Kesho ndio tunaenda kuufahamu unafiki wa baadhi ya watanzania

Timu yetu ya Taifa (Taifa Stars)Kesho ipate ushindi wowote ule dhidi ya Senegal,hata suluhu na kichwa cha habari hapo juu kinakwenda kutimia.
Hapa nilipo niko na Waburundi,Wazimbambwe,Waganda,Wakenya,WaSouthAfrica wenyewe bila kusahau Nigerians....Jamaa hawaongelei negative kuhusu timu zao za Taifa kabisa na unafiki/hypocrite kwao ni Ugonjwa.
Nyie watanganyika ni malofa sana maana mmeaminishwa uzalendo ni kujipa matumaini hewa au?.cha muhimu ni kuishabikia timu isijalishe sijui makonda,polepole ,sijui magufuli wameteka timu
 
wacheze kwanza. Wakifanya vizuri. Mpunga mwingi watapewa hadi waukimbie.
hata mechi moja hawajacheza wanakimbilia posho?
hyo ni timu ya taifa Lao. Wanatakiwa wapigane katika kila hali. Kikubwa wapewe chakula na maji ya kutosha na vifaa vya mazoezi.
Wachezaji waligoma wamepewa dola 75 badala ya 300 posho
 
Shida inakuja watu wanapofikiria football ni kama mbio ukiweka nguvu zako binafsi mnatobos ,football ni team work.sasa team ya Taifa letu haina kiungo mbunifu hata mmoja kukaa nyuma tu tutashinda njaa
 
Mlipogeuza timu ya Taifa kuwa timu ya Chama mlitegemea nini? Ni lipi ambalo CCM imeisaidia Taifa stars hadi muigeuze kuwa timu ya Chama?
Hivi nyie watu mbona mnakuwa Ma Hayawani kiasi hiki? Aliyesema Timu ya taifa ni ya chama ni nani mkuu. Usipende kufuata mkumbo kwa vitu usivyokuwa na uhakika navyo. Alafu tumelikumbatia pepo LA chuki kila nyanja, hivi kweli tutafika? Mwenyezi Mungu tunaomba utuponye na huu uovu wa chuki. Pepo chuki hebu ondoka katika vichwa vya watz na upendo na Amani vitamalaki miongoni mwetu na sote tuseme na iwe hivyo.
 
Sio unafiki hata huko Brazil tumeona watu wanaizomea team yao ujuwe kuna kitu hawajapenda. Mimi naipenda Taifa Stars tatizo hawa wana siasa kama naona siku wanarudi bongo wameshinda baadhi ya game wa kijani watajaza airport hapo na kampeni za uchaguzi zitapigwa. Hapana tupigwe tu turudi tuheshimiane hakuna budi. Nawachukia baadhi ya watu na nikiwaona wameichukuwa team ya Tanzania napata shida maana hata ahadi zile za Million 10 sijui hakuna mtu anathubutu kuuliza walipewa? zile za Simba mbona na video ikatolewa nataka kujuwa tunawatumia tu hawa wachezaji kwa malengo ya kisiasa? ni kama wameambiwa kaeni kimyaa ila na uhakika hakuna walichopewa sasa ukiona viashiria hivyo ujuwe hatuko serious tunatumiwa sote. kwa mimi big No tupigwe tu mpaka na majirani zote heshima irudi. Yanga wametumiwa pia kupewa kiwanja na hotuba za vijembe hatuwezi kwenda hivyo kabisa tunauwa mpira.
 
Ninachojua mimi hata nchi iwe na vita kali kiasi gani Timu ya Taifa ikicheza watu wanaweka silaha chini...
Bakini na siasa zenu huko huko na Ma CCM cjui timu ni ya chama gani mm sijali....Kwa kifupi nishamuua Msenegali zamani sana,nasubiria mpunga hapa.
2019-06-23%2007.45.03.jpeg
 
Hakuna unafiki, mie naaamini kabisa mpaka halftime tutakuwa tushapigwa 2goals na second half 3goals to make a total of 5, to mean awamu ya tano nikupigwa tu!!!
 
Unajua haya mambo haya... Eti uzalendo ni kuamini kuwa Taifa stars ya Ally Sonso inakwenda kuifunga Senegal ya akina Sadio Mane, Kalidou Koulibaly

Binafsi natamani timu ya taifa langu ishinde, lakini sioni hilo likitokea.... Tunakwenda kupigwa mpaka tuchakae leo.
 
Mwenyezi Mungu tunaomba utuponye na huu uovu wa chuki. Pepo chuki hebu ondoka katika vichwa vya watz na upendo na Amani vitamalaki miongoni mwetu na sote tuseme na iwe hivyo.
Amen 🙏🙏🙏..!
 
Hivi nyie watu mbona mnakuwa Ma Hayawani kiasi hiki? Aliyesema Timu ya taifa ni ya chama ni nani mkuu. Usipende kufuata mkumbo kwa vitu usivyokuwa na uhakika navyo. Alafu tumelikumbatia pepo LA chuki kila nyanja, hivi kweli tutafika? Mwenyezi Mungu tunaomba utuponye na huu uovu wa chuki. Pepo chuki hebu ondoka katika vichwa vya watz na upendo na Amani vitamalaki miongoni mwetu na sote tuseme na iwe hivyo.

Mnapokaa kimya watu wanaotumia madaraka yao kuendekeza uonevu wa kiitikadi kuhodhi timu mnategemea nini? Senegal funga hao wahuni wa ccm.
 
Back
Top Bottom