Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 158
- 175
Kesho mambo kuwekwa hadharani miradi yote iliyotekelezwa na Serikali
"CCM imejipanga"
Kamati ya siasa Wilaya ya Nyamagana, kesho itaanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 -2020.
Kamati hiyo kesho itakagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kuanzia Januari 2019 hadi Desemba 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Phillip Nyimbi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo, alisema kamati hiyo ya siasa itakagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali kuu na fedha za ndani.
Nyimbi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Nyamagana, alisema kamati hiyo ya siasa itatembelea miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu, maji na miundombinu.
Alisema fedha za utekelezaji wa miradi hiyo, zimetokana na fedha zilizotolewa na Serikali kuu na fedha za ndani ambazo zimetekeleza miradi hiyo itakayoleta manufaa kwa wananchi.
"Tutatembelea miradi katika kata zote zilipo Nyamagana, ikiwemo kata ya Igoma, Nyamagana, Lwahnima na kata zote ambazo miradi imetekelezwa," alisema Nyimbi.
Alisema miradi iliyotekelezwa na Serikali kupitia fedha za serikali kuu na za ndani imefanya kazi kubwa na ya mfano, kwani miradi mingi imefanyika kwa kiwango kikubwa na kilicho bora.
Nyimbi alitumia nafasi hiyo kuwaalika wananchi na wadau wa maendeleo kujitokeza kwenye maeneo yao kwenda kuangalia utekelezaji huo wa miradi ya maendeleo.
Miongoni mwa miradi ambayo imetekelezwa na Serikali kuu ni pamoja na mradi mkubwa wa maji nyegezi, ujenzi wa vyumba vya madarasa, kituo cha afya kilichopo kata ya Mhandu pamoja na mradi wa wajasiliamali wadogo wa kutengeneza viatu na bidhaa mbalimbali katika eneo la Makoroboi.
Kutoka kwa Mseti.