Kesho TFF kumtangaza Mdhamini wa ligi kuu 2021/2022

Shirikisho la mpira Tanzania, Tanzania Football Federation (TFF) Kesho linategemea kumtangaza Mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2021/2022.

Shirikisho hilo limewataka waandishi wa habari kuwepo kesho asubuhi katika ofisi za TFF zilizopo Dar es Salaam.
Hivyo kesho Mdhamini atatangazwa rasmi.
Nbc

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
vzuri TFF ,vilabu navyo visijibweteke.. vitafute wadhamini w maan wwasaidie kuboresha at viwanja wanavy chezea il tuon soka safi.
Kweli kabisa ngoja tusubiri tuone nani ni nani
 
Benki kama NMB ama CRDB kwa ukubwa wao na utengenezaji faida sijui kwa nin hawajaiona hii fursa.

Kwanza timu zimekuwa chache.

Ligi imekuwa na mvuto mkubwa sana kwa kuzipa biashara zao matangazo ya maana.

Hata kama sio full sponsorship, wangeweka hata kwenye zawadi tu.
Huenda kwa sasa wanaweza kuiona hiyo fursa
 
Azam hawezi kuwa mdhamini ,sheria hairuhusu mdhamini awe na timu ligi kuu, haiwezekani uwe na timu ligi kuu haalafu ukawa mdhamini wa ligi
Sheria ya nchi gani hiyo jamaa?!

Azam media si mdhamini wa ligi upande wa "Haki za matangazo"!!!?

South Africa kuna Super Sport fc na ligi yao inadhaminiwa na DStv mbona imewezekana au hiyo ni sheria ya TFF peke yake?!
 
Suala la viwanja ni suala la timu husika siyo bodi ya ligi
Team nyingi za ligi kuu hazimikili viwanja vyao...vingi ni vya ccm.

Ila Rais alisema viwanja vifanyiwe matengenezo na kama wakishindwa wavikabidhi kwa watu binafsi
 
Sheria ya nchi gani hiyo jamaa?!

Azam media si mdhamini wa ligi upande wa "Haki za matangazo"!!!?

South Africa kuna Super Sport fc na ligi yao inadhaminiwa na DStv mbona imewezekana au hiyo ni sheria ya TFF peke yake?!
haki ya matangazo hapa ,lakini siyo udhamini Kama wa ligi kuu Kama Vodacom ,hiyo ni sheria ya hapa.huwezi ukadhamini ligi halafu una timu kwenye ligi pia huwezi kuwa timu mbili kwenye ligi kuu
 
Team nyingi za ligi kuu hazimikili viwanja vyao...vingi ni vya ccm.

Ila Rais alisema viwanja vifanyiwe matengenezo na kama wakishindwa wavikabidhi kwa watu binafsi
Ni heri viwanja hivi virudi serikalini viwe na fungu la bajeti ya matengenezo kila mwaka.
 
haki ya matangazo hapa ,lakini siyo udhamini Kama wa ligi kuu Kama Vodacom ,hiyo ni sheria ya hapa.huwezi ukadhamini ligi halafu una timu kwenye ligi pia huwezi kuwa timu mbili kwenye ligi kuu
Asante kwa kututoa giza kidogo
 
Back
Top Bottom