WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,458
- 956
Mabandiko kadhaa yamefanya nianzishe mada hii. Inaelekea akina kaka/baba wanadhania kuwa mzigo wa kuimarisha uhusiano ni kazi ya akina dada/mama.Wanadhani kuwa kuna vitu wakina dada/mama wakivifanya vingeimarisha mapenzi au mahusiano. Kuna dhana pia kuwa wanawake wanapoolewa wanabweteka na kujiona wamefika.
Binafsi nadhani wote tuna jukumu na wajibu wa kuimarisha penzi, ndoa au uhusiano. Ningependa akina kaka/baba wayajue makosa yao yenye kusababisha kuvunjika au kuparaganyika uhusiano. Nitaanza kwa machache kama ifuatavyo:
1.Kujisahau na kubweteka pale mwanaume anapompata mwanamke/mke.
Hata wanawake nao hukerwa na hali hii, kwamba mwanaume anadhani kuwa maadam kaoa au kapata mpenzi, basi hawajibiki tena kuonyesha kujali au manjonjo mengine aliyokuwa akimuonyesha mpenzi wake. Maua hayaletwi tena, hakuna simu za hapa na pale, hakuna kujijali yeye mwenyewe nk.
2. Utegemezi
Baadhi ya wanaume wamekuwa na tabia ya kuwaachia wake zao mzigo wa familia, kuanzia chakula, ada za shule, na gharama nyingine.Hapo panachekesha hasa pale mwanaume anapolazimisha atambuliwe kuwa yeye ndio kichwa cha familia lakini hapo hapo haonyeshi uongozi wa aina yoyote. Hii inakera sana.
3. Wivu uliovuka mipaka
Wivu ni kiashiria kizuri cha kupendwa sikatai na huwa Unanogesha mapenzi sana.Hakuna raha mwanamke anaipata kama pale mpenzi wake anapoonyesha wivu. Inachekesha kidogo lakini.Wivu wa mpenzi pale hajakuoa na wivu wa mume wakati mwingine huleta ladha tofauti kabisa. Mpenzi wako akiwa na wivu huvumilika na kufurahisha.Wivu wa mume wakati mwingine huwa kero. Kero hasa pale unapoelekezwa kukupunguzia tija kikazi, unapoelekezwa kukupunguzia kujiamini. Mume anapoonyesha wivu unaolekea katika unyanyasaji hapa hauchochei penzi bali huchochea chuki na kuweka ufa katika uhusiano.
nitarudi tena.... endelezeni kina dada/mama...
kina kaka/baba mnaruhusiwa kuchangia pia...