Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mambo Jambo, Nov 12, 2009.

 1. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hii Kitu nilitaka kuipost hapa miezi kadhaa iliyopita sema nikasahau, leo kuna jamaa kanipigia anataka nimtumie dolali za mchango wa harusi ya binamu yake ambaye hata simjui wala sijawahi msikia.

  Tuendelee:-

  Wakuu hii kitu bado bongo ipo tena siku hizi ni project kubwa na za garama ya juu.

  Watu wanakutana kila wiki mara moja kwenye baadhi ya bar, wanakunywa na kusaza katika hivyo vikao vya maandalizi, vikao hivyo huchukua miezi miwili hadi mitatu. Na katika vikao hivyo watu hutoa ahadi ya kiasi cha fedha watakachotoa kwa ajili ya harasi, wanaume hutoa michango ya bachela parti na harusi kuu, na kina dada hutoa michango ya sendi off, bridoshawa, kichenipati, na harusi kuu.

  Kwa kifupi zoezi hili linakula hela nyingi sana, nimeambiwa sometimes you can be asked to contribute to more than 10 wedding a year, na ukitoa chini ya laki moja unaonekana mtu wa hovyo hovyo.

  Jamani ndugu zangu naombeni mwongozo mimi naona kama hii ni too much.

  Badala ya michango ya vikao vya harusi basi tuihamishie kwenye Elimu na Matibabu.

  MJ

  ====================   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hapa nilipo nna kadi sita ambazo harusi zote zinafanyika mwezi huu mwishoni na Disemba kila moja si chini ya alfu hamsini.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mimi kinachonishangaza ni huu utaratibu unaosema eti ukichangia elfu hamsini unakwenda na mpenzi wako,,,,lakini ukichangia elfu 25 unenda peke yako na kadi imeandikwa kabisa ni single.....

  Utasema concert....
  Wabongo bana.....

  Yaani huwezi kupata date ukaamua kwenda nae kwenye harusi
  kwa kuwa ulitoa mchango wa single.....aghhhh...

  Na bila mchango hualikwi....
   
 4. A

  AM_07 Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kinachokera zaidi mtu akiwa anakaribia kuoa/kulewa atakuwa karibu na wewe sana , akishapata mchango kwako ni kwaheri, i think kama tuchangie elimu na misiba tuu, anaehamua kuoa lywake.
   
 5. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Michango ni hiari ndugu zanguni hakuna anayekulazimisha kuchanga, na kama inakukela sana weka kabisa tangazo kama professor mmoja wa UDSM alikuwa ameandika kwenye mlango wa ofisi yake "MICHANGO YA HARUSI IMESITISHWA". Sidhani kama kuna mtu anakulazimisha kuchanga.

  Usipende kufanya kitu kinachokuumiza na kukukosesha amani kwa sababu ya kuogopa.

  Kama hutaki kuchangia sema no kama unachanga changa bila kinyongo ndo faida ya kuwa mwanajamii na kusaidiana!
   
 6. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mie nawashauri hii michango wanayokusanya badala ya kutumia hela zote kufanya harusi kubwa bora watumie hizi hela kuanzia maisha yao ya ndoa.ndoa nyingi nimeona harusi kubwa baada mwezi au miezi wana ndoa wanalalamika maisha magumu.Kwanini hii michango isitumiwe kwa manufaa zaidi baada ya ndoa kuliko siku ya ndoa?
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wajameni, hakuna kitu kero kama michango ya harusi kwa sasa... imepoteza maana!! Unakuta mtu anakupangia kabisa - wewe nimekupangia laki tatu tu!!! mtu income ya kawaida halafu anataka harusi ya mil 25 na ukiuliza kachanga ngapi anakwambi milioni moja!!! Very sick tradition... na mara nyingi unakuta mtu anaoa mkewe [meaning they are already living together or have already done everything wanandoa do!!

  Sasa subiri sijui chicken party, send-off, bachelors, inner party etc. etc.

  It is not a culture to embrace especially now that we need to put all our efforts in development
   
 8. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Budget ya Harusi siku hizi si chini ya mil.10,15, 20 ...wtf mimi naona tumezidi kuwa wapofu kula all that amount for one day tunachezea resorces...ukiangalia majirani zetu wanahitaji mtaji wa 50,000, 100,000, 200,000/- kuondokana na umaskini kwa biashara ya vitumbua, mandazi nk...
  tuna culture ya kutumia sana kwa ufahari..lol
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Huu ndio ukoma wa jamii yetu ya sasa... tunaweka vipaumbele sehemu zisizostahili!!!

  Kuna jamaa mmoja wa nje ya afrika kuna siku alisema maneno makali kidogo lakini he was right; alisema
  You africans are so amazing, you spend fortune on funerals but nothing on birth and that is where god bless you with a life; mothers and children deaths can be prevented.

  You also spend alot on celebrating weddings but you spend less on teaching about faithful marriage

  Ilikuwa kauli nzito lakini ina ukweli!!
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenena... ila hapo kwenye misiba mie ningependa tu-replace na kuchangia wagonjwa ili wapate huduma!!!
   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuna vitu siyo sahihi kwenye harusi zetu naamini tunaweza kufurahi bila kutumia hela nyingi sana mimi katika harusi item zifuatazo zinanikera..

  1. MC yaani mchekeshaji wa masaa tu 200,000 etc sioni mantiki kabisaaa kwanini asiye rafiki tu anaongoza kwa raha halafu bure kama vikao vyetu infomal sehemu zingine za starehe lol

  2. Mapambo ebwana wanakamua sijapata kuona bila sababu ya msingi

  3. Ukumbi weka kwenye uwanja wa wazi au nyumbani kwa mzee wako finito lol
   
 12. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani michango ya harusi tungebadilisha matumizi yake, badala ya kunywa na kula hizo mil 10, 15 au 20 kwa usiku mmoja, ni bora hiyo hela wakakabidhiwa bwana na bibi harusi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi au iwe kama mtaji wa biashara, utakuta mtu anafanya harusi ya mil 15 au 20, lakini hana kiwanja wala nyumba.. unakuta amepanga Sinza, Kijitonyama au mbezi beach, hehe hehe.....
  We need to change our attitudes and mindset!
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hivi huu utaratibu wa sherehe za arusi na patashika zake ni utamaduni wa kabila gani Tanzania? Au ni utamaduni wetu kama watanzania? Au ni utaratibu tuliouiga kutoka utamaduni wa watu gani?

  Nchi zilizo endelea kama hapa Marekani hachangishwi mtu, sherehe zinategemea uwezo.

  Kwa sababu ni hurka yetu kukopi kila kitu kutoka dunia ya kwanza hata kama ni ugonjwa au udhaifu, nauliza tena ni utamaduni wa nchi gani unafanana na utamaduni huu wa Tanzania wa kuchangishana fedha kwa hila za kishetani?

  Labda nyie mlioa miaka ya 196.. mtuambie. baba, mama, shangazi na wajomba zenu waliwachangisha akina nani ili nyie muozwe??

  Ili ndoa iitike ni lazima sherehe zake ziwe za kukata kwa Nyengo?

  Masikini ni yule atumiaye kipato asichokuwa nacho.

  Pendekezo langu kwenu nyie ambao hamjaoa ni hili.

  Achaneni na ununda huu wa kudhani sherehe kubwa ndo fahari ya ndoa.
  Acheni kuchangia harusi za watu wengine kwa mtindo huu usiojulikana asili yake.

  Jiandaeni kufunga harusi Private ambazo zitahusisha ndugu wa karibu tu na bajeti ndogo kabisa ya uwezo wa mfuko wako.

  Kuna harusi hapa Marekani jumla ya watu wote katika harusi ni 40 tu. ukitoa wanandoa. Pamoja na ukweli kwamba wana ndugu jamaa na marafiki debe zima.

  Kupanga ni kuchagua, hakuna mwenyenia ya wazi ya kuchagua kitu kibaya lakini tuliowengi sikuzote hushindwa kupanga, na hivyo kushindwa kuchagua.

  Sasa hawa wenye mifedha ya nguvu wanaandaa sherehe ndogo, sisi tuytemeao makalio nusu wazi tunaandaa sherehe kama wana wa Wafalme.

  Kama kuna nchi moja ilojaaa majuha waotao mchana si nyingine ni nchi yetu tukufu Tanzania.

  Nahisi Utamaduni wetu wa kuandaa sherehe zilizo zidi uwezo wetu na hamu yetu unatokana na ukweli kwamba, vipato vingi Tanzania si halali.

  Kwani viapatao vingi kwa namna moja au nyingine vina uhusiano na wizi udanganyifu na uuaji.

  Fedha haramu siku zote hutumika katika namna iliyo haramu. Kibaya zaidi fedha haramu hujenga utamaduni haramu katika jamii bila kujali mipaka.

  Watu wenye vipato halali nchini Tanzania ghafla wameshitukia wakijitumbukiza katika utamaduni haramu ambao asili yake ni ibilisi kwa kudhani kwamba wana enzi asili yao.

  Kila mtu angependa kunya mavi mengi na makubwa kwa mpigo vile afanyavyo Tembo.

  Je Kuna mwenye makalio makubwa ya kuwa na ngebe ya kumwiga Tembo huko msalani?

  Huu utaratibu wa kuazima makalio ya wengine yakusaidie huko msalani ni utamaduni gani??
   
 14. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Itisha michango kuwa umepata nafasi ya masomo nje ya nchi unaomba uchangiwe ili upate nauli ....wachache sana watakuchangia....
   
 15. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Mimi nimeishafanya uamuzi wa kutochangia harusi hovyo. Ni watu wachache tu walio karibu sana na mimi ndio ninaowachangia. Hata hivyo viwango vya kuchangia wanvyoviweka havinipi shida kwa sababu harusi za watu nisiowajua siendi hata nikipewa kadi. Kwa hiyo mimi najiamulia ni nani nimchangie na kiasi gani. Lakini uamuzi huo umenifanya nichukiwe na watu. Mimi sijali. Niko tayari kuchangia mtoto wa jirani aliyekosa au kupungukiwa karo, au mgonjwa aliye hospitalini, au mtu aliyefiwa. The paradox is mgonjwa anakaa hospitali miezi watu hawaendi kumjulia hali au wanaokwenda hawaendi na msaada wowote. Lakini akifariki hao hao wanalala kwenye msiba siku tatu au hata nne na michango wanatoa kwa mbwembwe kwa kuwa watu wanakuwa wanashuhudia. Lengo hapa ni kujitangaza na sikusaidia. It is completely irational.
   
 16. GP

  GP JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  sichangii mtu na wala sitahitaji mchango wa mtu!.
   
 17. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Huwa nasema siku zote bora hata harusi za waislam ambazo hazina complication nyingi, watu wakipiga mpunga na ndizi kazi kwisha. Utakuta mtu anabudget ya harusi ya milioni 20, halafu yeye ana milioni 1, sasa huu umekua mradi au? sasa hiyo pesa akipata yote anapeleka kwenye harusi then ikiisha wanarudi kuwa maskini. Watu kama wanaomba michango basi iwe kwa ajili ya maisha na sio kwa ajili ya kula siku moja then kwisha. Mimi Mungu akisaidia nikawa na mipango ya harusi sitawachangisha watu, na kila aliyekaribu nami nitamwalika. Hapo hapo mtu akiambiwa achangie yatima au wagonjwa wnakua wagumu sana kufanya hivyo
   
 18. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba mtu akiwa anaumwa huwa haitangazwi sana, lakini akiaga dunia ndo habari inasambazwa kwa kasi. Unaweza ukawa na moyo wa kusaidia mgonjwa lakini usipate taarifa na ghafla tu unakuja kujulishwa habari ya msiba.
   
 19. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kuna kitu kwenye kikao za harusi zinaitwa "UCHAKAVU" ina maanisha michango ya kula na kunywa pale kwenye kiao cha harusi, watu wanapiga beer na nyama choma kwenda mbele....usishangae ukatoa uchakavu 50,000 wakati umekunya beer mbili na kipande cha kuku..........hizi tuache jamani
   
 20. GP

  GP JF-Expert Member

  #20
  Nov 13, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  heeeeeeeee, yani hapo mkuu umelenga!.
  ebwana kuna kikao kimoja nilihudhuria, mshkaji alikunywa bia 4, kumbe watu wanamuangalia tu spidi yake, kufika kwenye uchakavu si akatoa 1000/=, acha akunjwe shati alipie,. hakuna usawa mie ninywe maji ya 300 mwingine anywe bia 5 halafu tutoe sawa uchakavu, Lol.
   
Loading...