Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,852
Unaona hata hawa jamaa wanazungumzia utumwa! Historia ya utumwa haikwepeki. Wanapozungumzia mauaji ya waarabu wakati wa mapinduzi ni lazima muangalie pia kwa nini palikuwa na chuki kiasi hicho. Si kutokana na simulizi tu bali ni kutokana na vitendo walivyokuwa wakifanyiwa watu weusi. Utumwa haukuwa lele mama.Ukumbuke vile vile hata baada ya BIASHARA ya utumwa kupigwa marufuku, utumwa ulikuwa halali Zanzibar! Hao wanaosifia mchanyiko wa damu Zanzibar inabidi wazungumzie ilipatikana vipi. Wazungumzie upendeleo waliopewa wao kuoa lakini kutoolewa. Unadhani kwa nini Karume mara baada ya kupindua alikimbilia kuoa muarabu na kuhalalisha waarabu na wahindi kuolewa na watu weusi! Ingekuwa ni mazoea pasingekuwa na haja ya kufanya hivyo. Utawala wa Sultan haukuwa benign kama mnavyotaka kutuambia. Maovu mengi yalifanyika. Kwa vile umejiita mtu mweusi nenda kwa watu weusi wenzako ukawaulize ilivyokuwa na watakuambia. Ni sehemu ya historia yako na haikwepeki.
Amandla......