Kitoabu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 10,326
- 10,943
Kwa mara ya kwanza katika uhai wangu, kesho naenda kupima Ukimwi.
Sio kwa hiyari yangu, bali ni mifumo ya kidunia imenibana. Sijui nani alieweka ushauri wa kupima UKIMWI kwa lazima kwa mama mjamzito? Mbaya zaidi si mama mjamzito pekee, bali wanataka na mumewe pia.
Mimi na mke wangu tayari tuna watoto wawili, lakini katika mimba zote hizo sijawahi kuhudhuria kwenye zoezi la kupima Ukimwi.
Mtoto wa kwanza kazaliwa 2014 kipindi hicho nadhani hakukua na ulazima kwa mke na mume kwenda kupima (nazungumzia kwa Mocambique)
Mtoto wa pili kazaliwa 2017, hapa nilikua mbali na mke wangu (nilimuacha na ujauzito wa miezi 5) hivyo mke wangu aliongopa kuwa mumewe kafa, kwa mbinde sana wakamsaidia.
Ila trip hii wamekataa mpaka tumeamua kwenda hospital ya wilaya nyingine.
Mke wangu ana ujauzito wa miezi 4, tatizo ujauzito wake unamzingua, hivyo kila alipo kwenda hospital walimwambia aanze klinik, hivyo utaratibu ni kwenda na mumewe.
Ni mwezi sasa nimekua nikipiga chenga, lakini namuonea huruma mwenzangu mimba inamsumbua, hivyo nimeamua KUJILIPUA liwalo na liwe, kesho asubuhi sana nawahi hospital, kupima UKIMWI.
Pressure ipo juu, naomba nisikutwe na moto, nikikutwa nao itakua balaaa. Nitamuambiaje mama mwenyewe?(mkewangu)
NB: Siogopi Ukimwi (siamini kama Ukimwi unaambukiza) ninachohofia, mke wangu nitamuacha na majonzi sana.
Uamuzi wangu ni hivi, kama nitakutwa na ukimwi alafu mwenzangu hana (sintaogopa) nitamuuliza anaamua vipi?
Tunaachana ama tunasonga mbele?
Ikiwaka wote hatutakutwa na ukimwi nitafurahi kinoma (sintoifananisha hiyo furaha)
Balaa ikiwa wote tutakutwa na Moto/ Shati la maua maua (Ukimwi) hapo sasa itakua balaaa, maana mwenzangu atapagawa sana, kitendo kitachoniachia majonzi moyoni.
Nimejipanga, hata niambiwe nina moto sintakula ARV ng'o! Yani siri ARV hata kwa Risasi ya moto kichwani.
Mwisho, USHAURI NA MAONI yenye busara vinahitajika.