Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

View attachment 235905

Kwa kweli michango ya harusi, sijui kitchen Party, Bag party, Send off party na kadhalika imekuwa too much. Unakuta mtu unakuwa na kadi za kudai michango hadi zaidi ya kumi kwa wakati moja. Tabu ya nyongeza ni kwamba viwango vinavyotegemewa ni vya juu. Tutafika?

Je, haijafika mahali wanajamii ya Tanzania tukapunguza madoido na gharama za shughuli hizi?

==============

Katika kumbukumbu zangu mimi, Harusi mtu ulikuwa unafanya kwa uwezo wako, unaita marafiki zako na ndugu mnasherekea hicho kilichopo.

Sasa mtu anakuletea Kadi tena ina kiwango na Watu hawakuchangii sababu wanakupenda ni kama wanakukopesha kwamba na wao siku yao ikifika na wewe utachanga.

Michango Inafika mpaka mamilioni ya pesa watu wanakuja wanakunywa na kula wewe na mwenza wako mnaenda kuanza maisha (wengine hata nyumba hamna) na deni la watu kama mia moja waliokuchangia ambao na wewe inabidi uwachangie.

HIVI NI MIMI TU NINAYEONA KUWA HUU NI UPUUZI NA UJINGA AU KUNA YEYOTE ANAYENIUNGA MKONO?

Jamani hivi kuchangia harusi sasa imekuwa lazima?

Nahisi sasa harusi zinatuletea umasikini, yani mtanzania wa kawaida nina kadi tisa mpaka sasa.

Bado natafutwa na jamaa yangu mwingine, yani simu imejaa meseji za watu wanakumbushia michango.

Jamani hatuwezi kuwa na utaratibu mbadala kwenye hili swala? Tupungiziane stress.

Halafu na hii tabia ya mtu anakutumia tu ujumbe uje siku fulani mahala fulani kuna kikao cha harusi, kumbe kesha kuweka kwenye kamati ya harusi we bila kujua afu ukifika wanaweka kiwango cha kila mwanakamati kutoa.

Nadhani tuhitaji mbadala wa hili.

Napata kadi za kuchangia harusi karibu kila mwezi naletewa karibu kadi 3, @50,000 approximately =150 , 000 .

Haya majanga sana ,mshahara wangu 550,000 , which means 30% michango harusi ,Ninaacha haya mambo ,mimi mwenyewe sitafanya hiyo mambo, yaani kila weekend tupo busy kuchangisha harusi.

Kama tunataka kutokomeza umasikini na wakati tunatiana umasikini ,siwezi tena.

Jamani kama huna uwezo usisumbue watu bwana ,funga ndoa ya kawaida tuache mambo ya kuiga.
Ni kawaida kwa jamii yoyote duniani kuoa ama kuolewa na hasa kwa binadamu aliyekamilika. Kimsingi kuoa ni jambo la heri kwa mtu kupata mwenzi. Na ndugu jamaa na marafiki kuchangia kwa mawazo mali na misaada mingine ya kijamii ili kufanikisha shughuli hiyo kukamilika.

Hata hivyo uchangiaji huu umekuwa wa kiholela mno, kwani waoaji na wanaoolewa ni vyema wakawa na utaratibu mzuri wa kugawa kadi hizo. Nasema hivi kwa sababu kuwa mgawa kadi anapaswa kufanya mawasiliano na mtu anayetaka ampe kadi kwa ajili ya kumchangia mchango huo. badala ya kuzigawa kadi hizo pasipo hiari ya mchangiaji, maana mgaw kadi unashangaa anakuletea kadi, ama anaibwaga mezani kwako kama ni ofisin au anawaachia watoto kama ni nyumbani.

Ombi langu kwa waoaji wote fanyeni mawasiliano kabla ya kugawa kadi maana sasa zimekuwa kero kiasi kwamba ndani ya mwezi mmoja unaweza kugawiwa kadi zisizopungua kumi na wote wantaka mchango usiopungua elfu hamsini. kwa namna hii hatuwezi kwenda kabisa.

Hata hivyo niwaombe watanzaia wenzangu tunahitaji kubadilika ili mitizamo yetu isilenge zaidi katika uchangiaji wa harusi, tunahitaji kuchangia zaidi katika elimu kwani kuna vijana wetu hawana hata dwati la kukalia, yatima, wajane na wenine wengi wenye mahitaji badala ya kuchangia harusi.

Kufanya harusi kubwa katika kumbi kubwa zenye kugharimu mamilion ya shilingi za kazi gani, kwani hazina tija kwa maendeleo ya taifa hili ambalo wananchi wake wako katiak wimbi la umaskini mkubwa.


Sitoi tena Michango ya Harusi

BAADA ya matukio ya harusi ya Jumamosi iliyopita natoa onyo ole wake atakayeniomba mchango wa harusi, sitaki utani. Labda kwanza nikueleze jinsi tulivyopata misukosuko sana kwenye uchangiaji wa ile harusi, maana siku hizi hakuna pa kukimbilia, kila asubuhi unaamshwa saa kumi na mbili na meseji kwenye simu;

"Ndugu, rafiki na jamaa wa familia ya Pingapinga inakukumbusha kuwa harusi ya mtoto wao imekaribia hivyo mchango wako unahitajika", baada ya wiki meseji huwa kali zaidi;"Siku zinaisha kwa nini hautoi mchango, unajua familia ya Pingapinga ina shughuli ya harusi ya mtoto wao, toa upesi au la usitulaumu."

Basi hizi meseji zilikuwa nyingi kuliko zile za kampuni yangu ya simu inayobuni namna ya kunitoa mkwanja kila wiki. Hatimaye nikatoa faini, maana nisiite mchango, maana mchango haulazimishwi.

Sasa Jumamosi ndiyo ikawa siku ya harusi, kadi nililetewa mapema , nikahakikisha koti langu la kuendea harusini nalicheki vizuri, maana haya makoti yanayokaa kabatini miezi ni muhimu kucheki vizuri maana unaweza kukuta panya kazalia kwenye mfuko halafu wakatimka kutoka kwenye makazi yao wakati uko katikati ya kucheza mduara wa harusi.


Kweli tukaingia ukumbini viti vilikuweko swafi, meza zimepambwa kwa maua na MC alitukaribisha kwa maneno mengi yaliyojaa vichekesho visivyochekesha, au vichekesho vingine vimesharudiwa na kila MC hapa mjini halafu akawa analazimisha watu wapige vigelegele!

Yote bure watu walikuwa wamenuna maana hakukuwepo na dalili ya hata chupa moja ya kinywaji, ila ahadi kibao zikawa zinatolewa na MC, mara ‘Roli la bia linakuja toka breweries, mara shampeni leo inatoka Ufaransa kwa helikopta."

Ghafla wahudumu waliovalia vikofia kichwani wakapitisha sambusa mojamoja na kinywaji round moja kwa kila mtu, wakisindikizwa na MC akituhamasisha tule tufurahi na bwana harusi. Kwa kweli hela yangu ikaanza kuniuma, kwanza nililazimishwa kulipa, halafu sioni chochote hawa jamaa vipi?

Wakati ukumbi mzima ukiwa umeendelea kununa utadhani kikao cha msiba, MC akatuambia eti bwana harusi ana machache kabla ya kutuaga kwenda kupumzika na mkewe. Pamoja na kisirani tulikuwa na hamu kumsikia mshenzi huyu anataka kusema nini.

Bwana harusi akasimama hata suti aliyovaa ilikuwa haijamkaa sawasawa, akakohoa kidogo akaanza, "Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu, kiukweli hapa nimepata mke mtulivu, mpole asiye na makeke, yaani najisikia nina bahati sana.

"Naomba niwashukuru wakwe zangu kwa kukubali kupokea robo tu ya mahari na kuruhusu ndoa hii ifanyike. Pia nishukuru kwa zawadi zao za kitanda, godoro, kabati na makochi asante sana.

"Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii, pia wafanyakazi wenzangu kwa zawadi yenu ya jiko la gesi. Namshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.

"Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama waliopika sambusa hizi tulizokula kwa kweli zilikuwa tamu sana, kwa kweli leo ni furaha tupu. "MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali kuwa mc wa shughuli hiikwakweli upo vizuri, aksante sanaaaaa!

Yaani inamaanisha ela zetu za mchango sijui zilinunua nini maana kila kitu almost kilikuwa bure.. mnaoowa karibuni poleni msinihesabu.

Ni kipindi kingine cha mwaka ambapo kila mwisho wa mwaka kadi za michango ya harusi inakuwa mingi, inakuaje mtu anataka kufanya sherehe kubwa na hana uwezo?

Kwanini usifanye hiyo harusi kutokana na uwezo wako ulionao, ni mpaka usumbue watu wakuchangie?

Tena kinachoudhi ni mtu ameshakaa na mke/mme na wana watoto anataka kupasha kiporo chake nae anataka afanye sherehe kubwa na anachangisha!!

Na kero nyingine mtu anakupa kadi ya mchango wa ndugu yake ambaye humjui.

Sijawahi kupewa au kuona mtu akichangisha kwa ajili ya maendeleo kama vile ada ya shule etc kama majirani zetu na harambee zao zenye maendeleo, sijui wenzangu mnafikiria vipi.
 
Uswahilini kuna mpaka michano ya birthday.....

Na siku hizi kuna michango ya kufunga kikao pia...
 
Nafikiri ingekuwa bomba tukachanga tukamwachia bwana na bibi harusi kama tume pata 4m tuwape waanzie maisha kama mtaji na harusi iishie pale tu wanapotoka kanisani au baada ya kufunga ndoa kwa waislam
 
Last month nimechangia harusi kama tatu ivi na mwezi huu kama 2 ivi natarajia kuchangia.
 
Nafikiri ingekuwa bomba tukachanga tukamwachia bwana na bibi harusi kama tume pata 4m tuwape waanzie maisha kama mtaji na harusi iishie pale tu wanapotoka kanisani au baada ya kufunga ndoa kwa waislam

hapo ndipo napenda wakenya, sherehe ni minor? better save for the maharusi to start new life!!
 
yote hii si hiyari mwisho wa siku? kuna anayelazimishwa?

sichangii kwa unafiki huku moyo ukiniuma, kama siwezi namwambi muhusika dhahiri kuwa sitaweza kukuchangia. na moyo wangu unakuwa na amani. kazi kwake kunielewa.
 
yote hii si hiyari mwisho wa siku? kuna anayelazimishwa?

sichangii kwa unafiki huku moyo ukiniuma, kama siwezi namwambi muhusika dhahiri kuwa sitaweza kukuchangia. na moyo wangu unakuwa na amani. kazi kwake kunielewa.


hata mimi nashangaa....kwani mmelazimishwa???kama hamuwezi/hampendi msichangie hizo harusi......
 
hata mimi nashangaa....kwani mmelazimishwa???kama hamuwezi/hampendi msichangie hizo harusi......

ndo unafiki huo PRONDO, mtu anakuchangia huku anakung'ong'a kwa nyuma. Ya nini ujitese mwenyewe kiasi hicho badala tu ya kuwa wazi na kuiweka huru nafsi yako!!!
 
sijawahi kuchangia harusi ya mtu ...............na kwa muelekeo niuonao, i never will.

kawaida hununua zawadi na kuipeleka na kwa wale walokuwa kama hujaleta mchango hatukupi kadi ya harusi .............huwa siendi harusi zao. I am not desperate kwenda shughulini kiasi cha kuwa nilazimishwe kiingilio
 
Michango hii tunaindekeza wenyewe. Ni jukumu la maharusi kujuwa pamoja na familia zao kujuwa how they will finance their wedding. Sioni ulazima wa kuchangia kila kitu. It's high time we killed this culture ambayo sjiui tumeitoa wapi.
 
sijawahi kuchangia harusi ya mtu ...............na kwa muelekeo niuonao, i never will.

kawaida hununua zawadi na kuipeleka na kwa wale walokuwa kama hujaleta mchango hatukupi kadi ya harusi .............huwa siendi harusi zao. I am not desperate kwenda shughulini kiasi cha kuwa nilazimishwe kiingilio

same here!!!
na ninamwambia mtu openly with a pure heart.

'kiingilio'' lol...........umenifurahisha hapo.
 
sijawahi kuchangia harusi ya mtu ...............na kwa muelekeo niuonao, i never will.

kawaida hununua zawadi na kuipeleka na kwa wale walokuwa kama hujaleta mchango hatukupi kadi ya harusi .............huwa siendi harusi zao. I am not desperate kwenda shughulini kiasi cha kuwa nilazimishwe kiingilio

Gaijin...umenimaliza kabisa, lol...mie hapa nilipo nina kadi za mpka ubatizo, yaani ndugu anabatiza mtoto anakutumia sms kuna kadi yako ya mchango n unaanzia 50 elfu,(hapo kwa ndugu ukisema huna unajua lawama zake tena) ubarikio m 3, wacha mbali haruc...huku nairobi cjawahi kuombwa mchango, ni zawadi yangu tu najiendea kwenye sherehe.
 
sasa sharti la kuwa toa 50000 ndio nikupe kadi si ni sawa na kiingilio tu!

mtu na afanye harusi kwa mujibu wa kipato chake .............kulazimisha wenziwe kumchangia ni tabia za ajabu tu. Hapo unamlazimisha na mtu kuvaa wenyewe wanaita theme color!

akanunue nguo ya rangi hiyo unayotaka na vikorombweza vyake na kisha alipe na kiingilio! .......mimi harusi za sare kwanza huwa siendi pia.....nimemaliza primary zamani, uniform basi kwa kweli
 
ndo unafiki huo PRONDO, mtu anakuchangia huku anakung'ong'a kwa nyuma. Ya nini ujitese mwenyewe kiasi hicho badala tu ya kuwa wazi na kuiweka huru nafsi yako!!!



mie sasa mpaka nimeamua kadi napokea kuchanga sichangi, hiyo ya kumwambia mtu live mwenzio imenishinda...hebu nipe maarifa coz kweli nikikaa vibaya na hii michango nitarudi njoro kulima kahawa.
 
mie sasa mpaka nimeamua kadi napokea kuchanga sichangi, hiyo ya kumwambia mtu live mwenzio imenishinda...hebu nipe maarifa coz kweli nikikaa vibaya na hii michango nitarudi njoro kulima kahawa.
dearest, sio rahisi na inataka moyo mgumu kama wangu. kiukweli mimi ni mtu wa misimamo, na I stand by my principles. So ukija na kadi yako nakwambia tu ukweli sasa how you take that ndo mi sijui (I can imagine though). ntakwambia vizuri kuwa mimi ningependa kuja kwenye harusi lakini huwa sichangi nanunua zawadi tu, so its at your discretion that unipe invitation card au lah!!!
 
heheh unachangia harusi halaf wiki 5 baada ya harusi bwanaharusi anafumaniwa gesti na kadada kachaf chafu ,ukifuatilia hela ya kuhonga kapata wapi? unagundua ni ile hela ya mchango ! kweli Bongo tambarare.
 
sasa sharti la kuwa toa 50000 ndio nikupe kadi si ni sawa na kiingilio tu!

mtu na afanye harusi kwa mujibu wa kipato chake .............kulazimisha wenziwe kumchangia ni tabia za ajabu tu. Hapo unamlazimisha na mtu kuvaa wenyewe wanaita theme color!

akanunue nguo ya rangi hiyo unayotaka na vikorombweza vyake na kisha alipe na kiingilio! .......mimi harusi za sare kwanza huwa siendi pia.....nimemaliza primary zamani, uniform basi kwa kweli

hahaaa G unanichekesha sana aisee lol!!

suala la kufanya harusi kulingana na kipato watu naona halijawaingia akilini bado. tena mi naona hii inakufanya uwe 'stress free' kabisa. Plan it they way you can afford it, usiwe mzigo kwako mwenyewe na kwa wengine pia!!!
 
Kwanza nachukia sherehe za kujitakia zisizokuwa na ubunifu wala mvuto. Matarumbeta yale yale, Ma MC wale wale, lugha zile zile, chakula kile kile, mapambo yale yale, ratiba ile ile, vinywaji vile vile, watu wale wale (sic), onesho lile lile kwa nini niende? Kwa msingi huo ukiongeza na mchango ndo umemalizia.Kiingilio wakati onesho ni lile lile?Inakuwa ngumu. Huwa natunza nguvu zangu kwa shughuli zisizo za kujitakia kama kuzika, kuangalia wagonjwa nk. Huko nitapeleka mchango hata kama sijaulizwa
 
Back
Top Bottom