Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Tunatoa kwa sababu tunaona aibu tunapoombwa . Inabidi tuwaelimishe wanoomba kwanza waone aibu ya kuomba michango ndipo hali hii itaisha maana duh. Nilikuwa na kadi
15 za harusi kwa mwezi Nov. na Dec. Nilitoa mchango 3 na zote nikasusa kwenda kuonyesha kuunga mkono hoja hii.
 
Pia ukiona mtu hujawasiliana nae kwa muda mrefu akikupigia usipokee simu hio ni KADI ya mchango
 
Kama ni utamaduni wa kipuuzi kwanini mnaendelea kuchanga mkiletewa hizo kadi za michango
 
Vyote hivi vimeanzia kwetu huku uchagani,ukijidai una fedha zako ukagoma kuwachangisha basi unasusiwa harusi.
Inashangaza mzaramo alipokuwa anatepembea kwa mdundiko alionekana mshamba wakati leo hii kuna matarumbeta yanayopiga style ile ile.
Mimi huwa sichangi na kwenye harusi yangu sitachangisha.
Naunga mkono hoja.

Sisi tulienda kwa mchungaji na wasimamizi wetu tukafunga ndoa bila mchango wa mtu wala sherehe miaka kumi sasa imepita na tunadunda bila wasiwasi. Ila kwa wakati ule watu walinishangaa sana na mpaka sasa nikiwaeleza watu hawaniamini.
 
Sharing is caring
kugawana ni kujali

Kwa nini tunagawana kwenye harusi na misiba tu? Kwa nini hatugawani kwenye mambo mengine ya maana kama elimu na afya za watu ambao wakifa tu tunachangishana pesa za kuwashonea sare ya kuwazika wakati tayari wameshaondoka?. Huu ni ubatili tu na kulishana upepo.
 
Watu wepesi sana kuchangia minuso mikubwa mikubwa waombe wakuchangie kwenye ugonjwa unatolewa patupu mgonjwa akifa utawaona kwenye mazishi wanavyo toa michango mikubwa mikubwa
 
Kwa nini tunagawana kwenye harusi na misiba tu? Kwa nini hatugawani kwenye mambo mengine ya maana kama elimu na afya za watu ambao wakifa tu tunachangishana pesa za kuwashonea sare ya kuwazika wakati tayari wameshaondoka?. Huu ni ubatili tu na kulishana upepo.

Hata huko tunagawana pia...au wewe ukiombwa kumchangia mtu ada unagoma?
 
Mimi kwa ufahamu wangu mtu akitaka kuoa, he works hard and put saving for it and its not that you're expecting other people to pay for your expenses. If you can not meet the basic needs for the wedding, then you're not ready for it. Achane kuiga mambo msiyoyaweza au msiyokuwa na uwezo nao. Back in old days, harusi it remains the cost of the bride and groom and relative will help with whatever they can afford na si kuwa mtu anakuwekea kiwango. Na mambo yalikuwa safi tu, the most important is the blessing of the marriage from God but not bless ya kuwalisha watu 100 au 200 ambao hata siwajui, its totally insane.

You have said it all MadameX. Mimi ni mfano hai wa ndoa bila mchango wa mtu wala sherehe za kipumbavu. Ninavyoongea nina zaidi ya miaka kumi kwenye ndoa hiyo na tuna watoto wawili. Leo hii nikipatiwa nafasi ya kufanya harusi nitarudia kama ileile sana sana nitaangalia maeneo ya kupunguza gharama zaidi ili nipate pesa ya school fees za watoto.
 
Kama ni utamaduni wa kipuuzi kwanini mnaendelea kuchanga mkiletewa hizo kadi za michango
Mimi huwa sichangi ila mimi ni mtu wa kushare na kusaidiana (jamaa yangu akipata sherehe uchangia) zawadi, au kufanikisha issue ile kama ni mtu wa karibu huwa ninamsaidia kwa kila niwezacho...... issue sasa ni kwamba hata mtu si jamaa wa karibu yangu sababu jamaa yangu wa karibu anamjua.. basi na mimi taletewa kadi (hizi kadi zenyewe unakuta zimecost 200,000/=) je jamani huu kama si ulimbukeni ni nini??? Mimi ningechanga kila harusi kama tungejuwa tunawachangia maharusi kununua nyumba au vitu vya kuanzia maisha
 
kadi ya mchango wa harusi sio invoice...u can contribute nothing or anything u like...ndo utamaduni wetu huo tuendelee nao tu
 
mimi huwa sichangi ila mimi ni mtu wa kushare na kusaidiana (jamaa yangu akipata sherehe uchangia) zawadi, au kufanikisha issue ile kama ni mtu wa karibu huwa ninamsaidia kwa kila niwezacho...... Issue sasa ni kwamba hata mtu si jamaa wa karibu yangu sababu jamaa yangu wa karibu anamjua.. Basi na mimi taletewa kadi (hizi kadi zenyewe unakuta zimecost 200,000/=) je jamani huu kama si ulimbukeni ni nini??? Mimi ningechanga kila harusi kama tungejuwa tunawachangia maharusi kununua nyumba au vitu vya kuanzia maisha

sasa vor ishu ni jamaa wako wa karibu au ni kuchanga maana hata kama ni jamaa yako wa karibu still umemchangia
 
mi niliacha jamani, mwanzoni ilikuwa kama utani utani tu nawaambia watu sichangii lakini nimeweza kweli hata ofisini mtu akija na kadi namwambia tu hapo hapo kuwa samahani mi huwa sichangii harusi na hata harusi yangu sintafanya sherehe. hiyo ni baada ya kuzidiwa na michango na kukosana na watu kibao kisa sijachangua harusi zao "gadem"
 
Hata huko tunagawana pia...au wewe ukiombwa kumchangia mtu ada unagoma?

Kwenye elimu mimi ninasomesha watoto kwa kuwalipia ada shule. Wengine nawachukua na kukaa nao nyumbani kwangu ili kuwasaidia siyo shule tu bali hata malazi, chakula na mavazi.

Kwenye misiba huwa ninachangia kwa wafiwa ili kuwasadia gharama za mazishi. Lakini napo siku hizi naona uzalendo unaelekea kunishinda kwani watu wanataka kuonyesha ufahari zaidi ya kufanya shughuli ya msingi ya kumfukia marehemu chini ya ardhi. Sijawahi kuchangia wala kushona sare ya msiba na sitakaa nifanye hivyo.
 
Yes mkuu...kote huko ni kugawana kwa kujali...unajua haya mambo lazima uyatazame kwenye angle tofauti tofauti sana...public services wengine wako reluctant kuchanga kwakuwa wanadhani tayari wanachangia through kodi...wengine wanasaidia ndugu au wale walio kwenye wakati mgumu...lakini kuchangia harusi ni hiari, mtu anaweza kuchanga au akaacha, sio kusema eti ni utamaduni wa kipuuzi...ni hiari sio lazima
 
sasa vor ishu ni jamaa wako wa karibu au ni kuchanga maana hata kama ni jamaa yako wa karibu still umemchangia

Issue ni kufanya kwamba hiki ni kitu cha lazima...... binadamu tunasaidiana kila siku na kwenye kila jambo... lakini sasa harusi imekuwa ina viingilio... na kiingilio ni michango... mimi kama pesa zipo siitaji kuombwa nitatoa kulingana na uwezo wangu wala singoji kukumbushwa au kuombwa na mara nyingi culture zetu ni kupeleka zawadi siku ya siku....

sasa mimi kama ninaoa na rafiki zangu hawana pesa za michango je wasije kwenye harusi???? bali waje wale watu hata ambao siwajui kwa sababu wana pesa na wanawajua wazazi wangu???? Hivi mimi nikifanya harusi kwa uwezo wangu mdogo watu walaka kidogo je huko sio kusherekea...... ???
 
badilisha heading ya hii thread tafadhali
 
Back
Top Bottom