Kesho Jumamosi viongozi wakuu wa CHADEMA, ACT Wazalendo kuzungumza na Waandishi wa Habari-Makao Makuu ya CHADEMA

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
6,309
2,000
Tatizo la nchi hii ni kwamba iko mikononi mwa limbukeni na washamba wasiojua nafasi ya Tanzania katika Afrika na duniani. Waliokuwepo wakati wa Baba wa Taifa wanakumbuka ziara ya Mwalimu alipoitembelea Marekani na mapokezi na heshima aliyopewa hakuna Rais kutoka Afrika amewahi kupewa toka wakati huo labda tu ya Mandela ndiyo iliikaribia. Mwalimu pia alikaribishwa nchini Uingereza katika ziara ambayo haina mfanowe Afrika hadi leo.

Nyakati hizo hukuhitaji viza kuingia Uingereza na nchi yoyote ya Jumuiya ya Madola, visa yako ilikuwa ni Utanzania wako tu. Lakini leo Tanzania inadharauliwa na inachekwa ikiwekwa kundi moja na mataifa ya ajabu ajabu. Mwakilishi wa Tanzania alipokuwa akiongea ndani ya Umoja wa Mataifa, dunia nzima ilisikiliza. Hiyo Tanzania ya siku hizo bado inakumbukwa huko nje kuliko inavyokumbukwa na baadhi ya viongozi tuliowasukumizia madaraka. Masikini Tanzania!
Huko kusifiwasifiwa na kubembwa ndo kumetufanya tuwe wagonjwa wa kuwategemea hao jamaa unaodhani ni marafiki wa kweli. Unahitaji tu kuangalia kwa ukaribu wa kina kilichotokea (na kinachoendelea kutokea) Libya na Venezuela ili uelewe rangi kamili na nia ovu ya Western & European imperialists. Huu ni wakati wa Tanzania kusimama imara, yenyewe. Hatutaki tena nchi yetu iwe koloni la London na Washington. Rais Magufuli ndiye kiongozi sahihi wa kututoa huko.

Jitafakari mara mbili2 pale unapoona adui yako anakusifia. Rais wetu anachukiwa kwa sababu amekataa kabisa, kwa kauli na vitendo, kuwalamba migongo hao jamaa, ametuhakikishia kwamba nchi yetu ni tajiri sana na ingepeswa kuwa nchi hisani kwa mataifa mengine, ameonesha mfano wa nini kinachotakiwa kufanyika, amesimama madhubuti dhidi yao na akashinda mara zote, mathalani, kwenye ule mtanduko wa korona, ametufanya kwa mara ya kwanza sisi Watanzania tujisikie ni kama watu wenye utu kamili na mchango kwa dunia.

Kubwa zaidi, ameikabidhi nchi yetu chini ya uongozi wa Maulana. Ni suala la muda tu, mataifa mengi yanakuja kuiga kasi ya ustawi & maendeleo ya kweli kwenye taifa zuri la Tanzania.
 

mbongo_halisi

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
5,944
2,000
Kesho majira ya saa nne asubuhi viongozi wakuu wa CHADEMA na ACT Wazalendo kuzungumza na waandishi wa habari. Yatafanyika makao makuu ya CHADEMA mtaa wa Ufipa Kinondoni.

Stay tuned!
Kwenye kile kibanda cha kupanga? Hawa hawana lolote, wanataka kusema tu kuwa wanaachana na siasa na kuua vyama vyao. Washaisoma namba sasa, kudadadeki zao.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
12,916
2,000
Nina wasiwasi kama huo mkutano utafanikiwa kufanyika, vifaru vitalizingira jengo lote la makao makuu ya Chadema. Tanzania mpya ya kijani.
Nitakwambia kwa nini haiwezi kuwa hivyo.

Si uliona walivyojitahidi kuonyesha kwamba uchaguzi utakuwa wa Haki na Huru? Wewe unadhani kwa nini walifanya hivyo, pamoja na kwamba mipango ya kunajisi huo uchaguzi ilikuwa ikiendelea!

Hapa pia hawawezi na hawataki kabisa waonekane kuvuruga ushindi wao. Wanapenda sana waonekane 'malaika' wakati huu na kuulinda 'ushundi' wao.

Na zaidi ya hivyo: unakumbuka siku ya Lissu Kurudi nyumbani; kuna unyasi wowote uliokanyagwa?
 

Mwenyewe0000

Member
Oct 30, 2020
51
125
Bado napata shida wale tunaotegemea gmail, mitandao ya kijamii kufanya biashara na wengine ndo kazi zetu, je kutakuwa na fidia zozote. Tunaonewa bundle za internet ni zetu ila wana block mitandao
 

redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,992
2,000
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi. Tunakumbushana tu.
 

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,422
2,000
Uyu jamaa ni Nan mbona anauza sura sana
Screenshot_20201031-111804.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom