Kero za Muungano na utatuzi wake - Sehemu ya Pili

Acha kudaganya umma fi la u n i wewe hakuna Mtaganyika anautaka huu muungano kwa asilimia ulizodaganya hapa, muungano huu upo kwa maslahi ya wanasiasa wa pande zote {bara na visiwani} lakini sikwa wananchi wa kawaida. Ukitaka kuamini huu utafki feki uliouleta hata basi waitishe kura ya maoni. Ushaona nchi moja ina TRA mbili kila moja ikipuyaga kivyake. Muungano huu ni kifungo kisicho na haki hata kidogo.
 
Kwa nini tusiseme kuwa huo utafiti uko biased? Yaani watanzania 45 mil ukaulize 2,400 mbona sample size ni ndogo sana wala msianze kutuuzia mapendekezo yenu kwa kuyaremba kuwa mmefanya utafiti. Sana sana mmepita sehemu mnazojua mtapata majibu mnayoyataka
Katika tafiti za ovyo ambazo nishazisoma hii ni namba O kabla ya 1! Siku moja waitishwe wabara walioko Zanzibar waulizwe kama huu muungano wanautaka au la,naamini watakachokiomba ni msaada wa kusafirishwa kurundi bara kwani huko wanaishi kwa kujipendekeza hasa kwa viongozi wa kisiasa hasa CUF na CCM na kusilimishwa.
 
Wakuu,
Ufafanuzi kidogo kuhusu utafiti. Udogo wa sample sio issue kabisa kwenye utafiti wa namna hii. In fact kura za maoni nyingi hutumia sample ya watu 1000 plus or minus hata kwa nchi kubwa kama USA. Muhimu hapo ni jinsi ulivyoipata hiyo sample yako. Lengo la utafiti wa namna hii ni kukusanya kila aina za perceptions ambazo zipo kwenye jamii. Kwahiyo kama kuna perceptions N basi unaandaa sample ambayo inaendana na hizo perceptions. Kadri unavyoongeza ukubwa wa sample na gharama ya utafiti inaongezela lakini kwa faida ndogo sana yaani quality ya utaifiti haiongezeki. Muhimu tu ni kuhakikisha usiziache baadhi ya perceptions nje ya utafiti wako. Lazima watu unaowachagua kwenye utafiti wawakilishe makundi yote ya hizo perceptions N.

Kwahiyo, kwa kifupi sample ya watu 2400 kwenye nchi ya watu milioni 40 ni sample tosha kabisa na kila kitu kingine kikifanywa vizuri ina uwezo kabisa wa kuleta maoni ambayo yanawakilisha watu milioni 40.

Pia kuna mtu anajumlisha 88 +23 na kupata asilimia 111. Hapana wakuu, mambo ya statistics hayaendi hivyo. Hizo sio hesabu za moja jumlisha moja ukapata mbili. Kinachofanyika ni kwamba kunakuwa na maoni yanayonyumbulishwa zaidi.

kwa mfano asilimia 60 wanataka muungano usivunjwe na uendeleekama ulivyo. Katika asilimia 40 ambayo haikubaliani na muungano kuendelea ulivyo kunaweza kuwa na asilia 10 wanasema usivunjwe ila ufanyiwe marekebisho. Unavyotoa summary yako lazima hapo utasema asilimia 70 wanataka muungano usivunjwe. Hapo hapo pia unaweza kusema asilimia 40 wapinga muungano. Ukiingia kwenye hesabu za kujumlisha na kutoa utasema mbona ni asilimia 110? Lakini ukipewa utafiti kamili utagundua mgawanyo wa hayo makundi.

Ni ngumu sana kwa JF kujadili mambo ya utafiti maana watu wengi hawajui jinsi utafiti unavyofanywa na ndio maana kila mara hili suala la sample ndogo linajitokeza. Huu utafiti unaweza kuwa fake kwasababu ya kushindwa kutumia vigezo vyote vya utafiti. Lakini udogo wa sample sio issue kabisa.

Ni hayo tu kwa wale wanaotaka kujifunza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom