Kesho asubuhi Maxence kufikishwa Mahakamani kwa amri ya mahakama baada ya mawakili wake kuomba

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
717
1,000
Kesho tarehe 19 Mwanzilishi mwenza wa mtandao wa JamiiForums kufikishwa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar kwa amri ya Mahakama baada ya Mawakili wake kuomba.

Atafikishwa Mahakamani hapo muda wa saa 2 asubuhi ambapo inategemewa maombi yake ya dhamana yatasikilizwa.

Cz9rRUEWIAA7HpW.jpg
 

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
Nyakati za Mfalme Suleiman;ili uwe kiongozi na uheshimike,ilihitaji uwe na jeshi kuuubwa lenye farasi wengi wa mapigano,uwe na askari wengi,mateka wa kukaa mstari wa mbele,mifugo mingi kama kondoo na ngamia na kashalika uteke himaya nyingi za Wafalme wengine ili kujizatiti ktk ufalme wako.Ukiyatimiza haya;wewe unakuwa Mfalme mwenye nguvu kupita falme zote...Jeshi imara ilikuwa ni sifa ya Mfalme.

Mfalme Suleiman alipata nafasi ya kuambiwa na MUNGU wake;apewe nini ili awe mmoja kati ya Wafalme wenye milki kubwa,nguvu na ushawishi katka himaya yake?Bila wengi kutegemea,Mfalme Suleima alimuomba MUNGU wake ampe HEKIMA!!

Mfalme Suleiman alimwambia Mungu..."NIPE HEKIMA,ILI NIWEZE KUWAONGOZA WATU WAKO KWA HAKI NA AMANI.."...Maana TUNDA la Haki ni AMANI.

Suleima angeweza kuomba mafarasi,ngamia,Jeshi,mali na watumwa wengi wa kufuru,lkn aliomba HEKIMA..Maana hekima ndio msingi wa Uongozi.

Ndio maana ktk hadidhi zinazothibitisha HEKIMA ya SULEIMAN ni ile ya kutatua ugomvi wa wanawake wawili waliokuwa wanagombania mtoto,kila mmoja akisema huyu ni mwana wangu,na mwingine akisema huyu ni wangu uzao wa nyonga yangu.Shauri lao likafika mpaka kwa Mfalme Suleiman ili lipate ufumbuzi.

Mfalme Suleiman akawaambia wale wanawake;kwa sbabu wote mnamng'ang'ani mtoto huyu;basi ni bora mkose wote au mgawane,nitamchukua mtoto huyu na kumchanranga;Yule Mama asiye wa mtoto akasema "Itakuwa vema Mfalme"...Lkn Mama mwenye mtoto akasema,kuliko kumuuwa mtoto huyu,ni bora uumpe mwenzangu aishi nae na sio kuutoa uhai wake.Hatimaye Mfalme akagundua ni nani mwenye mtoto.

Hii ni HEKIMA....hekima ni Tunda la haki....Tuwaombee viongozi wetu wawe na hekima.Suleiman inasemwa alikuwa na wake 400 na masulia 600...wakati wengine wanatamani hata kuwa na wake wawili wa hadharani,japo mafichoni inajulikana wana wake zaidi ya wawili.

Kumbe Suleiman kwa hekima zake,hakuhitaji hata kuomba apate wawili ili aishi miaka mingi ya afya kama wengine wanavyotamani Mwinyi anavyoishi,wale wake wawili kama wa Mwinyi.Siri ya Mwinyi sio wake wawili...Inaweza kuwa ni HEKIMA....Hekima husafisha roho na mwili
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,532
2,000
Tumefikia mia tano tuliojiandikisha kufanya maaandamano ya amani,mabango yapo tayar tunahitaji uhuru
Jamani, mwacheni mwenzetu angalao atoke huko Keko. Mnaotishia kuandamana hamjui mtamfanya hakimu amwangalie kwa jicho baya?? Tz hakuna mwenye umaarufu siku hizi. Mwacheni Melo atoke Keko jamani. Wingi wenyu mahakamani haumpi uhuru bali madhara zaidi.
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
50,960
2,000
Maandamano tunaanzia wapi...naomba muongozo
Maandamano ya nini wewe.
Waacheni mawakili wafanye kazi zao.
Msifanye mambo kisiasa kumbuka Jpm mpenda sifa mkijifanya mnaandamana au mnamshinikiza atatakua kujionyesha kuwa yeye ni nani.
Na Maxence ataendelea kuumia.
Cha muhimu tuanze kumsifia huyu dikteta anapenda sifa sana hata hapa JF mkianza kumsifia tu mtaona kama atakuwa anafuatilia .
Na hasa hasa atajiunga hapa
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
50,960
2,000
Mimi kesho nitakuwepo mwili jumba.
Ole wake mtu aje na t shirt ya chadema au ukawa
Nitamtudisha nyumbani kwa mikono yangu.
Hii issue ya Max sio ya siasa ni ya JF na JF haina chama .
JF nyundo ni nyundo na nyeupe ni nyeupe na Max ndio alivyo hana chama wala hayupo kisiasa.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,309
2,000
Kuna Watu Wanawatumikia Watu Kuliko Hata Wao Wenyewe ,wazazi Na Familia Zao - Kushikiwa Akili Ni Jambo Baya Sana.
 

Freema Agyeman

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
3,595
2,000
Maandamano ya nini wewe.
Waacheni mawakili wafanye kazi zao.
Msifanye mambo kisiasa kumbuka Jpm mpenda sifa mkijifanya mnaandamana au mnamshinikiza atatakua kujionyesha kuwa yeye ni nani.
Na Maxence ataendelea kuumia.
Cha muhimu tuanze kumsifia huyu dikteta anapenda sifa sana hata hapa JF mkianza kumsifia tu mtaona kama atakuwa anafuatilia .
Na hasa hasa atajiunga hapa
Safi sana. Free Max.
 

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,554
2,000
Hivi rais wa wananchi Mh. Edward Lowassa bado hajaongelea kuhusu nchi ilivyo sasa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom