Kero za Muungano na utatuzi wake - Sehemu ya Pili

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Ni muda muafaka kupeleka hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika.

Kutokana na hali na upepo wa kisiasa, natumaini kwa wabunge wa ‘Tanganyika' huu ni Muda muafaka wa kupeleka hoja ya kubadili katiba na kuanzisha serikali ya Tanganyika na kuanzisha vifungu vya kulinda maliasili za watanganyika .

That said, Rais JM Kikwete apewe muda wa kuongoza serikali ya Muungano [URT] kwa muda wa miaka miwili kusimamia mchakato wa kuanzisha Katiba mpya ya Tanzania ambayo itakuwa na maudhui ya kuanzisha Federal State.

Hii imekaaje?
 
Yaani humu ndani tumo WATANZANIA 84 tu!!!!!

Wengine wote ni Watanganyika na Wazanzibari...du

Sasa kwa sisi wenye kuota ndoto ya Afrika moja kazi tunayo. Hii inaniambia nina miaka kati ya arobaini 20 na 30 tu (kama nitafikia muda wa kustaafu maisha ya kuhangaika) kutimiza ndoto ya kuligeuza jangwa la SAHARA kuwa msitu wa KONGO...

omarilyas
 
Kinachopungua katika muungano huu wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ni kukosekana kwa utashi wa kweli katika kutafuta suluhu ya ya kweli ya matatizo yaliyopo. Jambo hata liwe gumu kiasi gani namna bora ya kutafuta suluhu ni kuongea na sio kuukwepa ukweli.

Binafsi nakubaliana na wale wote wanaoamini kwamba hakuna suluhu bila mazungumzo. Hata yale mambo ambayo yalikuwa hayafikiriwi kwamba yanawezekana imeonyesha kwamba yanawezekana kama mazungumzo kati ya maalim na Karume. Hivyo kwa suala lolote ambalo ni tete suluhu ni mazungumzo tu, vinginevyo tunajidanganya na kupoteza muda bure tukiamini kwamba tunaboresha kumbe ndio tunaharibu mambo.

Ni lazima udhaifu wa muungano kama upo uwekwe hadharani watu tujadili na tuone suluhu ya kweli ninini, vinginevyo hatufiki popote itaonekana kwamba wote tulio ndani ya muungano huu kwamba ni wahuni. Kumbe suala hili linajitokeza kwa watu (viongozi) kuufumbia macho ukweli. Tubadilike jamani, huu sio wakati wa kuficha ficha mambo hatutafika popote!!
 
not a bad idea at all considering the zanzibaris seems to want to part away with us may b its time to give the idea a serious thought afterall there is nothing major that we will loose by parting away with the plonkers(zanzibaris)
 
naungana nawe, tunahitaji nembo yetu ya taifa la Tanganyika huru, Bendera ya Tanganyika, na kawimbo ketu ka taifa....Mungu bariki wote wenye wazo hili, maana wanung'unikaji wa upande wa pili wanaboa.
 
Wakati wa mjadala wa suala la kuongezewa muda Rais Karume au la ili aongoze bila ridhaa ya wananchi kama Katiba ya Zanzibar inavyotaka, kuna baadhi ya watu walieleza kwamba mambo ya Zanzibar hayawahusu wasiokuwa Wazanzibari na waachwe washughulikie mambo yao!

Kauli hizo zimetolewa bila kujali kama Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano au la.

Lakini Wazanzibari wamekuwa wakitaka Serikali ya Tanganyika irudishwe bila kujali kuwa Serikali hiyo haiwahusu au la!

Ushauri wangu ni kwamba Wazenj wawaachie Watanganyika waamue kama wanataka kuwa na Serikali au la!
 
Sam,

Inasikitisha sana kusoma huo mswada unaotegemewa kufanywa sheria katika siku za usoni , swali langu mimi ni moja tuu Watanzania ni nani aliyetuloga ? Kwa nini atufikirii kabla ya kufanya maamuzi ?

Kweli , kuna haja ya kuwa rocket scientist kujua ya kuwa huo mswada ni ujinga na ni kuwatukana wazalendo ? Yaani mapato ya madini yagawanywe katika uwiano wa 60% bara na 40 % zanzibar ....Ni vigezo gani wametumia kupata hizi figure ? kwanza zanzibar ina population ya watu wangapi .

Sam , naona utakuwa unaumiza kichwa tuu . Hawa viongozi awajali watu wa kawaida wanachodai ni masilahi yao binafsi ! siasa za bongo ni upotevu wa muda kwani wananchi wako so dormant na mara nyingi wanaishia kulalamika tuu .kikifika kipindi cha uchaguzi wanapitishiwa mswada wa kuwapa pilau " wanahongwa pilau " then wanawachagua kwa asilimia 80%.

pole sana kaka,
haya mambo ni mazito. chama cha mapinduzi kimefanikiwa sana kuwatia watanzania , woga, upumbavu , njaa na ujinga. kwahiyo kila kinachofanywa katika tanzania ni kwa maslahi ya kundi fulani la watu.
tanzania sio nchi ya kuwa mpaka sasa watu wanahangaika na huduma muhimu kama maji na umeme. kwahiyo , watanzania wamefanywa kuwa waone hali hii iko kila nchi nyengine.
mimi niko nje ya tanzania na hapa nilipo naangalia mara kwa documentary on tv ... maisha ya mtanzania. machozi yananitoka. kwasababu hawa watu hapa wanashangaa kuona umasikini wa watu katika nchi ambayo inautajiri wakutosha...
baadhi ya watu wanawaona waZanzibari kama wakorofi fulani, lakini mimi nawaona kama watu ambao wameamka na wanadai haki zao. muungano hawautaki, bali unalazimiswa na bara. kwahiyo muungano ukivunjika zanzibar watasonga mbele haraka. ndio maana bara kutumia ccm kulazimisha muungano. ndio maana kila kitu cha muungano kinafichwa au inafanywa siri.
kwanini isipigwe kura ya maoni, watanzania wote wakatoa uamuzi. muungano ndio unazuwia maendeleo ya zanzibar na bara.
mimi sita muungano, na kama lazima basi uwe wa serikali tatu.
 
Ni muda muafaka kupeleka hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika.
Kutokana na hali na upepo wa kisiasa, natumaini kwa wabunge wa ‘Tanganyika’ huu ni Muda muafaka wa kupeleka hoja ya kubadili katiba na kuanzisha serikali ya Tanganyika na kuanzisha vifungu vya kulinda maliasili za watanganyika . That said, Rais JM Kikwete apewe muda wa kuongoza serikali ya Muungano [URT] kwa muda wa miaka miwili kusimamia mchakato wa kuanzisha Katiba mpya ya Tanzania ambayo itakuwa na maudhui ya kuanzisha Federal State. Hii imekaaje?

vizuri... kama itakuwa naamini zanzibar watafanya holiday wiki moja. kwasababu ule mnyororo wa kuburuzwa utakua umekatika. kwahiyo kila mtu atangalia mpango wake. free zanzibar , free tanganyika.
 
Ni muda muafaka kupeleka hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika.
Kutokana na hali na upepo wa kisiasa, natumaini kwa wabunge wa ‘Tanganyika' huu ni Muda muafaka wa kupeleka hoja ya kubadili katiba na kuanzisha serikali ya Tanganyika na kuanzisha vifungu vya kulinda maliasili za watanganyika . That said, Rais JM Kikwete apewe muda wa kuongoza serikali ya Muungano [URT] kwa muda wa miaka miwili kusimamia mchakato wa kuanzisha Katiba mpya ya Tanzania ambayo itakuwa na maudhui ya kuanzisha Federal State. Hii imekaaje?
As long as Zanzibar and Pemba will remain the 24th and 25th regions of tanzania or how about cutting down the 127 districts of Tanzania to 119 districts absorbing the 10 districts in zanzibar and unguja? :D I have no problem at all we can even be called Pemba country! if not Wete i hope it will sooth your heart!
 
Wakati wa mjadala wa suala la kuongezewa muda Rais Karume au la ili aongoze bila ridhaa ya wananchi kama Katiba ya Zanzibar inavyotaka, kuna baadhi ya watu walieleza kwamba mambo ya Zanzibar hayawahusu wasiokuwa Wazanzibari na waachwe washughulikie mambo yao!

Kauli hizo zimetolewa bila kujali kama Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano au la.

Lakini Wazanzibari wamekuwa wakitaka Serikali ya Tanganyika irudishwe bila kujali kuwa Serikali hiyo haiwahusu au la!

Ushauri wangu ni kwamba Wazenj wawaachie Watanganyika waamue kama wanataka kuwa na Serikali au la!

wazanzibar, wanataka kuwepo kwa serikali ya tanganyika. kwasababu na wao watakua huru na serikali ya zanzibar .it is a simlpe logic. kwahiyo , kama wewe na wenzio mntaka lazima kuwepo na muungano, iundwe serikali nyengine ya muungano. therefore, kutakua na serikali tatu.
 
wazanzibar, wanataka kuwepo kwa serikali ya tanganyika. kwasababu na wao watakua huru na serikali ya zanzibar .it is a simlpe logoc. kwahiyo , kama wewe na wenzio mntaka lazima kuwepo na muungano, iundwe serikali nyengine ya muungano. therefore, kutakua na serikali tatu.

Alaaa, kumbe ndio sababu ya kuingilia mambo yasiyowahusu?
 
..wa-Zenj walumbane hukohuko kwao.


..watuache wa-Tanganyika tubanane na mapambano yetu ya ufisadi.


..kila siku wa-Zenj ni kupiga makelele kwenye vyombo vya habari vya Tanganyika kwa mambo yasiyonafaida wala kutuhusu.


..hivi Zenj hakuna waandishi wa habari mpaka RAZA aje kufanyia press conference yake Dar-Es-Salaam?



Raza: Mjadala serikali ya mseto ufungwe

Mshauri wa zamani wa masuala ya michezo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Mohamed Raza, ametaka mjadala uliopamba moto kuhusu hoja ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo ufungwe.
Amesema badala ya kuendelea kujadili hoja hiyo, ambayo imeshazikwa, nguvu zote zinatakiwa hivi sasa zielekezwe bungeni, mjini Dodoma katika mjadala unaohusu ufisadi wa mkataba tata wa Kampuni ya Richmond Development LLC ya Marekani na ule wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira.
Raza, ambaye ni mfanyabiashara maarufu, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana na kusisitiza kwamba, amesema hayo akitoa fikra zake katika mjadala unaoendelea hivi sasa Zanzibar akiwa kama mkereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema mjadala kuhusu hoja ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, inapaswa kufungwa kwa vile imeshazikwa na Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapiunduzi (CCM) Zanzibar, baada ya kukutana visiwani humo, Jumapili wiki iliyopita.
Raza alisema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wanaong’ang’ania mjadala huo, hawana nia njema, bali lengo lao ni kutaka tu ushindi wa mteremko katika uchaguzi, baada ya kuona hawapati kitu majimboni kwao kwa vile wamefilisika kisiasa.
Alisema kikao hicho cha kamati maalum ya NEC Zanzibar, kilichohudhuriwa na watu wenye hekima na busara, akiwamo Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, kilipitisha azimio linalotaka maazimio ya Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, yaliyopitishwa katika mkutano wake wa Butiama, mwaka juzi, yaheshimiwe.
Miongoni mwa maazimio hayo ya NEC Butiama, ni pamoja na kutaka suala la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, lirejeshwe kwa wananchi kupitia kura ya maoni na kusema kwamba, anaamini wawakili wa CCM watatumia fursa ya leo kwenye Baraza la Wawakilishi kulitolea ufafanuzi azimio hilo ili Wazanzibari waelekee kwenye uchaguzi wa amani na utulivu.
“Kwa hivyo, mjadala huu tumeufunga...Sababu Wazanzibari wameyumba, hawajui wakamate wapi. Kumekuwa na siasa za Abunuwasi na kasumba mitaani. Mjadala sasa hivi tuelekeze kwenye ufisadi bungeni Dodoma. Tupeleke nguvu zetu huko, kwani huko kuna Richmond na Kiwira…Naomba maazimio yale yaheshimike kwani yalikuwa ya hekima na busara, masuala yote ikiwamo serikali ya mseto yarejeshwe kwa wananchi. Hakuna mwakilishi aliyetishwa. Kila chama kina utaratibu na maadili yake. ukiona njia kainamisha mgongo ujue kabeba mzigo si wake,” alisema Raza.
“Tuwaombee (wabunge) ili tujue mbivu na mbichi, maana tumeshaanza kusikia kuwa baadhi ya mawaziri wameanza kukimbia bungeni wanasema wana dharura. Bora tule mihogo na viazi kuliko kutawaliwa na watu wachache. Ni imani yangu kamati yamzee Mwinyi itatupa afueni,” aliongeza.
Alisema hivi karibuni walikutana Ikulu na Rais Karume na kuwahakikishia kwamba, katika mazungumzo ya faragha na Maalim Seif, hakukuwa na suala lingine lolote linalohusu serikali ya mseto, bali mazungumzo yao yalihusu amani na utulivu visiwani Zanzibar.
“Kama kuna lingine limekuja kwenye chama na kwenye kamati maalum sababu rais hafanyi kazi peke yake na wala hakuwa mgombea binafsi, bali anatoka CCM. Kina Mwinyi na Dk. Salmin Amour huko nyuma walitakiwa waongezewe muda, lakini katiba haikuruhusu. Na hata katiba si msahafu, lakini itafuata ridhaa ya wananchi, kwa faida ya wananchi. Sehemu zote inahitajika nia,” alisema Raza.
Alimpongeza Rais Karume kwa kauli yake kwamba, hatoendelea tena kuwapo madarakani na kusema kwamba, kauli kama hiyo aliishaitamka zaidi ya mara tatu.
Awali, Raza alimpongeza Rais Karume, Maalim Seif kwa kukutana na kufikia maridhiano ya kumaliza uhasama na chuki miongoni mwa Wazanzibari visiwani humo na kumtambua Rais Karume na kusema kwamba, hatua hiyo imebadili hali ya hewa visiwani humo na kuleta faraja si kwa Wazanzibari tu, bali kwa Tanzania, mabalozi na kwa dunia nzima kwani wote wanazungumzia amani na utulivu.
 
We dogo vipi! mwisho mtatesema wazenj wasiingie humu JF kwa kuwa inamilikiwa na wabara!
 
Lamba said:
We dogo vipi! mwisho mtatesema wazenj wasiingie humu JF kwa kuwa inamilikiwa na wabara!

Lamba,

..wa-Tanganyika haturuhusiwi kujiunga na kuchangia kule Zanzinet. au huna habari hizo??

..kwa kuanza basi nenda kawashawishi Zanzinet waturuhusu wa-Tanganyika kushiriki ktk mijadala yao.
 
Shadow,

..kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Federation siyo solution ya matatizo yetu.

..tatizo ni kwamba Zanzibar ni ndogo mno ku-avoid status ya junior partner ktk muungano wowote ule na Tanganyika.

..pia wa-Zenj wamekataa kata kata kuchukua identity ya u-Tanzania. wanapendelea kushikilia identity yao ya u-Zanzibari.

..sasa hivi wa-Tanganyika wana-finance shughuli zote za serikali ya Muungano na bado wa-Zenj hawaishi kututukana na kutudharau. sasa juu ya hayo mnataka tubebe mzigo wa serikali ya Tanganyika na ile ya federation???

NB:

..SOLUTION NI KUVUNJA MUUNGANO TU.
 
Natamani kulia. Nachukia sana uzanzibari na uzanzibara. Let zanzibar iwe mkoa.

Zanzibar iwe mkoa? wewe ndio utalia sana kwa sababu ya ujinga wako

Zanzibar ni kama Kenya, Uganda, Burundi etc itakuwaje mkoa?

Tuwaheshimu wazanzibar ndio tutapata kuungana vizuri kwa watu wenye mawazo kama yako matatizo yatakuwepo milele.
 
huu ni muungano ni wa kihuni na ndiyo maana hata sherehe zake husherehekewa na serikali tu kwa vile hauna tija kwa wananchi wa pande zote mbili hivyo wananchi hawauthamini, we uliona wapi mkoa na nchi kamili vikatengeneza jamhuri ya muunngano, wazanzibar waendelee na karafuu na tende na siye wabara tuendelee na kahawa, chai, na mengineyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom