Ningependa akina kaka/baba wayajue makosa yao yenye kusababisha kuvunjika au kuparaganyika kwa uhusiano

Kuna mada-jibu-mapigo - mtizamo wa wanaume..... nadhani lengo letu siyo kupambana bali kuelimishana tu.Uzuri wa majukwaa haya yanatoa fursa kuzungumza yale ambayo katika hali ya kawaida inakuwa ngumu kuyasema. Haina lengo la bashing au kutupiana lawama kama wengine wanavyodhania.......
haya twende kazi....
 
kero kubwa wanawake wanazowapa wanaume

1.kumchukulia mumeo kuwa ni loser kwa kuwa kipato
kimepungua au ameachishwa kazi au umepata kibuzi nje chenye pesa..

2,kutodai talaka pale unapoona kuwa basi,badala
yake mnaanza vituko na maneno ya kuudhi....

nitaendelea....

Boss....... hii kali!
Kwanini adai talaka? kwanini wewe usianze mbele?
 
Wos hapo ni maoni tu from
experience....
Wa kwangu hadai talaka...........
 
Wa kwangu anadai annivesary party...lol...
Bado haamini kuwa nimemuoa....lol
 
Kuna mada-jibu-mapigo - mtizamo wa wanaume..... nadhani lengo letu siyo kupambana bali kuelimishana tu.Uzuri wa majukwaa haya yanatoa fursa kuzungumza yale ambayo katika hali ya kawaida inakuwa ngumu kuyasema. Haina lengo la bashing au kutupiana lawama kama wengine wanavyodhania.......
haya twende kazi....
Kweli kabisa WOS hii ni sehemu ya kujifunza, kwa sisi ambao bado hatujaingia kifungoni kuna elimu kubwa na ya muhimu tunaipata.
 
Mabandiko kadhaa yamefanya nianzishe mada hii. Inaelekea akina kaka/baba wanadhania kuwa mzigo wa kuimarisha uhusiano ni kazi ya akina dada/mama.Wanadhani kuwa kuna vitu wakina dada/mama wakivifanya vingeimarisha mapenzi au mahusiano.Kuna dhana pia kuwa wanawake wanapoolewa wanabweteka na kujiona wamefika.
Binafsi nadhani wote tuna jukumu na wajibu wa kuimarisha penzi, ndoa au uhusiano. Ningependa akina kaka/baba wayajue makosa yao yenye kusababisha kuvunjika au kuparaganyika uhusiano. Nitaanza kwa machache kama ifuatavyo:
1.Kujisahau na kubweteka pale mwanaume anapompata mwanamke/mke.
Hata wanawake nao hukerwa na hali hii, kwamba mwanaume anadhani kuwa maadam kaoa au kapata mpenzi, basi hawajibiki tena kuonyesha kujali au manjonjo mengine aliyokuwa akimuonyesha mpenzi wake. Maua hayaletwi tena, hakuna simu za hapa na pale, hakuna kujijali yeye mwenyewe nk.

2. Utegemezi
Baadhi ya wanaume wamekuwa na tabia ya kuwaachia wake zao mzigo wa familia, kuanzia chakula, ada za shule, na gharama nyingine.Hapo panachekesha hasa pale mwanaume anapolazimisha atambuliwe kuwa yeye ndio kichwa cha familia lakini hapo hapo haonyeshi uongozi wa aina yoyote. Hii inakera sana.

3. Wivu uliovuka mipaka
Wivu ni kiashiria kizuri cha kupendwa sikatai na huwa Unanogesha mapenzi sana.Hakuna raha mwanamke anaipata kama pale mpenzi wake anapoonyesha wivu. Inachekesha kidogo lakini.Wivu wa mpenzi pale hajakuoa na wivu wa mume wakati mwingine huleta ladha tofauti kabisa. Mpenzi wako akiwa na wivu huvumilika na kufurahisha.Wivu wa mume wakati mwingine huwa kero. Kero hasa pale unapoelekezwa kukupunguzia tija kikazi, unapoelekezwa kukupunguzia kujiamini. Mume anapoonyesha wivu unaolekea katika unyanyasaji hapa hauchochei penzi bali huchochea chuki na kuweka ufa katika uhusiano.

nitarudi tena.... endelezeni kina dada/mama...
kina kaka/baba mnaruhusiwa kuchangia pia...

...WOS, hii mada kwa namna moja ama nyingine inanipa depression tu. Anyway, labda nipo kwenye mood swing siku mbili hizi. Natamani sana kuchangia lakini aaarrrgghhh, ....mijanamke mingine hata uipikie, uitandikie kitanda, uikogeshe na 'katika na hayo' hairidhiki ng'o!
Haimaliziki mwezi atatafuta sababu ya kukuudhi na kulalama. Raha jipe mwenyewe, pesonally am totally exhausted.
Investing kwenye taasisi hii inayoitwa mapenzi ni sawa sawa na kufungua account ya 'Upatu!'
 
Mkuu Mbu wengine ukiwafanyia hayo mambo wanaweza kutangaza kwa mashoga zao kuwa wamekuweka kiganjani!
 
Pia kutupa tupa vitu yani nyumba ipo neat akirudi viatu & soksi sebuleni mana binafsi inanikera sana..Sijui kwa sababu napenda kuona mpangilio wa vitu mahali panapostahili au la!!

Akitaka kutoka yeye anakutaarifu hata kwa sms wakati yupo eneo la tukio ila ukitaka kutoka wewe uombe ruhusa,agrrr! hii kera sana mimi kwakweli mana ni ubabe!!..

...BJ, nahisi kama hayo ni mapungufu tu, ambayo yapo ndani ya uwezo wako kukabiliana nayo. Ignore!
Kasheshe unapokuwa na mtu ambaye ni Muongo, Mchonganishi, Mharibifu!...
 
Mkuu Mbu wengine ukiwafanyia hayo mambo wanaweza kutangaza kwa mashoga zao kuwa wamekuweka kiganjani!

...si ndio hapo sasa?

anyway, bahati mbaya ama nzuri anapoongelea hayo mashoga ndio kwanza mashoga wanapojisogeza karibu kutaka urafiki na mume mtu. Binafsi sijali kabisa kutangaziwa huko nje eti nimewekwa kiganjani. Heshima tu iwepo, sio tena mke anakupigia simu akiwa Saloon anakuulizia kama umebandika tayari maharage na vitunguu umeshakata kwani ana njaa sana...akirudi akute chakula!
Au wageni wamekuja, anakufokea wewe ndio ukaandae meza na chakula...
wengine tunafuata mila na desturi japo kwa mbali bana
 
...WOS, hii mada kwa namna moja ama nyingine inanipa depression tu. Anyway, labda nipo kwenye mood swing siku mbili hizi. Natamani sana kuchangia lakini aaarrrgghhh, ....mijanamke mingine hata uipikie, uitandikie kitanda, uikogeshe na 'katika na hayo' hairidhiki ng'o!
Haimaliziki mwezi atatafuta sababu ya kukuudhi na kulalama. Raha jipe mwenyewe, pesonally am totally exhausted.
Investing kwenye taasisi hii inayoitwa mapenzi ni sawa sawa na kufungua account ya 'Upatu!'

Pole Mbu!
Umesema mwenyewe " mijanamke mingine" meaning its a few.... na pia kuna wanawake wanaosema hivyo hivyo.."mijanaume mingine"... Nadhani kuna sababu nyingi zinazopelekea kuwepo na chuki hizi hadi kuitana majina mabaya hivi.Ndio tunataka tuzijue kwa kuziweka wazi hapa ili wale ambao bado hawajaharibikiwa wakwepe kuharibu mahusiano yao.

I guess there comes a time in life when couples resent each other.... hii inasikitisha sana.... we need to come up with ways to arrest the situation.

Hivi jamani, ni sawa kuitana majina mabaya baina ya wanandoa?
Kitu kingine kinachochea chuki ni maneno na kauli mbovu...Kuna baadhi ya wanaume wao matusi kutolea wake zao ni kama kupiga chafya!.Wamesahau kabisa yale maneno mazuri kama darling, honey, sugar, sweetlove, honeypie, la aziz, mahbuba, kichuna, kimanzi, .............. mhhh!
 
Habari. nimekuja tusaidiane. Hapa kwenye samahani kuna mambo makubwa!!!!
Sema samahani. na sio :baisi samahani.
SAMAHANI YA KWELI NI GHARAMA SANA. KWA WALE WAJANJA HAWAKUBALI KUISEMA, KWANI WANAOGOPA KUWAJIBIKA.
Ikiwa umeiba lazima urudishe, hapo samahani itakua ya kweli.
Je/? kwa yale mengine tufanyeje!!!?
 
Mengine yepi ndugu? Kuwa muwazi
 
Mbu pole kaka ila hakuna mwanamke asiyefunzika..... Mtafutie dawa atapona tu.

Mimi mwanamme ananikera akiwa disorganized! Aggggr maana hata sijui nianzie wapi!
 
Pia kutupa tupa vitu yani nyumba ipo neat akirudi viatu & soksi sebuleni mana binafsi inanikera sana..Sijui kwa sababu napenda kuona mpangilio wa vitu mahali panapostahili au la!!

Akitaka kutoka yeye anakutaarifu hata kwa sms wakati yupo eneo la tukio ila ukitaka kutoka wewe uombe ruhusa,agrrr! hii kera sana mimi kwakweli mana ni ubabe!!..
Mbu pole kaka ila hakuna mwanamke asiyefunzika..... Mtafutie dawa atapona tu.

Mimi mwanamme ananikera akiwa disorganized! Aggggr maana hata sijui nianzie wapi!

...BJ na wewe mnaimba wimbo mmoja.
Wengine ni vice versa, maza hausi ndio ana kasoro hizo.
Unaishia kugomba weee...

...ule msemo "asiyefunzwa na mama'ye,...!" hata na dunia haiwezi wafunza lolote!
 
Pia kutupa tupa vitu yani nyumba ipo neat akirudi viatu & soksi sebuleni mana binafsi inanikera sana..Sijui kwa sababu napenda kuona mpangilio wa vitu mahali panapostahili au la!!

Akitaka kutoka yeye anakutaarifu hata kwa sms wakati yupo eneo la tukio ila ukitaka kutoka wewe uombe ruhusa,agrrr! hii kera sana mimi kwakweli mana ni ubabe!!..
That could be a sign that the king has returned into his territory.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom