SoC01 Kesho ya vijana wa sasa na kutoweka kwa daraja la kipato cha kati

Stories of Change - 2021 Competition

MtCHb

New Member
Sep 24, 2021
4
7
UTANGULIZI:

Hakutakua na daraja la kati, aminini nakuambieni,

Kesho yetu vijana wa sasa itakua ni ya madaraja mawili; aidha utakua maskini ama utakua tajiri.

Hakutakua na daraja la kati. Katika hizo zama zetu zinazokuja. Kwenye hii makala tutazisoma kwa pamoja nyakati, nakuona ni kwa namna gani hili daraja la kipato cha kati linaenda kufariki.

Je utaangukia kwenye daraja lipi?

Je kwa sasa upo daraja lipi kati ya haya madaraja matatu tuliyonayo?


MTAZAMO WANGU JUU YA MADARAJA MATATU TULIYONAYO.

I. DARAJA LA MASKINI;

Kwa kutumia muktadha wa jamii za kitanzania, nimekua nikishuhudia daraja la watu maskini, likisimama kama daraja lenye matarajio makubwa kutoka kwa serikali. Wana matumaini na serikali yao kwamba ikiwa bora itawarahisishia maisha yao, na itawaletea maendeleo mpaka kwenye mifuko yao.

Daraja hili la maskini mara nyingi linatumiwa na wanasiasa kwa manufaa yao binafsi ya kisiasa na kujipatia madaraka.

Ni tabaka ambalo hupenda kuhakikishiwa huduma za kijamii na kwa free of charge yani,BURE.

Tabaka hili likiwa na uhakika wa huduma za kijamii, huduma za afya , chakula na watoto wakasomeshewa bure na serikali basi kwao inakua poa, wanaridhika kabisa.

Hili ndo tabaka linaloongoza kwa kuisifia serikali, pia ni tabaka linaloongoza kwa kuiponda serikali— kutokana na namna itakavyokua imewagusa.

Ni tabaka linaloongoza kwa kujadili siasa. Kwa sababu ni tabaka linaloamini serikali ndo ina dhamana ya maisha yao.


II. DARAJA LA KATI

Hili ni daraja ambalo msingi wake ulijengwa namna hii;

Soma kwa bidii,
Tafuta kazi,
Fanya kazi kwa bidii,
Ishi kwa kujibana huku ukiweka akiba ya pesa,
wekeza&fungua biashara ama njia mbadala ya kipato ILI UKISTAAFU USIJE ADHIRIKA.

Msingi wa uwekezaji wa hili daraja ni kuwekeza ili usiipoteze level ya maisha uliyoifikia, SIO kuwekeza hili kushinda na kujipatia uhuru wa kiuchumi.

Wanajihami sana yaani wanawekeza sehemu ambazo wanahisi ni salama.


III. DARAJA LA MATAJIRI

Wanawekeza ili kushinda, yaani kupata "higher returns" kwenye investment zao.
Ni kundi la watu wanaowekeza ili 'kujikwamua' kiuchumi, na sio tuu kuishia kulinda walichonacho. Ni watu wanaoangalia uhuru wa kiuchumi na utajiri wa vizazi, na-vizazi-vyao vijavyo "generational wealthy"


KWANINI DARAJA LA KIPATO CHA KATI LINATOWEKA.

1.INSECURITY; Hutocheza pata-potea milele.

Daraja la kati ni daraja linalo-elea katikati ya daraja la matajiri na daraja la maskini, halina uhakika kama litaendelea ku-elea milele...na ndo maana linaishi kwa kujihami na kuchukua tahadhari sana.

Daraja hili linapambana sana ili kumudu gharama za elimu, afya na makazi.

Nimetumia neno "pambana" ili kulitofautisha daraja hili na daraja la maskini......

Wanasomesha watoto vyuoni ama shule za binafsi "private" lakini hivyo hivyo kwa kupambana kuisaka ada.

Wamepanga/Wanamiliki nyumba nzuri ya kuishi—(mfano; vyumba vitatu, jiko, sebure, vyoo vya ku-Flush, rangi ya kupendeza, tiles, gypsum, uzio na geti fulani hivi)
Usafiri pia unaweza kuwepo.

Akiwa mtumishi wa kuajiriwa; mara nyingi anakua na mkopo benki, anapokea mshahara unaokatwa na kubaki mdogo, anaishi kwa kujibana ili aweze kuAfford gharama za maisha na familia.

Akiwa amejiajiri; mara nyingi anakua anadili na marejesho ya benki.

Wote hawana uhakika wa kuendelea Ku maintain hayo maisha kesho. Wote wanajiuliza wakifariki leo familia zao nani ataziSupport "they are not secured"

Akiteleza kidogo tuu "In a blink of an eye" anadondokea kwenye daraja la umaskini.


2. KUSHUKA KWA THAMANI YA FEDHA NI JAMBO ENDELEVU.

Asilimia kubwa ya watu wa daraja la kati ni waajiriwa;
Fanya mahesabu kulinganisha ongezeko la mshahara kwa cheo fulani na thamani ya fedha kwa muda husika; jaribu kulinganisha na miaka mitano nyuma, jaribu tena kwa miaka kumi nyuma (tumia dollar kuthaminisha)
Afu utaona kadri muda unavyoenda ndivyo cheo chako kinavyozidi kupungua thamani yaani kiuhalisia mshahara wako unazidi kupungua, japo kiasi kinaongezeka.

Kila siku kipato chako kinapungua, mdogo mdogo unashuka daraja la chini.


3. TEKNOLOJIA NA USHINDANI WA KIMATAIFA.

Tunaelekea dunia ya "automation" teknolojia inaenda kuua kazi nyingi za watu wa daraja la kati

io italazimisha watu wa daraja la kati ku shift..wapo watakaopanda daraja la matajiri, pia wapo watakaoshuka daraja la maskini.

Nini kitawatofautisha?

(UJUZI)

Ujuzi 'skills' utakua na uzito zaidi ya vyeti.

Watu wa kipato cha kati wenye ujuzi mkubwa "highly skilled" hawa watapanda mpaka daraja la matajiri 'rich class'

Watu wa kipato cha kati wenye ujuzi wa kawaida (usiowatofautisha na wenzao) "average skilled" hawa watakua 'replaced' watashuka kwenye daraja la maskini "poor class"

Hapa hapa kwenye teknolojia...

Teknolojia itarahisisha "exportation of jobs"

Hii inaweza punguza kazi kwa watu wa middle class...sasa hivi tunashuhudia wakandarasi pekee ndo wakilalamika baadhi ya kazi ambazo wangeweza kuzifanya wanapewa wakandarasi wa nje hasa wachina.

Hii itahamia ata kwa shughuli ndogo ndogo za kijasiriamali; mfano nahitaji ramani ya nyumba naweza zama inbox ya designer/mchoraji/architect wa nje ya nchi kupitia website zao, emails ama mitandao ya kijamii afu tukafanya biashara.

Vivyo hivyo kwa apps and websites developers, naweza tengenezewa website yangu na mtu toka nje ya nchi. Yani kila kitu kitakua kinashindana na soko la dunia.

mfano, sasa hivi kuna watu wanapata kazi za freelancing kupitia mtandao wa "upwork". Watu wanaandika skills zao ukipitia profile zao, atakaekushawishi wewe kama ni mwajiri unampa kazi yako akufanyie bila kujali mtu huyo anatoka kona gani ya dunia.

Teknolojia ilitakiwa itusaidie kwa sababu wigo wa fursa unakua umeongezeka....lakini kwanini nahisi itaturudisha nyuma?

i. Ni kutokana na mwamko hafifu wa nchi juu ya teknolojia
Raia wanaamini fursa za kidijitali zitawakutanisha na utapeli tuu, yaani ni utapeli mtupu.

Mfano, Wafanyabiashara wa Tanzania hawana utamaduni ya kua na website, unakuta mtu ana biashara kubwa tuu. Unakuta mtu ana kampuni kubwa tuu, lakini hana website.
Hizi account za mitandao ya kijamii zinatupa viburi ila kwa wenzetu kama huna website hawawezi kukuchukulia serious na utakua ukipishana na wateja wako.

ii. Serikali haijaweka mazingira wezeshi; ngoja nielezee kidogo.....
kama umewahi kufanya biashara za online za kimataifa..unazohitaji kutuma na kupokea pesa kutoka ulaya, marekani na kwingineko utakua umeshanielewa, kuna ugumu mkubwa sana wa kufanya miamala ya kimataifa.

Hatupati huduma kama PayPal ambazo zingerahisisha huduma za kifedha mitandaoni, kuna kipindi laini za safaricom ya Kenya ziliuzika sana Bongo, yote hii ili kujiunganisha na dunia kupitia nchi ya Kenya kwa sababu nchi yetu haijaweza kufanya hivyo. Ni jambo la aibu.

Nimewahi kusikia kauli kama "TANZANIA SIO KISIWA" lakini tumejifungia sana katika masuala ya kiuchumi na kujitangaza kama nchi kiasi kinachofanya mimi niione nchi yangu kama KISIWA.

Hata niki'gugo' orodha ya lugha maarufu duniani, sehemu ya kiswahili watakua wameweka bendera ya Kenya. 'Hatujitangazi'.


HITIMISHO
Daraja la kati ni daraja lisilo na uhakika wa maisha—Ni daraja lenye msongo na mkazo kushinda madaraja ya maskini na matajiri, Ni daraja lenye uoga wa kesho kupoteza vyote na kushindwa kuishi level ambayo wamekua wakiishi, na hiyo ni kwa sababu uwekezaji wao na mali zao hazina msingi imara.

Hutakiwi kuwaza kua katika daraja hili

Naiona kesho ambayo inazidi kutengeneza mazingira magumu kwa daraja hilo.

Naliona likisinyaa na kutoweka.



BASI MIMI-NA-WEWE TUFANYE-NINI KAMA-VIJANA.

ili kua salama na hiyo kesho inayokuja;

Vijana,

Yani mimi na wewe inabidi tuwe MATAJIRI

Hakuna mbadala wa hilo.


HOW? KIAJE YANI?

Tunafanyaje-fanyaje ili kuwa matajiri?

Historia inapendekeza kuwa; watu wanakua matajiri kwa:

Kutatua matatizo, "By Solving Problems"

And solving problems is a skill,

Kwa vijana wenzangu nawashauri tuwekeze muda wetu katika kutengeneza ujuzi. Ujuzi unaenda kulipa zaidi ya vyeti.


Sitaki kuongea kwa nadharia lakini njia pekee itakayotutoa ni kutumia ujuzi wetu kutatua matatizo yaliyopo katika jamii zetu.

Historia imethibitisha hilo; chunguza matajiri wote unaowafahamu kuna huduma fulani ya kipekee-yake wanaizalisha.

Kwenye akili zetu ndo kuna utajiri wetu, tukizitumia vizuri bila kuathiriwa na mitazamo ambayo jamii imeshatuchorea, tunaweza kufanya mambo makubwa na kufika mbali bila mipaka.

Natambua sio rahisi kupata wazo jipya, natambua sio wote watakua wavumbuzi. Lakini kila mmoja ana uwezo wa kuboresha na kukiongezea ubunifu kile ambacho tayari kinafanyika.

Tukiwa na mitazamo na malengo ambayo tumekubaliana na nafsi zetu kuyapigania hakika tutafanikisha. Tusikate tamaa. Tuwe na ngozi ngumu. Tusilie-lie tuikatae kabisa 'entitlement mentality' haitatufikisha popote maana maisha yetu ni mizigo yetu wenyewe. Na dunia haitujui na hata kuja ndani yake tulikuja mmoja-mmoja.

Pia tupende kushirikiana na kushikana mikono. Tufanye kazi kama timu. Ni rahisi kutoboa tukiwa kama kundi. Matajiri wanaungana kila siku, kuna kitu cha kujifunza hapo.

Ubinafsi kwa kivuli cha kujiita 'jeshi la mtu mmoja' ni kauli za watu wasiofanikiwa. Ukienda Google kuna ushahidi wa matunda ya ushirikiano.

Uki'google aliegundua Facebook utamuona Markzuckerberg na majamaa zake akina Saverin...
Pia Twitter utamuona............ na............
Apple utamuona................na ................
Pia Microsoft utamuona Billgate na ..............

Fanya hivyo kwa kampuni kubwa nyingine unazozijua utaona kuwa ili kujenga Roma unahitaji watu. Kuna power katika kushirikiana hasa kwa sisi vijana.

Ushirikiano unahamasisha uwajibikaji; ukiwa peke yako ni rahisi kughairisha jambo na kuchukulia poa vitu.

*************

Ahsante sana.
 
Naomba tusisahau ku vote, kura yako ndo itakayolipa andiko hili thamani. Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom