialy kuhakikisha kwamba bank zinabaki stable na, hatu- tunabuild trust to the customers kwa hiyo linapotokea kama hivyo kwenye risk management, tuna kitu tunaita operational risk kwa hiyo tunatakiwa kuripoti kwenye operational risk kwenye risk committee kwa hiyo risk Committee inakupa guidance, guidance iliyotolewa ni kwamba tulipoti polisi, kwa kuwa BoT wanapokuja kufanyia auditing wanatakiwa kujua ni action gani imefanyika, tuliporipoti polisi sisi tulikuwa tumemaliza. Kilichofuatia baada ya hapo kwa kweli sifahamu

Wakili wa Jamhuri: Hebu tuambie siku ile Wile anakuja kwako, nikurudishe nyuma kidogo, unaweza kukumbuka kwamba taarifa hiyo yeye ali-access kwa kutumia chombo kipi?
Shahidi: wanaponiletea ripoti huwa nauliziaga links kwa hiyo huwa wanatuma links kwenye simu, ila sikuangalia ni kitu gani na kuangalia gravity ya ishu yenyewe, as I have said kila kitu mbacho kinaandikwa lazima ukirekodi, kwa hiyo walinitumia links kwenye simu yangu, nikakamilisha ripoti na kuattach ile ripoti to the committee

Wakili wa Jamhuri: Kwa hiyo ulitumia kitu gani kuzi-access hizo links
Shahidi: Kuzisoma:

Wakili wa Jamhuri: ndio kuzisoma?
Shahidi: Nilitumia simu ya mkononi

Peter Kibatala Wakili Upande wa Utetezi, anamuuliza Maswali Shahidi aliyeletwa na Jamhuri.

Kibatala: Kwanza ni sahihi kwamba, originally ambaye aliyeziona hizo posts, links or whatever sio wewe ni mtu mwingine?
Shahidi: Mmh!

Kibatala: Na hizo posts au links leo kaka angu anakuuliza maswali, hakukuonyesha uzitambue yaani kwamba zile ambazo niliziona nimeletewa na huyo uliyemtaja, hajakuonyesha wakili uzitambue hapa mahakamani
Shahidi: hapana hajanionyesha

Kibatala: Simu pia, ulisema kwamba uliiangalia hizo links/posts kwa kupitia simu yako ya mkononi, hiyo simu haujademostrate chochote kuhusu vile namna ulivyofanya ili kuzifikia hizo linkis ili na sisi tuweze ku-cross check? Haujafanya lolote si ndio
Shahidi: Hapana

Kibatala: Wakati wakili anakuongoza alitaja tarehe fulani, sasa kwa taratibu zetu wewe sio shahidi, sasa wewe uniambie kumbukumbu zako, ulisema tarehe 18 January, ulisema tarehe 18 january mwaka gani au ulisema tu tarehe 18 January?
Shahidi: Nilisema tarehe 18 Januari

Kibatala: Hukutaja mwaka si ndio?
Kibatala: Ni sahihi pia kwamba kitu kilichoisukuma bank kwenda kuripoti, ilikuwa ni risk management yaani kuprotect the bank, the image of the bank. Protection of Image of the bank, inahusiana na profitability of the bank
Shahidi: Aah..!

Kibatala: Is it true kusema kwamba the more clean the image the more profitable is the bank?
Shahidi: If I put it Technically, Not neccessary, lakini what bank sells to customers ni trust kwa hiyo. It is not neccessary kwamba, inategemea pia mtu royalty yake anavyoitaka, kwa hiyo it is hard to say it is clear part that the image of the bank, lakini image inasaidia not only one bank but industry

Kibatala: Aaah! Mimi nazungumzia crdb, kwani unatoa ushahidi kuhusu industry nzima au kuhusu bank yenu
Shahidi: Kuhusu crdb bank

Kibatala: Hivi Tawi la CRDB Burundi bado linafanyakazi?

Shahidi: Ndio! Na burundi sio tawi ni full subsidiary na ina matawi manne chini yake

Kibatala: Unaongozwa kusema chochote kuhusu profitability ya hiyo Burundi subsidiary
Shahidi: Samahani sijaelewa swali

Kibatala: Nasema wakati kaka yangu wakili, anakuongoza alikuuliza chochote, kwa sababu moja wapo ya post ambazo uliziona au taarifa ambazo uliripoti kwenye risk Committee, ni kwamba crdb burundi subsidiary ilikuwa inatengeneza losses. Ndio nakuuliza, wakati kaka anakuongoza alikuambia useme chochote kuhusu crdb burundi subsidiary ku-make loss au profit?
Shahidi: wakati ananiuliza leo asubuhi! Hapana

Kibatala: Amekuuliza ufafanue chochote au umezungumza chochote kuhusu ukweli ama uwongo wa collision kati ya crdb na TFF kuhusiana na .... au role yoyote ambayo either crdb as institution au afisa wa crdb ambaye anaweza kuiplay katika kuathiri mapato ya TFF game collection
Shahidi: Sijaulizwa hilo swali

Kibatala: Pia bila shaka haujasema chochote kuhusu ukweli au kutokuwa ukweli kwa crdb kushirikiana na majambazi, yaani haujasema kama taarifa hizi ni za ukweli au sio za ukweli. Haujasema chochote
Shahidi: Sijaulizwa hilo swali

Kibatala: Pia kuhusu mabasi
Shahidi: Nilichoulizwa nii..

Kibatala: Aaa wewe nisikilize tu ninachokuuliza, alikuuliza chochote kuhusu mabasi ya wanafunzi au ulizungumzia chochote maana wewe ndio unatoka crdb na inakuwa reported kwako ndio maana nakuuliza angekuja kaka Wile, nani Kamwela naye ningemuuliza lakini kwa kuwa wewe ndio taarifa imekuja kwako ndio maana nakuuliza
Shahidi: Asubuhi hii sikuulizwa

Kibatala: aliyekwenda kuripoti polisi ni wewe au ni mtu mwingine
Shahidi: Kisheria ni mimi ndio nilitakiwa kuripoti kwa hiyo niliripoti mimi

Kibatala: Kwa hiyo wakati unaongozwa ulimwambia muheshimiwa wakili kwamba ni mimi ndio niliyeripoti
Shahidi: Nafikiri nilielezea process...

Kibatala: Ah, sitaki process. Alikuuliza kwamba wewe ndio uliyeripoti au la
Shahidi: Hakuniuliza

Maswali mzunguko wa pili kutoka kwa Wakili wa Serikali.

Jamhuri: Dada Tully nitakuuliza mambo machache sana, nilisikia wakili alikuwa akikueleza kuhusu tarehe 18 January, amesema kwamba wewe haukusema mwaka. Hebu tuambie mwaka huo
Kibatala: Objection! Muheshimiwa hawezi kuuliza mwaka huo hivi sasa labda aulize ni kwa nini hakutaja mwaka

Wakili wa Jamhuri: Muheshimiwa na-rephrase swali langu!, unasema uliambiwa, unasema niliyokuwa nakuuliza tarehe ile, unaweza kukumbuka swali langu nilivyouliza
Shahidi: Uliuliza...

Wakiliwa Jamhuri: Specific katika siku ambayo katika siku ambayo..
Shahidi: Uliuliza tarehe 18 mwezi wa kwanza na mimi nika-respond

Wakili wa Jamhuri: Unakumbuka mimi niliuliza kuhusu mwaka
Kibatala: Objection Mheshimiwa
Hakimu: Uli-respond vipi? Kuhusiana na tarehe 18
Shahidi: Nili-respond kwamba tarehe 18 mwezi wa kwanza ndipo nilipopewa ile ripoti ambayo ndiyo tulitumia kuripoti kwenye risk committee na baadae kuripoti polisi

Wakili wa Jamhuri: Na wakili alikuuliza kuhusu kitu kilichokusukuma, au kitu kilichoisukuma benki kwenda kuripoti tukio hili na akakwambia kuhusu profit ya bank. Sasa hebu tusaidie kama bank itachafuliwa kama abavyo wewe umesema. Kama taarifa hizo ambazo zilikuwa negative, kama zingeachwa kwenda open, je faida ya bank ingebaki kuwa sawa
Hakimu: Swali liko wide sana, hebu rephrase

Wakili wa Jamhuri: Umeulizwa kuhusu profitability ya bank baada ya bank kuwa imechafuliwa si ndio?
Shahidi: Ndio

Hakimu: Amesema ni procedures za BoT
Wakili wa Jamhuri: Kama bank imechafuliwa ni ile profitability..
Hakimu: Sasa wewe una-conclude kwamba bank imechafuliwa, lakini hicho ni kitu, labda itakuwa ishu ya ku-decide, alimuuliza kwamba baada ya hizo posts zinaweza kuwa zimesababisha profit au loss?

Wakili wa Jamhuri: Hebu tuambie kuhusiana na hizo posts ambazo kulingana na wewe umesema zimechafuliwa, kwa posts hizo ambazo ni negative
Kibatala: Mheshimiwa hakusema bank imechafuliwa

Wakili wa Jamhuri: Ni post negative right!
Kibatala: Hata negative hakusema, mwenyewe yupo hapa

Hakimu: alisema ni kutokana na BoT kwa hiyo ali-comply na BoT

Wakili wa Jamhuri: Hebu tuambie, hivi suala hilo lingeachwa likaenda wazi, kwa uzoefu wako will the profit remain the same
Shahidi: Muheshimiwa suala hilo nimekaa kimya kwa sababu hilo swala ni probability na sijui kisheria probability inakaaje. It is yes and No, inadepend na gravity

Hakimu: Labda mimi niseme, did you note any negative baada ya hizo post?
Shahidi: No!

Wakili wa Jamhuri: Umetueleza kuhusu branchi ya Burundi ambayo umetueleza sio Branch ni subsidiary, tawi hili la Burundi limeendeshwa kwa hasara au
Kibatala: Objection, swali niliuliza hivi, uliongozwa kusema chochote kusema kuhusu profitability au loss banking ya CRDB

Wakili wa Jamhuri: Your honor to save the court time, maybe let me rephrase my question, kwa nini hamjafunga tawi la Burundi, nilisikia umeulizwa kama mmefunga au bado mnaoparate

Hakimu: Nafikiri hilo swali liliulizwa na alijibu nilipouliza kama alinote any negative

Wakili wa Jamhuri: Nasikia umeulizwa kuhusu habari ya mabasi ya CRDB, ambayo moja kati ya vitu ambavyo nyie au wewe, au moja kati ya kitu ambacho kiliwapeleka nyie kuripoti hii kitu. Wakili aliuliza kama niliuliza kuhusu ukweli wa hii kitu. Hebu ikumbushe mahakama sasa, nilipokuuliza kuhusu ukweli wa taarifa ilizokuwa zimeripotiwa na Jamiiforums
Shahidi: Ishu ya mabasi ya wanafunzi

Wakili wa Jamhuri: In general nilipokuuliza kuhusu ukweli wa hizo taarifa
Shahidi: Kulikuwa na misinformation

Wakili wa Jamhuri: Nijibu tu kile ulichokisema nilipokuuliza kama taarifa hizi zilikuwa na ukweli au hazikuwa na ukweli
Shahidi: Hazikuwa na, I don’t know how you say misinformation kwa kiswahili, sijui kama naruhisiwa kuelezea kwa sababu

Hakimu: Charge inasemaje?

Wakili wa Jamhuri: ni kusajili kikoa, na kuzuia investigation

Wakili wa Jamhuri: kwa hiyo niambie nilipokuuliza kuhusu hizo taarifa kwamba zilikuwa na ukweli au hazikuwa na ukweli?

Shahidi: Nilisema hapana, sijui labda ni-clarify kwamba niliposema hapana kwamba bank ya CRDB kama part ya social responsibility tulinunua magari matano ili kuwasafirisha wanafunzi wa Dar es Salaam na kuwapa UDA. Baada ya UDA kuwa privatised, UDA wakasema hawawezi kufanya..

Kibatala: Where are we landing, I mean this road leads you, maana sasa tunapoelekea tutaulizana kuhusu hayo mabasi

Wakili wa Jamhuri: Swali langu la msingi, muheshimiwa ni alipoulizwa kuhusiana na ukweli kuhusu mabasi haya. Sasa mimi ninamuuliza, generality nilivyomuuliza kuhusu ukweli wa maswala haya yaliyoandikwa na jamiiforums

Hakimu: Kumbuka I don’t mean kwamba unaweza ukaruhusiwa

Wakili wa Jamhuri: Muheshimiwa ni hayo

Hakimu: Kuna Shahidi mwingine?

Wakili wa Jamhuri: Hapana Tunafunga Ushahidi.

Hakimu kesi inaahirishwa. Tarehe ya Utetezi ni tarehe 20 Agosti 2020.Dhamana kwa Washitakiwa inaendelea
Mungu atende kwa Neema.

JF ni mahala sahihhi kwa wanaoikubali na wanaoichukia.

Ushindi kwa JF
 
Back
Top Bottom